ANNUUR 1228d.pdf

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    1/20

    ISSN 0856 - 3861 Na. 1228 SHAABAN 1437, IJUMAA , MEI 6 - 12, 2016  BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamu

    www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Tunajichimbia shimo-ShahariTusiwafkishe watu wakaona…

    Hawana cha kupoteza ila roho

    Tusiwagawe watu kwa dini, kabila Ukandamizaji utavunjaMuungano- Ally SalehAibua hoja ya muundo wa Shirikisho

    Sio ‘Ugaidi’ ni ubunifu Mhe. ALLY Saleh, Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF).

     Abdul Nadir Mumin.

     Mh. Riziki Shahari.

    Mtume(saw) amesema, “…Mahujaji wanalipwakwa kila walichokitumia katika Hijja, shilingimoja kwa milioni moja.” Mali ya Muislamuhuongezeka anapohiji! Unapata duniani naunafanikiwa Akhera. Wahi sasa kuja kulipauitakase mali yako. Gharama zote kwa Hijja2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhanini Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna walJamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora.Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/

    0688895777; 0765462022; 0712735363.Zanzibar: 0777468018; 0777458075;0777845010; 0777497300.

    (7) TAJIRIKA KWA KUHIJJI!

    “Haikuwa kazi rahisi kukia hapa tulipo hivi sasa. Tupo tuliokaa rumandekwa kushitakiwa kuwa tumeleta vurugu Msikitini. Kesi zimeunguruma katika

     Mahakama za mwanzo hadi kuka Mahakama Kuu.”  Soma Uk. 20

    Usione vyaelea…

    Watu wamekaa rumande!

    ANNUUR NEW.indd 1 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    2/20

    2  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

    Fethullah-Gulen

    Jee Unajua?

    CHEMSHA BONGO: 50Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

    “ISIPOKUWA, iliatimize MwenyeziMungu jambo ambalolilikuwa ni lenyekutendwa ili aangamie

    yule atakayeangamiakutokana na hojana asalimikeatakayesalimikakutokana na hoja. Nakwa hakika MwenyeziMungu ni mwenyekusikia mjuzi”. [AL-ANFAAL 42]

    Uhakika kufuatanana aya hii (Na lauangetaka Bwana wakowangeamini waliokatika ardhi wotekabisa) [Younusu99] kulikuwakunawezekana kuwana utaratibu maalumumwingine katika dunia.Isipokuwa ni kwambamatakwa ya MwenyeziMungu yamehukumiliakuwapo kwamapambano ya tangu,kati ya imani na kati yaukari kipindi chotecha maisha ya dunia.Na kunawezekanakuishuhudia hakikahii ambayo iko waziwakati wa kuichunguzahistoria ya binadamutokea Adam (a.s.)mpaka leo. Kwa msingihuo, muda wa kuwatunataka kuishi katikadunia ya imani, ni juu yetu tusisahamukitambo chochote

    kwamba sisi tutapatwana kero za ukari namabavu yake na nguvuzake, na khiyana yakena uadui wake.

    Kwa hakika uaduiwa ukari ambao

    umejijenga dhidi yaimani, unausukumaupande wa ukari kwenye kutekeleza uadui

     juu ya waumini kwasura yenye kuendelea.Kunapasa kutopatikanambele zao hisia kwambawao wanakwenda katiya watu ambao hawahisina hawatambui kituchochote ili aangamieatakayeangamiakutokana na hoja naawe hai atakayekuwahai kutokana na hoja.Kusipatikane kwa mtuyeyote udhuru mbeleya Mwenyezi Mungumtukufu na hali ya kuwa

    hawezi kusema: Nikwanini na kwa sababugani?

    Na huenda kukazukakinyume cha hayatuliyoyaelezea pundehivi, maana watakuwawaumini wenyekushindwa juu ya mamboyao na inakuwa duniaya ukari ndiyo yenyekushinda. Isipokuwamatokeo hayabadilipamoja na hali hiyo.Na haumiliki upandewalio katika pande mbilihizi udhuru wowoteambao watautoa mbeleza Bwana wao, kwa

    sababu usumbufu namapambano maalumukumeshapatikana.Kuishi nayo nakuyatenda na katikahayo ameangamiaaliyeangamia naamekuwa hai aliyekuwahai.

    Kwa ajili ya kuliwekawazi zaidi jambohili tunasema: Kwahakika MwenyeziMungu mtukufuameyafanya makundimawili yanakutanamahali ambapolau yangeahidianayangetofautiana katika

    ahadi, na ameyaandaamazingira yamapambano, na uwanjawake na mashartiambayo yameyafanya

    mapambano haya niya lazima. Umefanyika

    mpango wa jambohili upangaji ambaoumevuka uelewa wakibinadamu mpakakunapatikana kukiakwenye hatua yamapambano uso kwauso. Ikadhihirika kwauwazi wote uhai wayule ambaye anastahikikuishi, kutokana nahaja na yule ambayeanastahiki kufakutokana na ushahidina hoja, wakaporomokawanyonge na yale yoteambayo wameyabebakatika mfundo nakutopenda na chuki nakuwa mbali na unyoofuna kushiriki katikasharia. Haukubalikimbele zao udhuruwowote katika jambohili.

    Ama wale ambaohawakutenda kosalolote au uhalifuwowote, baliwamesimama tu kwakuwatia adabu waleambao wanastahikikutiwa adabu katikaBadr na mahalipengine, kuna hakikawamegusa upeo wauhakika wa maishakwa utulivu wote wamoyo, wa kiroho na wa

    kihisia.Kwa ufupi kwahakika mamboyaliyopita katika Badrina katika mapambanoyote ya mfano wa Badr,hapakubakia jamboambalo tunawezekanakulizungumzia njeya kipimo sahihi chachombo hiki. Si mbeleza wale ambao wakuuliwa mbele zawale ambao wameishi,si mbele za waleambao wamefuzuwala wale ambaowamepata hasara.Hapo hapakubakia

     jambo lolote kwasababu mambo yalipitakufuatana na vilealivyopanga MwenyeziMungu msikivu mjuzi.

    UWANJA WA VIJANA-JIONGEZEE MAARIFA 

    Suratu An-faal

    Leo ni Tarehe 28 Rajab mwaka 1437 AH, sawa na tarehe 6 May, 2016.Tarehe 6 June tunategemea kuangalia mwezi kwa Ramadhan naTarehe 7 June 2016 tukijaaliwa tutaanza Ramadhan Rasmi. Kutokeahii leo Ijumaa ya tarehe 6 May 2016 hadi kuka kuanza mfungo waRamadhani tumebakisha siku 30.

    JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA:49

    MASUALA1. Itaje Sura ipi na aya ya ngapi? ‘’ Na wote wawili wakakimbilia

    mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake Yusuf kwa nyuma. Nawakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hapana malipo yamwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewaadhabu chungu. ‘’

    2. Itaje Sura ipi na Aya ya ngapi? ‘’Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovuna khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, namkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.’’

    3. Itaje Sura na Aya ya ngapi ‘’ (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo

    ndiyo siku ya daima dawamu’4. Zipo Sura ngapi katika Qur’an?5. Zeynab, Rukaya, Ummul Kulthum, Fatma hawa ni akina nani?6. Kipando cha mnyama aliompanda Mtume Muhammad (SAW) katika

    safari ya Miraj anaitwaje?7. Vitabu vitukufu waliopewa Mitume ni Taurat, Zaboor, Injeel na ………..8. Surat Al Faatih’a ina aya ngapi?9. Unaposhukuru unatakiwa useme kalima gani?10. Kitabu cha Injeel kateremshiwa Mtume yupi?

    1. Katika vita vikuu vya Pili Duniani inakisiwa kuwa watu wapataomilioni 25 waliouwawa kwa nchi ya Urusi pekee: http://www.secondworldwarhistory.com/world-war-2-statistics.asp

    2. Bangladesh ni nchi yenye mito mingi duniani ikiwa ina mito zaidi ya 800:hps://answers.yahoo.com/question/index?qid=20120825102745AAE9akK

    3. Nchi ya Canada ina maziwa yakayo idadi ya maziwa 31,752: hp://www.zmescience.com/other/great-pics/geographical-facts-youre-not-going-to-believe-22022010/

    4. Mlima Everest unaopakana baina ya nchi ya Nepal na Tibeti ndioMlima mrefu kuliko yote: hp://www.answers.com/Q/What_country_in_the_world_has_the_most_mountains?#slide=1

    5. Nchi ya Nepal ndio nchi ilio na milima mingi duniani : hp://10mosoday.com/10-highest-mountains-in-the-world/ na hps://answers.yahoo.com/question/index?qid=20100525024502AAtXTMk

    6. Nchi ya Guyana ndio nchi inayoongoz kwa watu kujiua, kati ya watu100,000 watu 44 hujiua : hp://list25.com/25-countries-with-the-highest-

    suicide-rates-in-the-world/5/7. Nchi za Ulaya ya Mashariki ndio nchi zinazoongoza kuwa na waleviwengi, nchi ya Belarus ndio inayoongoza kwa wastani mtu mmoja hunywaLita 17.5 kwa mwaka na ulevi ndio unaochukua maisha ya watu wengi, katiya vifo vyote vinavyotokea katika nchi hio asilimia 34 hutokana na ulevi :hp://www.marketwatch.com/story/10-countries-where-people-drink-the-most-2014-05-30?page=5

    8. Nchi ambazo Pombe zimepiga marufuku kati ya hizo ni Falme zanchi za KiarabuUAE, Iran, Iraq, Libya, Saudi Arabia, Bangladesh, Brunei: hp://www.thedailymeal.com/drink/10-countries-where-alcohol-illegal-slideshow/slide-4

    9. Nchi 10 zinazopendwa kufanya uchawi ni Nigeria, Zambia, Malawi,Kenya, Congo DRC, Ghana, Uganda, Papua New Guinea, Gambia naTanzania : hp://kkdaniels.blogspot.com/2015/08/top-10-african-countries-at-practicing.html

    10. Mexico ndio nchi inayoongoza kuwa na wizi mwingi duniani : hp://www.insidermonkey.com/blog/11-countries-with-the-highest-rates-of-identity-theft-in-the-world-351940/

    (Kutokana na kutokuwa na wasomaji wengi katika Ukumbi waUwanja wa Maarifa na kutopata majibu ya kuuboresha huu wa Uwanjawa Maarifa, tunakiria kuanzisha ukumbi mwengine. Tuma barua [email protected] au ujumbe mfupi kupitia simu 0777436949 unahisininii uwe mbadala wake?)

    M A I D I E R Y 3:154 Y Z Y Z

    U S S A S E P O 40 A A U A

    S D H U H F E S 41 K Q S K

    S F A D A V T F 42 O Q U A

     A G Q na Q B Y V 43 O U F R

     J H na S na N U G 44 B M A I

    U I I U Y M I Y 45 na W I Y

    M JK B L A V O U 46 Y A S A

     A L R E K B K I 47 U S H na

     A M A I O V D O 48 S D A Y

    I N H M O C S P 94:5-6 U C V A

    L O I A B D W W 25 F V B H

    O P M N Y S E E 55 P G N Y

    P Q V L Z A R R 5 Y S E A

     AN R Z C C W Z T 40:68 U E G U

     W A I E A 12:25 D I Q U R A N

     A L S D L 7:30 A N T T A R O

    T H S F F 8:9 U A H A T A U

    O A A G A 7:22 D I A M A Y R

    T M E Y A 50:34 S N M R B A E

    O D M I T 914 U S U T T A D

    M U U U I 114 I A D E A N Y

    T L S Y H 22 B U R A Q Y Y

    U I S T A 7 Y N T N T U H

    M L A R U 49:6 N N U D N J N

    E H P R X C V B N M K L I

    S R A T H A S D F G H J K

     A H A T U P P P S F H U O

     W N N Y D E R T U O P Y Z

    I M U I A L A M A L I F H

    Mwandamo wa mwezi

    ANNUUR NEW.indd 2 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    3/20

    3  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Habari

    Tunajichimbia shimo-ShahariUMEPIGWA mfano kwambaviongozi wa serikaliwamekuwa kama walewaliotajwa katika vitabu vyadini kwamba mioyo wanayo,lakini hawataki kufahamukwayo, macho wanayo, lakinihawataki kuona kwayo kamaambavyo wana masikio,lakini hawasikii kwayo.

    Hiyo ni kutokana nakuyafumbia macho madai yaWaislamu bila ya kuyatafutiaufumbuzi halikadhalikakwenda kinyume na kanuniza haki, uadilifu na utawala bora kwa ujumla.

    Yakatajwa baadhi yamadai ya Waislamu kuwani pamoja na MoU, utendajiwa baadhi ya watumishi waNECTA, pamoja na suala laMasheikh wanaoshikiliwakwa miaka mitatu sasa bilakesi zao kuzungumzwawala kujulikana hatma yao.Kwamba kosa lao nini?

    Tahadhari hiyo imetolewaBungeni mjini Dodoma naMbunge wa Viti Maalum waMaa, kupitia Chama ChaWananchi CUF, Bi. RizikiShahari akichangia hotubaya Osi ya Rais, Tamisemi naUtawala Bora, katika Bunge la

    Bajeti linaloendea hivi sasa.Mh. Riziki, akichangiahotuba hiyo, alipinga uwepowa Utawala Bora nchini,akihoji ni utawala bora ganiambao haujali watu wake nahauzingatii misingi ya haki za binadamu na hata kupuuzawatu wake.

    Akasema, ni jambo lakusikitisha kuwa viongozi waserikali wanaojigamba kuwawaadilifu na wanaofuatahaki na utawala bora, lakiniinapokuja suala la Waislamuwanakwenda kinyume kabisa.

    “Kwa hali hii mnatakaWaislamu wasimame wapi na

    waielewe vipi Serikali hii, hivihawa Waislamu si sehemu ya jamii ya wanchi wa nchi hii?”

    “Utawala bora ganiusiofanyia kazi madai ya watuwake. Kwa mwenendo huutuelewe kuwa tunajichimbiashimo wenyewe natutaangamia.” Amesema Mh.Riziki na kutahadharisha.

    Mh. Riziki, akahoji nakuweka wazi zaidi kwambani jambo la kushangaza iwapowanazungumzia Utawala

    Na Bakari Mwakangwale Bora, huku utawala wenyeweukiwa na watumishi ambao

    wanawagawa wananchi waokatika makundi ya kiitikadi nakidini jambo ambalo ni hatari.

    Aidha, Bi. Riziki,akalieleza Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano waTanzania, kwamba Bungehilo lilishaambiwa mudamrefu kuwa Waislamuwanalalamikia sualala ‘Memorandum ofUnderstanding’ (MoU)kwamba kuna pesa zinatolewana Serikali kwa upandemmoja wa dini vipi kuhusuwao, lakini akasema hakunamajibu wanayopewa zaidi yakuambulia kejeli.

    Si hayo tu, lakini piaakasema, Waislamu hao

    hao walilalamikia Baraza laMitihani la Taifa (NECTA) juu ya (aliyekuwa) MtendajiMkuu na Serikali iliundakamati ya uchunguzi, lakinihawakueleza chochote mpakasasa badala yake mtu huyohuyo amewekwa juu nambaya zaidi katika eneo lilelilela elimu, alilolalamikiwa na jamii ya Waislamu.

    “Ifahamike kwamba binadaamu akikishwamahala ambapo anaonahana cha kupoteza ila rohoyake, haoni thamani hataya hiyo roho yenyewe, rohoina thamani kama maisha

    yake yatakuwa na thamanipia lakini kama ataishi kwa

    mashaka na uonevu ni hatari”.Amesema Bi. Riziki.Awali, kabla ya kuanza

    kuchangia hutoba hiyo, alitoanasaha zake kwa wabungewenzake waliotanguliakuchangia hotuba hiyoakisema, inaonekanaWabunge wengi wanaonekanakukata tamaa kufuatiakuzungumza maswalahayo hayo kila awamu bilakufanyiwa kazi.

    Akasema, hakuna sababu yakukata tamaa, bali washikamanena amri ya kutoa nasaha nakukum busha kama vitabu vyaDini vinavyoagiza.

    IMEELEZWA kuwa kamagharama ya muungano nikukandamiza demokrasiaZanzibar, basi hiyo itakuwapia ndio sababu ya uhakika yakuuvunja Muungano wenyewe.

    Hayo yamesemwa na WaziriKivuli na Msemaji Mkuu waKambi Rasmi ya UpinzaniBungeni katika Osi yaMakamu wa Rais-Muungano,Mheshimiwa Ally Saleh (MB).

    Ally Saleh, ambaye piani Mbunge wa Jimbo la MjiMkongwe, amesema hayomapema wiki hii akichangiahotuba ya bajeti ya Osi yaMakamu wa Rais – Muunganona Mazingira.

    Mheshimiwa Saleh katikahotuba yake amedai kuwa,Serikali ya Tanzania imekuwamsemaji hodari wa demokrasiaza wengine, huku ikiendeshaukandamizaji wa demokrasiaZanzibar kwa lengo la kukilindachama tawala, CCM na serikaliyake.

    Akatoa mfano wa uchaguziuliopita ambapo alidai kuwailitumika hadaa na njia haramukupindua matakwa ya wananchi,ukaletwa uchaguzi kiini macho

    na matokeo ya kuupika.Ally Saleh akasema, ulikuwani uvunjaji wa wazi wa katibana sheria ya uchaguzi, lakini

     badala ya serikali ya muunganokusimamia haki, ikaja navisingizio kwamba hainamamlaka ya kuingilia Tume yaUchaguzi Zanzibar.

    Hata hivyo akasema kuwa,wakati ikileta madai hayo,ikatumia jeshi kuzima matakwaya wananchi na kusimamia batilikutendeka.

    Tumekuwa “hodari kusemeaukandamizaji wa demokrasiakatika nchi nyingine, lakini

    Ukandamizaji utavunja Muungano-Ally SalehNa Mwandishi Wetu kwetu tunaendelea kujivika

    ‘kilemba cha ukoka’ kwamba;sisi ni kisiwa cha amani wakatikilichopo ni utawala wa kibabe.”

    Alisema Ally Saleh nakuongeza kuwa “Serikali yaTanganyika (Tanzania) inayojidaikwamba ndiyo ya Muungano,imesimamia kuvunjwa kwaKatiba ya Zanzibar kwakuiweka kwa nguvu Serikali…huko Zanzibar” kinyumena matakwa ya Wazanzibariwaliyoyadhihirisha Oktoba 20,2015.

    Akasisitiza kuwa “kulikuwahakuna msingi wowote wakikatiba wala kisheria wakufuta uchaguzi wa Zanzibarambao ulifanyika kwa amani nawashindi kutangazwa na kupewashahada za ushindi.”

    Katika kuonyesha kuwa kunamambo mengi ya kujadiliwaili kuweka mazingira mazurikuhakikisha kuwa muunganounadumu, Ally Saleh alisemakuwa serikali ya Tanganyika,iliyojivika koti la Muungano,inaonekana kama mkolonianayeinyonya Zanzibar.

    Akasema, ni kutokana na surahiyo inayojitokeza, Muunganounakosa ridhaa ya wananchina hivyo serikali kulazimika

    kutumia jeshi kuulazimisha.“Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inatoa rai kwa Serikalihii ya awamu ya tano kwamba;kama kweli ina nia ya kuuenzina kuudumisha Muungano, basiizingatie maoni ya wananchiwaliyoyatoa kwenye Tume yaMabadiliko ya Katiba kuhusumuundo wa Muungano ili kuwana Muungano unaoridhiwa nawananchi wa pande zote mbili zaMuungano.” Alisema.

    Kwa upande mwingine AllySaleh akahoji juu ya vitendovinavyofanywa na vikosi pamojana wanaoitwa ‘Mazombie’ vya

    kupiga watu na kuharibu mali.Hayo yote yakionekana

    kuwa yana baraka za serikalikwa vile hakuna hatua zozotezinazochukuliwa dhidi ya jinaizinazofanywa na makundi hayo.

    Akahoji, inakuwaje mambohayo kufanywa hadharanilakini, Jeshi la Polisi chombo chaMuungano, limekuwa likisemahalijui kama kuna makundi hayona wala vitendo vyao.

    “Naibu Waziri wa Mambo yaNdani (Mh.) Hamad Masaunina Waziri wa Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa, Dk. HusseinMwinyi wamesema eti hawajuichochote kuhusu matendo hayoya dhulma ya wale wanaoitwaMazombie.”

    Lakini “wakati Panya Roadilipotikisa Dar es Salaamilichukua muda mchache tukufyagiwa wote, hata manyoyayao hayakuonekana.”

    Akahoji, vipi la mazombielishindikane, hali ambayoinajenga dhana kuwambahuenda vitendo vyao vyakihalifu na jinai, vinainufaishaCCM Zanzibar, na ndiomaana Serikali ya Muunganoimelinyamazia kimya.

    Kwa upande mwingine, AllySaleh akaonyesha wasiwasi

    wake juu ya uwepo wa kesi zakubambikiwa ambapo akadaikuwa, jeshi la polisi limekuwalikiwakamata raia wema alimradini wanachama au wapenzi waCUF na kuwabambika kesi zauongo.

    Akatoa mfano kuwa katikakipindi cha uchaguzi Zanzibar,takriban watu 250 walikamatwana polisi wakiwemo viongoziwakuu wa CUF.

    Akasema, ni katika mkumbohuo, walikumbwa NaibuKatibu Mkuu wa CUF Nassor

    Inaendelea Uk. 4

    ANNUUR NEW.indd 3 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    4/20

    4  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Tahariri/Makala

    AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

    Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.www.annuurpapers.co. E-mail: [email protected]

    Ofsi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    TUNACHUKUAfursa hii kukumbushaWaislamu kwa ufupikuhusiana na kupotezamaadili (kupoteamwelekeo tulioachiwana Mtume (s.a.w.) kamaalivyoamrishwa naAllah (s.w.) atukishie.Na yeye amefukishia.

    Ni dhahirikwamba Waislamuwameupoteza uleUislamu tuliofundishwana Mtume (s.a.w.) iwe

    ni kwa kujua au kwakutokujua.Waislamu hawana

    umoja, wamejigawamakundi kwa makundina kujengeana uadui waokwa wao, hali yakuwawameisahau kauli yaAllah (s.w.):

     “Na shikamanenikatika kamba ya Allah(s.w.) wala msiachane.”(Qur. 3:103).

    Kwa mtazamo wamafundosho ya Qur’an,kujigawa makundihakutaiepuka adhabu(kwa Allah (s.w.) kamaalivyosema Allah (s.w.).

      "Tumeiteremshaadhabu kwa walewaliojigawa makundi".(Qur. 15:90).

    Hatudhani kuwa jamiiya Waislamu hususanviongozi wa taasisi namashirika mbalimbali yaWaislamu hawajui ayahazi na makusudio yake.Lakini matokeo ya kibri,

     jeuri, hasad na tamaazimewakisha Waislamuhapa walipo.

    Tujiulize katika maishaya Mtume (s.a.w.)yalikuwepo makundikama haya tuliyojiundiasisi? Kama yalikuwepo,

     juhudi gani zilifanyikakuyamaliza na Waislamuwakabaki kitu kimoja?

    Tunaona katikamazingira tuliyo nayosasa, ni dhahiri kwambatumepoteza mwelekeowa Uislamu na maadiliyake, sheria na Tawhiid,na kukubali kuchezewakama mwanasesere(toy) na makari kupitiaudhaifu huu.

    Amewahi kusemaMtume (s.a.w.),"Atakayeishi muda mrefu(Maswahaba) ataonamambo mengi ya uzushina jiuepusheni nayo."

    Kauli hii ya Mtume(s.a.w.) imetimia maana

    Tuache kibri tujengeumoja kwa Waislamuumma wa Kiislamuumetopea katikauovu na uzushi kamatunavyoshuhudiaWaislamu wakijigawakatika makundi nakujengeana uhasama nakupoteza umoja wao waKiislamu.

    Huu si Uislamualiotuletea Allah (s.w.)kupitia kwa Mjumbewake. Tunajiuliza, kwa

     jinsi hali ilivyo hapanchini ni nani ataunusuru

    Uislamu (dini hii yaMwenyezi Mungu) kamainavyosema Qur’an, "Ninani atakayeinusuru dinihii". (Qur. 61:14).

    Wako wapi wanazuoniwa Kiislamu, viongoziwa Kiislamu, Masheikh,Maulamaa, Maimam,ambao kimsingi ndiodira katika kusimamiamiongozo ya dini, ndiowanaotegemewa kujengaumoja wa jamii yaKiislamu nchini.

    Tukumbuke kuwaUislamu ni dhamanatuliyoyopewa naMuumba na kuamuruwatu waishi katikaustaarabu wake.Ameeleza MwenyeziMungu: "TumekuridhieniUislamu kuwa diniyenu." (Qur. 5:3).

    Ni vipi tumeuachaustaarabu wa Uislamuambao Allah (s.w.)ameturidhia, kiasi chakubaki katika Uislamuwa vipande vipande haliya kuwa viongozi wapo?

    Umoja katika Uislamuhapa nchini umepigiwakelele sana. Zimeelezwaathari walizopatana wanazoendeleakupata Waislamu kwakuwekwa kwao katikamafungu mafungu, tenayanayohasimiana.

    Lakini pamoja nakudhihiri athari nakufahamika kiini chatatizo, bado hadi sasahakuna hatua zozote zauhakika zilizochukuliwakunusuru hali.

    Tunaona wakatiumeka wa hatua zamakusudi na za harakakuchukuliwa. BARAZAKUU, BAKWATA,MABARAZA yaWANAZUONI na Taasisinyingine za Kiislamunchini, pamoja na tofautizao za kifalsafa. Kunahaja ya kuketi na kuwekamkakati wa pamoja wa

    kutengeneza jamii mojaya Waislamu nchini.

    Tukiacha kibri na jeuri,tamaa za maslahi binafsi,chuki na husda, hililitawezekana na utakuwamwanzo mzuri kuitimizaaya ya Qur’an:

    “Na shikamaneni

    katika kamba ya Allah(s.w.) wala msiachane.(Msifarikiane).” (Qur.3:103).

    Kama ni tofauti zenu

    za kifalsafa katikataasisi zenu bakininazo, vumilianeni naheshimianeni kwazo,lakini hakuna haja yatofauti zenu hizo ziwesababu ya kuendeleakuwagawa Waislamu.

    Ikiwa mtabaini

    mapema na kutahayarina kuchukua hatua,mtaunusuru Uislamukwa kuweka kipaumbelecha umoja wao kwanza,

    maslahi ya taasisi baadae.Tunaamini ikikosekana

     jamii ya Kiislamuiliyojengwa katikamisingi madhubuti yaumoja, hakuna taasisimadhubuti ya Kiislamuitakayoweza kufaulukatika malengo yake

    kama ilivyokusudiwa.Kama taasisi zenu nikwa ajili ya Waislamu,

     basi ni vyema mkajengaudugu wao kwanza.

    Ukandamizaji utavunja Muungano-Ally SalehInatoka Uk. 3

    Mazrui na wajumbewa Kampeni MansourHimid na MuhammedRiamy, ambapo wapowaliobambikiziwa kesi zakuchoma moto nyumba,na matukio ya ulipuaji

    wa mabomu.Kuhusu kero zaMuungano, Ally Salehalisema kuwa kero hizozimeendelea kuwepo“kwa sababu ya kukosadhamira ya kweli yakisiasa, na muundousiokidhi haja.”

    Kwa sababu hiyo,“Muungano umekuwana matatizo mengi namengine yakidumu kadriya umri wa Muunganowenyewe.”

    “Muungano huuumekosa taratibu zakikatiba na kisheria zakutatua migongano,mivutano au uchukuajiwa madaraka (Usurp ofPower) unaofanywa naSerikali ya Muunganodhidi ya Zanzibar nakadhalika Zanzibarinapojitutumua kudaihaki na stahiki zakekatika Muunganoambazo hazitimizwi,”alisema.

    Akadai kuwa fursaadhimu ya kutengenezamfumo mzuri waMuungano ilipatikanakupitia Mapendekezo yaTume ya Warioba, lakiniCCM wakaipiga teke niahiyo kupitia Bunge laKatiba na kuleta mamboambayo yataendelezakero kama zilivyokuwa

    na kuzidi.“Mheshimiwa Spika,Wengi tunaamini hizozinazoitwa KERO zaMuungano zinatumikakama mtaji wa kisiasana kila zinapobakia aukuzuka nyingine nazisipatiwe suluhu, ndipomtaji huo unapokuwamkubwa zaidi. Mtaji huuunatumika kuwazugawatu, yaani Watanzaniakuwa kero ni sehemuya Muungano na kuwazote zimetatuliwaisipokuwa chache tu,

    yaani kuwaaminishaWatanzania kuwaMuungano ni wa usawana wa haki ilhali hakuna

    nia kabisa ya kumalizakero za Muungano.”Alisema Waziri huyoKivuli.

    “Mheshimiwa Spika,aliyekuwa MsemajiMkuu wa Kambi Rasmiya Upinzani Bungenikatika Bunge la kumi,Mheshimiwa TunduLissu alizungumziakwa kina juu ya suala laMgawano wa Mapato yaMuungano na jinsi Zanzibarinavyopunjika na jinsimfumo huo ulivyogeuzaZanzibar kuwa koloni. Hiloni katika suala la fedhaambazo zinatokana nawafadhili yaani mgao waasilimia 4.5.

    Mheshimiwa Spika,pamoja na takwimukuonyesha kuwa kiasifulani cha fedha hupelekwaZanzibar, lakini bado

    kiwango hakijakia asilimiaambayo imekubalika napande hizo mbili ambapokiwango hicho hakijawahikuvuka asilimia 2.8. Tatizohili limekuwa la nenda rudimiaka mingi bila suluhu yakweli na ya kudumu.

    Mheshimiwa Spika,Kwa mujibu wa hotubaya Mheshimiwa Lissu,fedha hizo hujumuisha piamakandokando menginekadhaa ila hutajwa nakutiwa katika kapumoja ambalo huonekanalimenona.

    Alisema kwa mwaka juzi Zanzibar iliyopaswakupokea shs billion71.23 ilipewa asilimiakumi tu ya fedha hizo.Inasikitisha kwamba;Ripoti ya Utekelezaji ya

    Osi ya Makamu waRais iliyopelekwa katikaKamati ya Katiba na Sheria,haikugusia chochote juuya eneo hili muhimula masuala ya fedha zaMuungano na mgawanyowake.

    Mheshimiwa Spika, Kitukingine kinachohusu fedhaambacho kwa kukosekanania ya kisiasa hakijapatiwaufumbuzi pamoja nakuundwa kwa Tume yaPamoja ya Fedha ya Jamhuriya Muungano ya 1984 nisuala la sehemu ya Zanzibarkatika mtaji uliounda Benki

    Nukuu ya Ally Saleh juu ya Mgawo wa Mapato.Kuu ya Tanzania ikiwa nifedha za Zanzibar kutokanana iliyokuwa Bodi ya Sarafuya Afrika Mashariki. Leomiaka 50 tangu kuundwakwa Benki Kuu, hakunasuluhu ya suala hilo.

    Suala hilo maarufu kamaHisa za Zanzibar, lilitolewaagizo na Bunge kwa Serikalikuleta Bungeni taarifayake, lakini limepuuzwa naZanzibar haijapata fedhazake halali. Kisingizio nikutopata taarifa jamboambalo linatia khofu kuwataarifa hizo hazitapatikanatena.

    Mheshimiwa Spika,kimsingi kuna utatamkubwa juu ya mgawanyona matumizi ya fedhaza Muungano. Ripoti ya

    Tume ya Pamoja ya Fedhaimesema wazi kuwakiasi kikubwa cha fedhaza Muungano hutumikakwa mambo yasio yaMuungano, lakini Serikaliya Muungano imekuwaikikalia mapendekezo yakutenganisha matumizi yafedha za Muungano, ikijuainaidhulumu Zanzibar.

    Mheshimiwa Spika,kero za Muunganozinazidi kuongezekakutokana na uzembewa viongozi waliopewadhamana ya kuusimamiamuungano. Maamuzikuhusu masuala muhimuya muungano kama vileajira za Wazanzibarikatika Muungano au

    ushirikiano wa Zanzibarna taasisi za kimataifa, auutozaji kodi mara mbilikwa wafanyabiashara waZanzibar yanachukuamuda mrefu mno kiasi chakuongeza kero juu ya zilezilizokuwepo toka mwanzo.

    Ndio maana, kutokanana kero hizi zisizo nautatuzi Wazanzibari,katika maoni ya Tume yaWarioba wakataka tuwe naSerikali ya Mkataba jamboambalo liliungwa mkonona Tume hiyo kwa kuja napendekezo la muundo washirikisho katika Jamhuri yaTanzania.”

    ANNUUR NEW.indd 4 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    5/20

    5  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016HABARI ZA KIMATAIFA

    Chama cha siasa nchiniUjerumani kinachopingaUislamu nchini Ujerumani,wiki hii kimepata upinzanimkubwa kutoka kwamamia ya waandamanajiwanaopinga sera za chuki zachama hicho.

    Polisi nchini Ujerumaniwamewazuia mamia yawaandamanaji wanaopingachama cha mrengo wa kuliacha AFD, chenye sera zakupiga vita Uislamu.

    Polisi wametumia majiwa kuwasha kuwatawanyawaandamanaji waliobebamabango na kuchomamoto matairi katika eneo lakuingilia kwenye mkutanowa chama hicho, ili kuwazuiawanachamana wake.

    Hali hiyo ililazimu maasazaidi ya 1000 kutumwa katikaeneo la mkutano katika mjiwa Stugart kutoa ulinzi.

    AFD kinatarajiwa kuzindua

    Ujerumani waandamana

    kupinga wapinga adhana

    KIONGOZI wa AFD-Frauke-Petry.

    upya kampeni zake nakutangaza wazi kuwakinapinga dini ya Kiislamu.

    Chama hicho kimekuwakikipiga marufuku mwito waWaislamu katika swala yaaniadhana, vazi la burga, uwepowa minara ya Misikiti.irib.

    SAUDI Arabia imesemahuenda ikafungua ubaloziwake mjini Tel AvivIsrael, iwapo utawala waIsrael utakubali kusitishamgogoro katika eneo laMashariki ya Kati.

     Jenerali Anwar Eshki,kamanda mwandamizi wazamani wa jeshi la Al-Saud,ameiambia televisheni yaal-Jazeera ya Qatar kuwa,iwapo Waziri Mkuu waIsrael Benjamin Netanyahu,atakubali mpango huowa kusitisha mgogoro na

    kuwapa Wapalestina hakizao zote, basi Saudi Arabiaitafungua ubalozi Tel Aviv.

     Jenerali Eshki, ambayekwa sasa ni Mwenyekitiwa Kituo cha Mafunzo yaKiistratejia na Sheria chaMashariki ya Kati kilichoko Jeddah, ameongeza kuwautawala wa Al-Saudhauna haja ya kushinikizakutengwa utawala waIsrael katika eneo hili laMashariki ya Kati.

    Itakumbukwa kuwamwaka 2002, Saudia

    kwa mara ya kwanzailipendekeza kuwaiwapo utawala wa Israelutawaagiza walowezi waKizayuni kuondoke katikaUkingo wa Magharibi waMto Jordan na Ukanda waGaza, basi utazishawishinchi nyingine za Kiarabukuutambua utawala huodhalimu.

    Hata hivyo kamandahuyo wa zamani wa jeshi laAl-Saud na ambaye aliwahikuwa mshauri wa MwanaMfalme wa Al-Saud naaliyekuwa balozi wa Saudianchini Marekani, BandarBin Sultan, alikwepakujibu swali alipotakiwakufafanua ni kwa niniutawala wa Saudiaumetuma vikosi nchiniYemen na umeshindwakutuma vikosi katikaUkanda wa Gaza ilikuwalinda Wapalestina.

    Zaidi ya watu 8,280wameuawa wakiwemowatoto 2,236 tangu Saudia

    Saudia kufungua ubalozi IsraelMahusiano ya siri yaimarika

    na washirika wakewaanzishe mashambuliziya anga dhidi ya YemenMachi mwaka jana, kwalengo la kumrejeshamadarakani Rais wa nchihiyo aliyekimbia AbdRabbu Mansur Hadi.

    Wakati kukiwa nawasiwasi kuhusu ukaribuwa Saudia na Israel, kunataarifa kwamba utawalaharamu wa Israel unatoamafunzo ya kijeshi kwaaskari wa Saudi Arabiakatika mpango wa siri wa

    uhusiano wa tawala hizombili.Naibu Katibu Mkuu

    wa Hizbullah ya LebanonSheikh Naim Qassem,amechua kuwa maasawa Saudi wanapatamafunzo kufuatia uhusianowa siri wa Israel na Saudia,ambao sasa umeimarikana kuwa ushirikiano wakijeshi.

    Imeelezwa kuwa Israelimeamua kuwapa mafunzoaskari wa Saudia baadaya utawala wa Saudia

    kushinikiza Jumuiyaya Nchi za Kiarabu naBarazala la Ushirikianola Ghuba ya Uajemikuitangaza harakati yaHizbullah kuwa kundi lakigaidi.

    Wakati ushirika huoukionekana kuimarika kwasasa, kwa miaka mingiSaudia imejizuia kutoamafunzo na misaada yakekwa wanaharakati wakupigania ukombozi waPalestina.

    Siku ya Jumapili, gazeti laKizayuni la Jerusalem Postliliripoti kuwa, “si tu kuwaIsrael haijatengwa bali piasasa imeingizwa katikaduara la Saudi Arabia.Sehemu ya mpango huoni Israel kufungua osi yakidiplomasia Abu Dhabi nakuimarisha maingiliano nanchi za Ghuba ya Uajemi."

    Kwa mujibu wa tovutiya Bloomberg, mikutanokadhaa ya siri imekuwaikifanyika kati ya maasa

    wa Saudia na Israel.

    Imeelezwa kuwa pandehizo mbili zimekutanamara tano katika kipindicha miezi 17 mwaka 2014-1015, ambapo maasa haowa Saudia na wa utawalawa Israel walikutana kwanyakati tofauti nchini India,Italia na Jamhuri ya Czech.

    Aidha mapema mwezi Juni mwaka jana, maasamashuhuri wa zamani wa

    Saudia na Israel walikutana

    katika taasisi ya Councilon Foreign Relations hukoWashington. Kikao hichokilihudhuriwa na AnwarMajed Eshki, mshauriwa zamani wa serikali yaSaudia, na Dore Gold baloziwa zamani wa Israel aliyekaribu na Waziri Mkuuwa Utawala wa KizayuniBenjamin Netanyahu.

    WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kushoto) na MfalmeSalman wa Saudi Arabia.

    ANNUUR NEW.indd 5 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    6/20

    6  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Makala

    STAREHE inapozidi akiliya mwanadamu, basi hatalile linalodhuru hulifumbiamacho au hulifunikapazia ili lisimshughulisheau kumrudisha nyumaau kuzuwia azma yake.Starehe pia ina kawaida yakumsahaulisha mwanadamukutenda yaliyo ya heri naya msingi kwa maisha yakena kwa kukosa ya hofuMwenyezi Mungu pia.

    Starehe ikikolea, humfanyamwanadamu kuishi kwakujipangia atakavyo kama

    vile hakuna anayedhibitimaisha na uhai wake. Ilehali ya mtu kustarehe hadikukinai, akalala na akaamkasalama, humpa kibri na jeurina kujihakikishia salama yakuiona kesho na kesho kutwana kujiamini kuwa uhaiutaendelea kuwepo maishaya starehe yataendela kamakawaida.

    Katika hali ya kawaida,starehe humfumba machomwanadamu hata paleumri wake utakapopea,humfanya asigundue udhaifuwa kizee hata pale maungoyatakapokataa kunyambukavyema na nywele kubadilikarangi na uzee kuingia.

    Mara nyingi starehehunogeshwa zaidi na hulkaza kivivu na kupenda urahisi.Inapokolea humfanya mtuasahau anakotoka, alikona anakoelekea na zaidianasahau aliyemneemeshapia. Na hata kamaameruzukiwa, ni vigumukwake kukumbuka kuwawako wenye kudhikishwa,ambao ujira wao ni sehemuya ruzuku yake.

    Mara nyingi stareheikimkolea mtu, Ibilisi

    anakuwa ndiye raki wakaribu kwake. Wakatimwingine humfanya mtuakajitafsiria mambo kinyume,ili kukidhi matamanio yake.Kawaida hujenga mazoea.Starehe ukiizoea, hujengapumbazo kikra na hali hiihumfanya mtu kuchaguakile tu anachoona kitakidhimatamanio yake.

    Hata Firauni katika utawalawake wa kiovu kule Misri,aliponzwa na kibri, jeuri na

    Tusikubali kutekwa na starehe za duniaStarehe kamili ipo akhera

    Na Shaban Rajab starehe kiasi kwamba hakuwatayari kuona kuna mtawalazaidi yake yeye. Alilewastarehe za madaraka, alipatautii wa shuruti, kila alichotakaalipatiwa, akalemaa kiasicha kumfanyia kibri hataMwenyezi Mungu Muumbana yeye akajiita mungu.Alilewa starehe na kulemaa,lakini Anayemiliki uhai waviumbe alimtafuna mithiliya gogo linalomung’unywana mchwa ndani kwandani hata linapotanabahi,mambo yalishaharibika.Alimeangamia.

    Tufahamu kwambakustarehe si dhambi walakosa. Lakini starehe shartiziwe za halali, kwa wakatina kwa kiasi. Tatizo nipale zinapozidi na kukosamipaka kiasi cha kufanyamaasi. Tatizo ni pale stareheinapogeuzwa kuwa ndiomfumo wa maisha kiasi chamtu kuhadaika kwazo nakuwa pumbao na kuadhirimfumo sahihi wa maishaaliouridhia MwenyeziMungu.

    Wale ambao wamehadaikana kutopea katika starehe, nivyema kurudi katika misingi

    ya maisha kwa kuzoea maishaya uwastani na ya kiasi hukuwakiwa na hakika kwamba,Mwenyezi Mungu ndiyemkadiriaji wa kila jambo.

    Ifahamike kwamba maishaya hapa duniani ni mchezowa muda tu na pumbao.Kuonyeshana ufahari kwalengo la kupata sifa na kutakakuheshimiwa, kushindanakukithiri katika mali nawatoto ni kama mfano wamvua inayowafurahishawakulima kwa mimea yao,kisha inasita. Furaha yamkulima wakati wa kunyeshamvua ni kustawi mimea yake.

    Lakini hugeuka kilio palemvua ikatikapo na mimea(mazao) kuwa na rangi yanjano, kisha inajisokota nahatimaye hukauka.

    Vile vile kwa kuendekezastarehe kupitiliza katikakipindi kifupi cha uhai,kunawafanya watu kusahaukuwa akhera (kuna)adhabu kali. Ni vyemawale waliozoea starehe nakuonyesha fahari wakatiayakini akilini kwamba, kila

     jambo linatendeka kwa kiasina lina wakati wake, nafasiyake na malipo yake.

    Ni vyema walewalioathiriwa na mazoeahaya wakajitambua mapemana kubadilika kwanianayetubu na kubadilikakwa dhati, Mola huleta radhizake. Maisha ya dunia sichochote isipokuwa ni sterehedanganyifu.

    Kujamiinana (katikamahusiano ya ndoa halali)ni aina pia ya starehe. Njeya ndoa ni starehe ya kiovu.

    Ulevi pia ni starehe ovu,maonyesho ya urembo,kamari, night clubs nk.Michezo ni mazoezi na ainaya starehe kwa watu wengine.Kulala kunaweza kuwa ainaya starehe kwa baadhi yawatu, japo kila mtu ni lazimaalale. Maana ya starehe nikitu au jambo ambalo mtukwa hiari yake hupendakulifanya, ili kuiburudisha nakuiridhisha nafsi yake.

    Namna ya kuiridhisha nafsikunatofutiana baina ya mtuna mtu na hapo ndipo kilamtu anapokuwa na starehe

    yake. Hata hivyo kupendawanawake, watoto na malisi vibaya na wala MwenyeziMungu hajaharamisha.Tahadhari ni mapenzihayo yasije kuwa sababuya kukufuru, kuendekezalaghawi na israaf nk.

    Starehe mara nyingi huendasambamba na matamanio.Matamanio ni hisia za kupatavile unavyovipendelea nakuhisi raha (kustarehe)

    unapovipata. Hulka yamwenye kutamani maranyingi hatosheki. Akipatamia anatamani kupata namia nyingine. Kadhalikaaliyetopea kwa starehehakinahi. Akistarehe leo nakesho atataka aendelee nastarehe nyingine.

    Binadamu anaweza kuwana raha kama atabarikiwakuwa na vitu vinavyoonekanakuwa ni vya msingi hapaduniani kama afya, mali, mke,watoto, hadhi (heshima).

    Lakini raha hii kwa binadamuni kwa wakati au kipindifulani tu, si kwa mudawote. Hali hii inajitokezakwasababu ni vigumu binadamu kufurahi mudawote wa maisha yake, kwakuwa hana pa kuziwekahisia za matatizo ya kiduniakama vile hofu na wasiwasina hali ya kutotosheka aukuridhika, matatizo ya uzao,ya nyumbani nk.

    Kwa maana hiyo, rahakamili katika maisha ya binadamu hapa dunianikamwe haiwezi kupatikana.Labda katika maisha mengine baada ya yale ya dunia. Rahaau starehe wanazowezakuambulia wanadamu katikamaisha ya duniani ni rahakwa wakati fulani tu.

    Mwenyezi Mungutunakuomba uilinde jamiiyetu na starehe potofu,ijaalie kufuata njia ya haki nakuionyesha popote ilipo batilili waikimbie na uiwezeshekuifuata haki ilipo iliutunusuru (Amiin).

    ANNUUR NEW.indd 6 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    7/20

    7  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Hoja ya Visram

    RAIS wa Marekani BarackObama amekiri kwa maraya kwanza kwamba serikaliyake ilishindwa katikauvamizi wa Libya mwaka2011. Amesema hilo huendandilo “kosa kubwa” zaidialilolitenda wakati wa utawalawake. Bw Obama amesemaMarekani haikua na mpangomahususi wa jinsi Libyaitakavyotawaliwa baada yakuuliwa kwa mtawala wakeKanali Muammar Gaddatarehe 20 Oktoba 2011.Obama alisema haya katikamahojiano ya hivi majuzi naruninga nchini Marekani.Matokeo yake ni kuwa Libyaimetumbukia katika dimbwila matatizo baada ya nchi hiyokusambaratika.

    Mwanzoni NATO walidaikuwa lengo lao lilikuwa nikuwalinda raia wa Libya ili

    wasishambuliwe na majeshi yaGadda. Lakini baada ya mudawakaamua wampindue Gaddana kuikabidhi nchi kwa waasi.Siku za nyuma Obama amewahikuwalaumu wenzake wa NATO.Amesema waziri mkuu waUingereza, Bw David Cameronhakufanya matayarisho yakutosha walipoanza uvamizi waLibya. Pia Obama alimlaumurais wa wakati huo wa Ufaransa,Bw Nicolas Sarkozy.

    Matokeo ya “makosa” yotehaya ni kuwa Libya ambayo ninchi iliyo na utajiri mkubwawa mafuta, sasa imemegukavipande vinavyotawaliwa namakundi ya waasi waliopewa

    silaha, mafunzo na fedhana NATO. Baada ya majeshiya NATO na waasi kumuuaGadda na kupindua serikaliyake, waasi wakaanzakugombania ngawira. Kilakikundi chenye silaha kikadaimaeneo yake na ndipowakaanza kushambuliana nakuwashambulia raia.

    Wakati wa mauaji ya Gadda benki kuu ya Libya ilikuwana akiba ya dola bilioni 85.Waasi wakaanza kuporahazina hii ya wananchi nandipo vita vipya vikaanza

    Na Nizar Visram

    huku NATO wakishangilia.Kikundi kilichojiita Dola yaUislamu (ISIS) kikawazidinguvu wengine. Dola bilioni

    1.1 za walipa kodi wa Marekanizikatumika. kuisambaratishaLibya na kusababisha kukuakwa ISIS siyo tu Libya bali katika

     bara la Afrika na kwengineko.Kikundi cha mujahidina

    kilichosaidiwa na NATOndio baadae wakaja kumuuaBalozi Christopher Stevens waMarekani na wasaidizi wakewatatu mjini Benghazi tarehe 11Septemba 2012. Marekani ikabidiwafunge ubalozi wake hukoTripoli na kuikimbia Libya.

    Kosa walilofanya Marekanihuko Libya walifanya piaAfghanistan na Iraq. Ukiachiaraia wa nchi hizo waliouawana nchi kusambaratishwa,Marekani nayo ikapoteza askariwake 7,000 na wengine wengikujeruhiwa vibaya. WakatiObama anajutia alichokifanyahuko Libya, anayofanya hukoSyria ni baya zaidi. Katika nchihiyo, licha ya maelfu ya raiawaliouawa, milioni 12 hawanamahali pa kuishi na milioni nnewameikimbia nchi yao, wengiwao wakielekea Ulaya ambakowanapigwa mabomu na polisi.Mwaka jana tu wamekufa raia1,500

    Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linasema nchini Libyawameibuka mujahidina wapatao6,000 wa kikundi cha ISIS.Wanasema nchini Syria wakokati ya 20,000 na 30,000 ingawa

    wengine wanakisia ni 50,000ukichanganya na walioko Iraq.Wote hawa wanaeneza harakatizao hadi Ulaya ambako wanamawakala wao. Si ajabu kuwawashambuliaji wa mjini Paris naBrussels walipata mafunzo yaohuko Syria. Huu ndio uongoziwa kina Bush, Blair, Obama naCameron.

    Wakati Obama anazungumzia‘makosa’ yaliyofanyika, BiHillary Clinton anaonekanaakichukua msimamo tofauti.Yeye wakati anagombea uraisnchini Marekani amekuwaakisifu utumiaji wa majeshihuko Libya na kusema Marekaniimetumia vilivyo nguvu zake za

    kijeshi.Mwaka 2011 Bi Clintonalikuwa waziri wa mambo ya njewa Obama. Wakati huo baadaya Gadda kuuliwa kikatili nawaasi wakisaidiwa na majeshiya NATO, Clinton alionekanakatika TV akisherehekea nakufurahia mauaji hayo. Bi HilaryClinton ndiye aliyemshauriObama kuidhibiti anga ya Libyaili Gaddafy asiweze kusarishaaskari wake au kuwashambuliawaasi. Matokeo yake waasiwaliweza kujiimarisha kwakupokea misaada ya silaha na

    mafunzo.Kwa mujibu wa gazeti la

    The Washington Post Clintonalishauriwa na wanasheria wa

    wizara yake kuwa kuivamiaLibya ni uhalifu wa sheria yakimataifa. Makamo wa raisBw Joe Biden na mshauri waObama wa mambo ya usalamawa taifa, Bw Tom Donilon naowalipinga mpango wa kuivamiaLibya. Clinton alipuuza ushauriwao na akafaulu kumfanyaObama atoe misaada ya kijeshina kifedha kwa waasi. Mabilioniya dola yaliyokamatwa kutokaakaunti za serikali ya Gaddayalikabidhiwa kwa waasi.

    Katika mkutano nchiniUturuki, Clinton piaalizishawishi serikali 30 za Ulayana Uarabuni kuwasaidia waasi.

    Mara nyingi vyombo vyapropaganda vya magharibivimekuwa vikitulisha uwongokuwa uvamizi wa Marekanina NATO katika nchi kamaIraq, Libya na Syria ni kwamadhumuni ya kuondoaudikteta na kuleta demokrasia.Ukweli ni kuwa mashambulizihaya ni matokeo ya mikakatiiliyopangwa kwa muda mrefuili kutimiza lengo lao la kisiasana kiuchumi. Ushahidi mmojaulitolewa na Jenerali WesleyClark wa Marekani, aliyeongozamajeshi ya NATO akiwakamanda mkuu wakati wauvamizi wa Yugoslavia mnamo1999. Yeye alitamka kuwaMarekani siku zote ilikuwa nampango wa kuzivamia nchi saba

    katika muda wa miaka mitano.Nchi zenyewe alizozitaja ni Iraq,Syria, Lebanon, Libya, Somalia,Sudan na mwishowe Iran.

    Mwaka 2004 Jenerali (mstaafu)Clark alijaribu kugombea uraiswa Marekani kwa niaba yachama cha Democratic lakinihakuteuliwa na chama hicho

    Mnamo 2007 mtangazajiAmy Goodman wa runinga yaDemocracy Now alimuulizaClark kuhusu mkakati huu.Clark akasema alipokuwa jeshinialitembelea makao makuuya wizara ya majeshi jijiniWashington na huko akauonawaraka wa siri ulioelezeamkakati huo. Jenerali Clark

    alisema ni jambo la kawaida kwamarais wa Marekani kuanzakugundua makosa yao baadaya kuachia madaraka. Kwamfano rais George W Bushkatika kitabu chake cha 2010anazungumzia uvamizi waIraq akisema alifanya makosa.Halafu naye rais Clinton mnamo2008 alisema alifanya makosamakubwa wakati wa mauaji yahalaiki nchini Rwanda mnamo1994.

    Kuhusu uvamizi wa Iraq hatawaziri mkuu wa Uingereza,Bw Blair aliomba radhi kwa

    kutoandaa mipango baada yakumuondoa Saddam Hussein.Obama anaungama makosa yakeya Libya lakini kosa lake kubwa

    (tena kosa la jinai) ni kuunganana rais Sarkozy wa Ufaransana waziri mkuu Cameron waUingereza katika kuivamia Libyakinyume cha sheria ya kimataifana kinyume cha azimio la barazala usalama la Umoja wa Mataifa.

    Uvamizi wa Iraq wa mwaka2003 umepelekea raia milionimoja kupoteza maisha yao.Kabla ya hapo vikwazo vyaNATO vilipelekea raia milionimoja wa Iraq kufa. Ndio maanakuna shinikizo kuwa kina Bush(mkubwa na mdogo) na TonyBlair wa Uingereza wakishwemahakama ya kimataifa. Nakuhusu Libya kinachochwa nikuwa sababu halisi ya kumuuaGadda siyo udikteta, bali

    ni kwa sababu yeye alikuwaanaanzisha mawasiliano yasatelaiti kwa Afrika nzima ilituache kutegemea makampuniya magharibi. Halafu pia kwasababu ya ‘kosa’ la kuuza mafutayake kwa China pamoja nakukataa kuruhusu vituo vyakijeshi vya Marekani nchinimwake.

    Gadda pia alikuwaakianzisha benki kwa bara zimala Afrika ili tuache kutegemea‘wafadhili’ wa magharibi.Yote haya yaliwakwanzasana watawala wa NATO.Baada ya Marekani na NATOkuisambaratisha Libya, sasawanakabidhi kazi ya kuikarabatinchiyo kwa Rais Mstaafu JakayaKikwete, akiwa mwakilishimaalum wa Umoja wa Afrika(AU).

    Wakati NATO walipoivamiaLibya ni AU ndiyo iliyopazasauti yake ikipinga. Ilikuwatayari kuingilia kati nakuzungumza na Gadda iliyamalizwe bila ya vita. Ujumbeulitumwa hadi Libya ukaonanana Gadda. NATO waliipuuzaAU. Leo wanaifadhili AUeti waikarabati nchi hiyowaliyoibomoa.

    Tusidanganyike na radhiwanazoomba. Hatua za kisherialazima zichukuliwe kamazinavyochukuliwa dhidi yawatawala wa Kiafrika. Swali

    ni je, nani wa kumfunga pakakengele? Tungeanza na kukataahivi vilemba vya ukoka vyakupewa usuluhishi wa Libya.Ukweli wa mambo ni kuwawaliolikoroga, ndio wanaowezakulimaliza maana ndio haohao wanaoendelea kununuamafuta kutoka kwa makundiyanayouwana halikadhalikakuwapa silaha. Ufupi wamaneno, ni vijana wao. Na ndiohao hao wanaowatumia hukoSyria.

    ([email protected])

    Obama aungama ‘makosa’ aliyofanya nchini Libya

    ANNUUR NEW.indd 7 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    8/20

    8  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Makala

    Inaendelea Uk. 15

    “NILIPATWA na ugumu kwelikuamini kuwa Yesu hakufamsalabani”

    Hayo yalikuwa ni manenoya Balqis Chepkwony (awaliakiitwa Caroline Chelang’atChepkwony) baada ya kusomakitabu cha Mhadhiri maarufu waKiislamu wa Afrika Kusini namzaliwa wa Pakistan, marehemuAhmed Deedat, kiitwachoCrucixion or Cruci-ction (Nikweli Yesu kasulubiwa au niubunifu tu!)

    Caroline Chelang’atChepkwony, alikuwamwanafunzi mwenye juhudisana na siku zote alikuwaakishika nafasi ya juu katikamaisha yake ya masomo ya shuleya msingi. Baba yake alitaka awedaktari wa binadamu, lakiniMzungu mmoja raki wa babayake alishauri Caroline awemtakwimu bima (Actuary) nawakafuata ushauri ule.

    Kama ilivyo kawaida katikamataifa mengi ya Kiafrika, ni

    wanafunzi wafanyao vizurizaidi tu kitaifa, ndio wanaowezakupata nafasi katika shulechache za serikali. NchiniKenya Caroline Chelang’at,alikuwa mmoja wa wanafunziwalioteuliwa kuendelea naelimu ya sekondari katikashule ya serikali. Alichaguakatika shule ya sekondari yaAlliance (Alliance Girls HighSchool), shule inayotambulikakwa kutoa elimu nzuri nakufaulisha watoto sana, sifa zakezikitawala katika vyombo vyahabari vya redio, televishenina magazeti kinapoka kipindicha kutangazwa matokeo.Wanafunzi wa hapo wakipenda

    kuiita shule yao “bush”(kichaka) na wanafunzi wakiitwa‘busherians (wanakichaka). Jinahilo lisilo rasmi limetokana namsitu mkubwa uliozungukashule hiyo. Shule hiyo marakwa mara imekuwa ikifanyavyema katika mitihani ya taifakidato cha nne, ikiwa ni kawaidakuingia kumi bora katika shuleza Kenya.

    Baada ya kufanya vizurikatika mitihani hiyo ya elimu yasekondari, alifaulu kwa kupatawastani wa alama ‘A’ katika wamasomo yote Alipata darajala juu la (A) katika masomoya sayansi ya Hesabu, Fizikia,Kemia, Komyuta na Jiograa.Moja kwa moja Carolinealinyakuliwa na Chuo Kikuu chaNairobi (UoN), Chuo kikubwazaidi nchini Kenya, ambachokilimchukua kwa kitivo chasomo la Hesabu, akisomeaUtakwimu Bima (ActuarialScience).

    Wakati huo kilikuwa ni ChuoKikuu hicho cha Nairobi pekeenchini Kenya kilichokuwakinatoa shahada ya UtakwimuBima. Mwaka huo 2002, Chuocha Nairobi kilikuwa kikichukuawanafunzi 16 tu, Kenya nzimawaliochaguliwa na serikali na

    Zana za mapigano zamuokoa

    Balqis Chelang’at ChepkwonyKufufuka au kurudishiwa fahamu?Ipi ilikuwa miujiza ya Nabii Yona?

    Suluhisho thabiti la ubishani wa Utatu

    Chelang’at alikuwa mmoja wawaliostahili.

    Akiwa mwaka wa pili wamasomo, Caroline alikutanana Salim, mwanafunzi katikahicho aliyekuwa akichukuamasomo yake katika Kitivocha Sanaa (Faculty of Arts).Moja ya vipaumbele vya Salimkatika maongezi ilikuwani mazungumzo ya dini.Alimchokoza Chelang’atkuhusu imani yake ya dini.Salim alimuomba Chelang’atafanye ufatiliaji mzuri kuhusu

    dini na yeye akamsikiliza.Bila kupoteza muda, Salimalimkabidhi Chelang’at

     baadhi ya vitabu na makalayanayoongelea linganishi ya dinimbalimbali na kumtajia orodhaya tovuti ambazo zinachambuamasuala ya dini vyema, tenakwa kutumia akili ya kawaida.Baadhi ya vitabu ambavyoCaroline alivisoma ni pamoja navya Marhuum Sheikh AhmedDeedat kuanzia kile cha ‘Is theBible Word of God? (Je, Biblia niNeno la Mungu?). Crucixion or

    Balqis Chepkwony (awali akiitwa Caroline Chelang’at Chepkwony)

    Cruci-ction! (Kusulubiwa kweliau kusulubiwa kwa kubuniwa?),Resurrection or Resuscitation?,(Kufufuka au kurudishiwafahamu?)

    Vingine ni What Was the Signof Jonah? (Ipi ilikuwa muujizawa Yunus?), Who Movedthe Stone? (Nani aliyesogeza

     jiwe?), Qur’an Miracle ofMiracles (Qur’an ni muujiza wamiujiza), What the Bible SaysAbout Muhammad (pbuh)?(Biblia inasema nini kuhusuMuhammad?) Christ in Islam

    (Kristo ndani ya Uislamu) naCombat Kit (Zana za mapigano).Vitabu vyingine alivyosomakabla ya kusilimu ni pamojana kile cha Let the Bible Speak(Wacha Biblia izungumze) chaAbdul Rahman Dimishkiah,Oneness of God: The UltimateSolution to the TrinitarianControversy (Umoja wa Mungu:Suluhisho thabiti la ubishani wautatu) cha Marmarinta UmarP. Mababaya na Pillars of Faith(Nguzo za Imani) cha JaafarShaikh Idris.

    Vitabu hivyo na venginevyovya Ahmed Deedat, vilivunjakabisa imani ya Kikristo yaCaroline na hatimaye akabakiwana moja tu la kufanya: kuamuakuingia katika Uislamu. Hivyoilipotimu tarehe 14 Aprili 2005,akiwa na umri wa miaka 22ndipo Caroline alipoamua rasmikuwa Muislamu na kuliacha

     jinale la Kikristo na kuchukuala Kiislamu, akibakisha majinayake ya Kikalenjin (Kalenjinni moja ya kabila za Kenya).Sasa amekuwa akiitwa BalqisChelang’at Chepkwony.

    Kabla ya kusilimu, akili yakeilijaa mawazo mgando na hasikuhusu Uislamu na Waislamu.

    “Nilikuwa nikiwachukuliaWaislamu kama watu wa ajabuna waliopotea kweli, kwaniwalikuwa wakimuamini Mtumeambaye amekufa.” Alisema.

    Baada ya kusilimu, Balqisaliweza kuangalia kwawasaa video za AhmedDeedat, akifanya midahalo na

    wanatheolojia mashuhuri waKikristo. Ilimchukua mwezimmoja na nusu tu kuhifadhi

     Juzuu Amma, Juzuu ya mwishokatika Qur’an iliyo kwa lughaya Kiarabu (Qur’an ina juzuu30, Juzuu moja ikiwa na kurasa20 na Qur’an nzima ina kurasa604). Japo alibanwa sana naratiba za masomo shuleni naprojects (miradi ya majaribio),

     bado alithubutu kuhifadhi Juzuunzima ya mwisho ya Qur’an. Hiiinaweza kuwa sawa na kuiwekakichwani injili ya Mathayo, nenokwa neno!

     Jamia Mosque, Msikitimkubwa zaidi nchini Kenyauliopo jijini Nairobi, una

    kitengo maalumu kwa ajili yawanaosilimu, mahususi kwaajili ya kuandaa madarasa yakuwasaidia walioingia katikaUislamu ili kuijua dini yao. NayeBalqis baada tu ya kusilimu,aliweza kuka hapo, alisoma nakuhitimu masomo hapo katikaTaasisi hiyo ya Jamia.

    Balqis alifatilia masomo yaKiislamu kwa dhati, akiendanana aya, “…Kishike kitabu [yaanidini] kwa nguvu!…” [Q 19:12].

    Baada ya kupata shahadayake ya kwanza kutoka ChuoKikuu cha Nairobi mwaka2006, na kama ilivyo ada kwamhitimu yeyote, Balqis nayealiingia katika michakato yakutafuta kazi. Familia na rakizake walimsaidia pia katikahilo. Mzazi wake wa kiume,ambaye alikuwa ni mhasibumkuu (Chief Accountant) waChuo Kikuu cha Moi (MoiUniversity), bila shaka alikuwaanajuana na wafanyabiasharawengi au makampuni mengi.Hii ingetosha kumpatia kazinzuri yenye hadhi Balqis.Tena kwa shahada aliyokuwanayo, alikuwa na asilimia 100ya kuchukuliwa na mabenki

    ANNUUR NEW.indd 8 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    9/20

    9  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Makala/Tangazo

    KWA hakika jamii yeyotemiongoni mwa wanajamiikatika wanadamu, hawezi

    kuishi peke yake kwa furahabila ya kuungana na mtumwingine kwa tabia nzuri.

    Tabia nzuri ni dalilikutoka katika Qur’ani naHadithi alizotuteremshiaAllah (sw) juu ya umuhimu

    Tabia njema sababu ya kudumisha mapenzi kwa Waislamu

    Na Shekih Mohamed Al-amirOsman.

    wa tabia nzuri, kwani ndizozinazohakikisha maisha bora hapa duniani na kesho

    akhera. - Hii ni moja ya amriza Mwenyezi Mungu.

    Amesema Allah (sw)“Samehe na amrisha memawapuuzeni wajinga) (199 Al-Aaraf).

    Kumtii Mtume (S.A.W)toka kwa Abii Dhari (R.A)amesema, amesema Mtume(S.A.W), “MuogopeniMwenyezi Mungu popotemlipo na fanya jema harakapale utapofanya baya kwani jema hufuta baya, ishi nawatu kwa tabia nzuri”.Ameipokea Tirmithi.

    Pia ni sababu ya kupatamapenzi ya MwenyeziMungu mtukufu. AmesemaMwenyezi Mungu Mtukufu,“Na fanyeni memakwani Mwenyezi Munguanawapenda wafanyao

    mema” (195 Al-Bakarat).Na amesema Mwenyezi

    Mungu, “Allah anawapenda

    wafanyao uadilifu, usawa(42 Al-Maidah). Na tokakwa Usama Bin Shariki(R.A) amesema, “Tulikuatumekaa mbele ya Mtume(S.A.W) tukiwa tumetuliakama vichwani mwetuwametua ndege, hakuna hatammoja anayezungumza katiyetu, mara wakataka watukujua, wakasema ni mjagani wa Mwenyezi Munguanayependeza sana kwaMwenyezi Mungu? Akasemani Yule mwenye tabia nzurizaidi”. – Ameipokea Al-

    Hakim na Twabaraa.Sababu ya mapenzi ya

    Mtume (S.A.W) toka kwa Jabiri bin Abdillahi (R.A),amesema Mtume (S.A.W),“Kwa hakika inayempendasana mimi na atakayekuwa

    karibu sana na mimi siku yakiama ni yule mwenye tabianzuri”. Ameipokea Imam

    Tirmidhi.Na tabia nzuri huongeza

    uzito katika mizani. Toka kwaAbii Dardai, toka kwa Mtume(S.A.W) amesema, “Hakunakitu chochote kilicho kizitozaidi katika mizani kulikotabia nzuri”. Ameitoa AbuuDaudi.

    Toka kwa Abii Hurairata(R.A) amesema aliulizwaMtume (S.A.W) juu ya mambomengi yanayowaingiza watuwengi peponi? Akasema“Ni kumuogopa MwenyeziMungu na tabia nzuri”.

    Hivyo Muislamu anatakiwakuishi kwa tabia nzuri kwawatu ili apate maisha borahapa duniani hadi hukoakhera.

    Email : [email protected]

    ANNUUR NEW.indd 9 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    10/20

    10  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016

    Gen. David M. Rodriguez. Generali William E. "Kip" Ward

    MAKALA 

    Na Omar Msangi

    HIVI majuzi Rais BarackObama amemteua MarineCorps Lt. Gen. Thomas David"Tom" Waldhauser kuwakamanda mpya wa Kamandiya Kijeshi ya Marekani katikaAfrika-U.S. Africa Command(Africom). Waldhauserakithibitishwa na Bunge laCongress, atachukua nafasiya Army Gen. David M.Rodriguez. Kamanda wakwanza alikuwa GeneraliWilliam E. "Kip" Ward (2007-2011) akifuatiwa na GenraliCarter F. Ham (2011-2013.)

    Kwa Wamarekani, kupitiaCongress, pengine taarifamuhimu kwao, itakuwa ni kujuasifa za Lt. Gen. Waldhauserkatika Operation Desert Storm(Gulf War) na Operation EnduringFreedom (OEF) ili wapatekuamua iwapo atamudu nafasihiyo mpya au la. Ila kwetu sisi

    Afrika, nadhani muhimu kwetuni kujua, hii Africom ya nini?Kwa nini Africom? Inatufaa kwalipi? Nini agenda na malengo yawenye Africom yao?

    Katika yale yanayoelezwana wenyewe, malengo yaAfricom kwa sasa ni kusaidiakupambana na ugaidi, makundiyenye msimamo mkali (violentextremists) na kuzisaidia nchi zaAfrika kuwa na Amani.

    “Ushirikiano katika masualaya ulinzi ni katika malengoyetu makubwa katika Africom(core missions at U.S. AfricaCommand) kwani kwaushirikiano huo tutawaimarishawashirika wetu katika

    kukabiliana na changamoto zausalama.”Alisema Kamanda Rodriguez

    alipotembelea Djibouti,Somalia, Ethiopia, Kenya naUganda mwaka jana akielezeaumuhimu wa Africom kwaAfrika. Akaongeza kuwaAfrika hivi sasa imekuwa naitaendelea kuwa eneo muhimula kinyang’anyiro cha rasilimalina mambo ya kiuchumi kwaujumla, hivyo suala la usalamalinakuwa na umuhimu mkubwa.

    Kama taifa kubwa duniani,Marekani inajaribu kuidhibitidunia nzima kupitia uwezowake wa kijeshi. UkitokaPentagon, utakutana na–European Command, CentralCommand, Pacifc Command,Southern Command na NorthernCommand.

    Kabla ya kuundwa Africom,Afrika ilikuwa chini yaEuropean Command ukiachanchi za Misri, Seychelles,Djibouti, Eritrea, Ethiopia,Kenya, Somalia (Horn of Africastates) na Sudan, ambazozilikuwa chini ya CentralCommand huku Comoros,Madagascar, Mauritius naReunion, zikiwa chini yaKamandi ya Pacic (Pacic

    Sio ‘Ugaidi’ ni ubunifuMshenga mpya wa ajali anakuja

    Ukoloni unarudi kwa ruhusa yetu

    Command.)Ilikuwa ni mwaka 2007

    ambapo Africom iliundwa,lakini makao makuu yakeyakiwa Stugart, Ujerumanihuku ikielezwa kuwa Kamandihiyo itaigawa Afrika katikamakundi matano yote yakilengakuhudumia jumuiya na umoja

    wa kikanda wa kiuchumi ndaniya Afrika (Africa’s main RegionalEconomic Communities). Timumoja itashughulika na nchi zaAlgeria, Libya, Mauritania,Morocco na Tunisia (Arab

     Maghreb Union). Kanda yetu yaAfrika Mashariki-East AfricanCommunity (EAC) ikiwana nchi za Burundi, Kenya,Rwanda, Tanzania na Uganda,nayo itakuwa na watu wakemahsusi ndani ya Africom wakuishughulikia.

    Kanda nyingine ni ile yaEconomic Community of West

     African States (ECOWAS), ikiwana nchi za Benin, Burkina Faso,Cape Verde, Cote d’Ivoire,

    Gambia, Ghana, Guinea-Bissau,Liberia, Mali, Nigeria, Senegal,Sierra Leone na Togo.

    Kuna pia zile nchi za Jumuiyaijulikanayo kama EconomicCommunity of Central AfricanStates (ECCAS). Hizi ni Angola,Burundi, Cameroon, CentralAfrican Republic, Chad,Republic of Congo (Brazzaville),Democratic Republic of Congo (Kinshasa), Equatorial Guinea,Rwanda na Sao Tome naPrincipe. Hizi nazo zitakuwana deski lake ndani ya Africom.Ukitoka hapo unakutana na

     Jumuiya ya Southern AfricaDevelopment Community (SADC),ambapo unazikuta nchi zaAngola, Botswana, DemocraticRepublic of Congo, Lesotho,Madagascar, Malawi, Mauritius,Mozambique, Namibia,Seychelles, South Africa,Swaziland, Tanzania, Zambia

    na Zimbabwe. Na yenyewehii, imewekewa watu maalum,kuishughulikia.

    Kipo pia kikosi maalum chawataalamu, kuzishughulikianchi za Kanda inayoitwaHorn of Africa. Humozinatumbukizwa nchi zaDjibouti, Ethiopia, Eritrea,Kenya, Seychelles, Somalia,Sudan, Tanzania na Uganda.Yemen inatumbukizwa humopia. Zote hizo zinahudumiwana kikosi kinachoitwa Combined

     Joint Task Force – Horn of Africa (CJTF-HOA) chenye makaoyake Djibouti ambapo Pentagonimeweka askari wake wapatao2000.

    Ukiacha CJTF-HOA,Marekani ina kambi kamili zakijeshi (military base) Djibouti,Camp Lemonnier. Lakinipia inazitumia Seychelles,Kenya, Ethiopia, Morocco,Mali, Rwanda na baadhi yanchi nyingine za Kiafrikakufanya harakati zake za kijeshiipendavyo.

     Japo makao makuu yaAFRICOM, bado yapo Stugart,Ujerumani, lakini utaonakuwa kupitia utaratibu huo wakuishika Afrika kijeshi kupitiakanda hizo, ni kana kwamba

    Bara lote hivi sasa limedhibitiwa.Upo utaratibu na mikakati yakuandaa vikosi vinavyoitwaThe African Standby Force (ASF)ambayo, kinadharia ipo chini yaUmoja wa Afrika (AU), lakinimakamanda watoa mafunzo nawapanga na waongoza mipangoni Pentagon (U.S. Special Forces)

    na NATO (NATO Strike Force/NATO Response Force (NRF)).

    Ukiacha zile kanda zakiuchumia-EAC, AMU,ECOWAS, ECCAS na SADC,ambazo zina madeski yakemaalum ndani ya Africom,vimeundwa pia vikosi maalumvya kipolisi na kijeshi kwa kilekilichoitwa kusaidia kupambanana magaidi. Hapa unakutanana Pentagon’s Trans-SaharaCounter-Terrorism Initiative(TSCTI), ikizihudumia nchi zaAlgeria, Chad, Mali, Mauritania,Niger, Senegal, Morocco,Nigeria na Tunisia. Washirikawa Washington katika nchi zaNATO ambao ni Uingereza,

    Ufaransa, Ujerumani, Hispaniana Uholanzi, nao wanaingiakatika Trans-Sahara Counter-Terrorism Initiative.

    Kupitia mpango huu,vinaundwa vikosi maalum(Special Forces) vikipewamafunzo na kusimamiwa na U.S.Africa Command (USAFRICOM)pamoja na Special OperationsCommand (SOCAFRICA).

    Taarifa zinaonyesha kuwakatika eneo letu hili la AfrikaMashariki, kumeundwa kikosi

    Inaendelea Uk. 11

    Lt. Gen. Thomas David "Tom"Waldhauser.

    ANNUUR NEW.indd 10 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    11/20

    11  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 201611 AN-NUUR

    Makala

    Inatoka Uk. 10

    Sio ‘Ugaidi’ ni ubunifukikijulikana kwa jina la EastAfrican Standby Brigade(EASBRIG) ambayo makaomakuu yake yapo katika Chuocha Maosa wa Kijeshi (DefenceSta College) Karen, Nairobi.

    Humo kukiwa na wataalamuwa kijeshi kutoka Marekanina nchi za Ulaya. EASBRIGina wanajeshi kutoka Burundi,Comoros, Djibouti, Eritrea,Ethiopia, Kenya, Madagascar,Mauritius, Rwanda, Seychelles,Somalia, Sudan, Tanzania naUganda. Gazeti la The Nation,la Oktoba 29, 2009, lilimnukuummoja wa makamanda wakijeshi wa Kenya Julius Karangi,akieleza uwepo wa EASBRIGkatika Kenya halikadhalikauwepo wa makamanda wakijeshi wa kigeni ambaoalisema kuwa watasaidiasana kuimarisha kikosi hichomaalum.

    Aidha, inaelezwa kuwa U.S.Africa Command (Africom)itafanya kazi bega kwa bega naEASBRIG katika kupambana namagaidi eneo hili la Afrika chiniya ule mkakati wa ujumla waVita dhidi ya ugaidi (Global Waron Terrorism).

    Kwa hiyo katika mazungumzorasmi ya kiserikali yanayowekwahadharani, Africom ni sadakakwa Waafrika. Ni msaadaunaokuja “kwa hisani ya watuwa Marekani” kutokana na rohonzuri na huruma ya Wamarekanikutaka kutuimarisha kiulinzina usalama. Ndio maanaukaona hivi sasa kunaharakati na program nyingi zamafunzo, misaada ya kijeshina yanayoitwa mazoezi yapamoja. Na ili kuhakikishakuwa program hizo zinakwendavizuri, tayari jeshi la Marekanilina kambi za kijeshi (military

     bases) katika nchi kadhaa zaKiafrika.

    Katika mlango huo wakusaidia kutujengea uwezo wakiusalama, imepatikana sababuya Marekani kuwa na kambizake za kijeshi katika nchi zetukwa ridhaa yetu wenyewe!

    Swali ni je, utando huu wakijeshi ukishalikamata Barazima, nchi za Kiafrika na Bara laAfrika litabakia tena kuwa huru?

    Hivi ndani ya nchi yakokukiwa na kambi ya Marinesna ghasia zake zote za vifaa vyakisasa vya kijeshi, jeshi la nchiyako litakuwa tena na kauli?Wenye Marines katika ardhiyako, wakitaka jambo kutokakwako, unaweza kuwakatalia?Ukiwa na jeshi ambapomakamanda wake wanapokeamaelekezo na kupewa mafunzona U.S. Africa Command(USAFRICOM) pamoja naSpecial Operations Command(SOCAFRICA), bado utasemakuwa hilo ni jeshi lako?

    Africom la ujumla ambalo ni USHegemony, lakini pia ukolonimpya wa kudhibiti rasilimaliya mafuta na madini katika

     bara hili. Na kwa maana hiyo,ugaidi si jambo la kuondokakwa sababu sio adui halisi balimkakati wa kukia malengo

    fulani ya kibeberu na maadhalimalengo hayo yanaendeleakutekelezwa, basi ugaidiutaendelea kuwepo ili kisingiziocha kuwa na ‘Special Forces’ nakambi za kijeshi katika Bara hili,kiendelee kuwepo.

    Nimalizie kwa kusema kuwa,hakuna jipya linalofanyika.Ni Ukoloni, unyang’anyi naubeberu ule ule wa tanguzama. Ila hivi sasa watuwamestaarabika kidogo. Kamaalivyojisema JB katika moja yalamu zake akionekana kutapeliwatu. Alisema “mimi sio tapeli.Mimi ni mbunifu.”

    Kwa kuja Vita Dhidi yaUgaidi, unaletewa mpangowa kukusaidia kupambana naAl-Shabaab, unawakaribishamwenyewe, unawakabidhipolisi wako na wanajeshi wakowakuundie ‘Special Forces’ hukumahali pengine wakipewa fursaya kuweka kabisa kambi zao zakijeshi.

    Kwa hiyo, “Vita Dhidi yaUgaidi”, nayo ni ubunifu waaina yake katika uvamizi,uporaji na ukoloni. Hivi sasawanatuambia eti ‘gaidi’ AbdulNadir Mumin ameikimbia AlShabaab akiwa na mipango yakuanzisha kundi la ISIS AfrikaMashariki. Kwamba eti, AfrikaMashariki ni “region that is ripefor the group’s expansion buthas yet to be exploited.”

    Kwamba, hii Afrika Masharikiyetu, ni eneo lenye fursa nzuriza kusitawi ‘magaidi’ wa ISISlakini fursa hizo hazijatumiwaipasanyo. (Tazama: The Orange-

     bearded Jihadi general spreadingISIS brand in Somalia-By JackMoore.)

    Kama kawaidawanatengeneza video zapropaganda, wanazirushakwenye Sky News zao.

    Mtu unajiuliza, kama kuna

    AMISOM na wameshatuleteaEast African Standby Brigade(EASBRIG) na Combined JointTask Force – Horn of Africa(CJTF-HOA), hayo mazingiratena mazuri ya kusitawi magaidiwa ISIS, yanatoka wapi?

    Alijisemea mtaalamu mmojakwamba ubeberu wa zamahizi, unatumia “sophisticatedtechniques consciously designed toconfuse the human mind.”

    (Soma zaidi: AFRICOM andthe Recolonisation of Africa.)

    Maswali kama haya ndiyoyanayopelekea wachambuzi wamambo kusema kuwa ujio waAfricom ni ukoloni mpya.

    “New Colonialism: PentagonCarves Africa Into MilitaryZones”, ni Makala iliyoandikwana mwandishi Rick Rozo(Global Research, May 05, 2010).Katika Makala hiyo anasemakuwa kwa utaratibu kama huu,utaona kwamba ni kana kwambaMarekani inajitengenezea

    majeshi ya kuifanyia kazi(Surrogate Armies) kuidhibitiAfrika

    Hayo yanaelezwa pia katikaule uchambuzi uliopewaanuwani ya “AFRICOM and theUSA’s Hidden Bale for Africa”uliochapishwa Machi 30, 2010.Humo inaelezwa juu ya kikaokilichofanyika Januari 2, 2002,kule Washington DC agendaikiwa mafuta ya Afrika (AfricanOil: A Priority for US NationalSecurity and African Development).

    Katika kikao hicho ambacho

    kilihudhuriwa na wazito wamakampuni ya mafuta, maosawa serikali na mtaalamu wakijeshi katika Afrika Lt-Col.Karen Kwiatkowski pamoja naWaziri Mdogo wa Mambo ya Njeanayeshughulikia Afrika (wakatiule wa Bush) Water Kansteiner,ndiko kulikoibuka program hizitunazozishuhudia leo katikaAfricom.

    Likiripoti juu ya habari hizi,gazeti la The Christian ScienceMonitor linasema kuwa ilikuwa

    ni katika kikao cha Januari2002 kule Houston, Texas,kilichoandaliwa na kundilinalojiita African Oil PolicyInitiative Group (AOPIG),ambapo yaliibuka mambo mengiyaliyoongoza sera za Marekanikwa Afrika, hasa katika masualaya raslimali, na hasa mafuta.

    Katika uchambuzi wa-AFRICOM and the USA’sHidden Bale for Africa, vitadhidi ya ugaidi inatumiwa kamakisingizio kucha lengo halisi la

     MMOJA wa Makamanda kutoka Afrika akiyatembelea Makao Makuu ya AFCOM.

    ANNUUR NEW.indd 11 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    12/20

    12  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 201612 TANGAZO

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

    Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

    Ubungo Islamic High School - Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172

    Kirinjiko Islamic High School - Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441

    Nyasaka Isamic High School - Mwanza: 0786 417685/0713 749020

    Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezibora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.Zipo Combinations zote za SAYANSI,  ARTS na BIASHARA.Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha ‘Credit’  (yaani A, B na C)

    Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination. 

    Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/05/2016.

    Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

    NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

    WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI

    Bismillahir Rahmaanir Rahiim

     ARUSHA:  Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo

    Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu

    Bondeni : 0783 438676/0715 438676.

    KILIMANJARO:  Moshi: Msikiti wa Riadha:07673453

    67/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na

    Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko

    Islamic Secondry School: 0784 296424/0713

    115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054.

    Ugweno – Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa:

    0784 656514

    TANGA:  Twalut Islamic Centre – Mabovu

    Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu

    Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA

    SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop

    - Lushoto: 0782257533. Handeni –Mafiga -0782105735/0657093983

    MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717

    417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education

    Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-

    Amin 0785 086 770/0714097362.

    BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056

    MUSOMA:  Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa

    Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611

    SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa

    ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

    KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya

    Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School : 07

    56584625/0657350172/0712 033556. Ofisi yaIslamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin

    : 0655144474/0787119531

    MOROGORO:  Wasiliana na Ramadhani Chale :

    0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu:

    0659 158958

    GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya

    kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056

    DODOM A:Hijra Islamic Primary School : 0716

    544757/0718661992

    SINGIDA:  Ofisi ya Islamic Education. Panel

     – karibu na Nuru snack Hotel : 0786425838/0784 928039.

    MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid

    Rahma: 0784491196

    KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727.

    Kibondo – Islamic Nursery School:

    0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS:

    0714710802/0763 298440

    LINDI:  Wapemba Store: 0784 974041/0783

    488444/0653 705627.MTWARA:  Ofisi ya Islamic Education Panel,

    Mtaa wa Magomeni A mkabala njia panda ya

    uwanja wa ndege: 0715 465158/0787 231007.SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa

     NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic High

    School :0654 876317MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini

     – 0785425319. Rexona Video mkabala na

    Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319.Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786313830TABORA:  Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784

    944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754

    576922/0784576922.IRINGA: Madrastun – Najah: 0714 522 122.PEMBA:  Wete: Wete Islamic School : 0777

    432331/0712772326.UNGUJA: Madrasatul – Fallah: 0777125074.

    PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na

    uwanja wa Lumumba

    MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na

    msikiti mkuu : 0773580703.

    Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 30/05/2016

    ANNUUR NEW.indd 12 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    13/20

    13  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Safu ya Ben Rijal

    Wanyama waliotajwa katika Qur’an: Ndege - 3

    KATIKA makala iliopitatulichambua aya mbalimbalizinazomuelezea ndege Hudhudambaye ni ndege mwenyekupendeza na kuelezewajuu yake katika Qur’an jinsialivyokosekana wakati MtumeSuleiman AS alipokuwa akikagua

    vikosi vyake.Tumeweza kufahamu kuwa

    Mtume Suleiman AS, alikuwaakijua na kuzifahamu lugha zawanyama na majini wote walikuwachini yake. Mtume Suleiman AS baba yake ni Mtume Daud ASakiwa ni kati ya Mitume ambao baba alikuwa ni Mtume na mtoto.Orodha hio ya Mitume ikiwa babani Mtume na mwana ni Mtume, nikama ifwatavyo, Mtume Ebrahim,watoto Ismael na Ishaq na wotewalikuwa ni Mitume, MtumeZakariyah na mwana Yahya, Ishaqna Yakoob, Mtume Yakoob namwana Yusuf.

    Ndege Hudhud ni ndegemwenye kupendeza na wataalamuwa Sayansi baada ya kumsomakupitia Qur’an na Baibilia,

    walifanya utati kuona kama ndegehuyu bado yupo au ametoweka?Wamekuja kuelewa kuwa badoyupo na anaonekana katika sehemuza mabara ya Ulaya, Afrika na bara la Asia. Katika bara la Afrikahuonekana zaidi katika maeneoya Afrika ya Kaskazini, Afrikaya Kusini na kwenye kisiwa chaMadagascar.

    Kabla hatujamuelezea kwa kinahebu tuangalie anavyojulikanakatika Ulimwengu tunaoishi:Wayahudi huko Israelwamemtukuza na kumfanyani ndege wa taifa hilo. Wamisriwa kale katika maandishi yaoyameonyesha kuwa Hudhud nindege adhimu, kizungu anaitwakwa jina la Hoope kwani anavyoliahulia “Ooop Ooop”, kama alivyo

     jogoo na yeye ana upanga juuya kichwa chake kitu ambachokinakuwezesha kumuelewa marammoja unapomuona. Mabawayake yana rangi ya mdalasini nakwenye mabawa yake akiwa narangi nyeusi na nyeupe pamojana kwenye mkia ambazo ni rangizenye kuleta haiba. Malaji yakemakubwa ni kukamata waduduwadogo wadogo, hula vyura,mbegu mbalimbali, na mdomowake huuweka wazi mara nyingikwa kuwa tayari kwa mawido.

    Hudhud ana tabia yakuvutia pale anapoota juahuwa anagaragara huku akiwa

    Na Ben Rijal

     Mchoro wa Hudhud aliochorwana Zhao Mangfu ukionekanakatika Makumbusho ya Shanghai.

    ametanua mbawa zake na mkiawake kuweka juu. Katika moja ya jambo lake lilokuwa sio la kawadiakumlinganisha na ndege wengine,ni pale anaporuka na kuanza safarizake hufanana na kipepeo.

    Hudhud ana hikma za kujiwekakuwa katika maisha endelevu kwanikwenye nyumba yake huwekaharufu ya uvundo ya kuwafanyamaadui wake kutomkaribia, lakini

    Yaonekanavyo mayai ya Hudhud.

    wakati huo huo kuwavutia wadudukuingia katika tundu lake nakuweza kupata chajio chake kwaurahisi kabisa.

     Wanyama wengi hujengamamlaka ambayo huwa hatakimwengine kumuingilia. Kwamfano Simba kwenye mamlakayake hunyunyiza mkojo sehemuyote anayoimiliki. Kwa hio, huwatayari kupambana na Simba yoyoteatakayejiingiza katika mamlakayake kutaka kumvunjia, hapa nikuzungumzia kutaka kufanyamapenzi na jike lake.

    Upande wa Hudhud, dumehujenga mamlaka yake katika jumba lake na kubembea namwandani wake wakiwa peke yao.Hapo atakayetaka kuja kumharibiahupambana naye na mapambanomara nyingi huwa makubwahata kupelekea kutofoana machoau kujeruhiyana na mwenginekufariki. Wachunguzi wa maisha

    ya wanyama wamegundua kuwamaisha yao hayazidi miaka 10.Kujua umri ambao viumbe

    mbalimbali huishi ni muhimukwani inasaidia kujua namna yakukabiliana, kwa mfano jamii yanzi hawazidishi maisha yao zaidiya siku 30, wakati mbu maisha yakeyote hayapindukii zaidi ya miezi 2na ni mbu jike ndio anayomuumamwanadamu kutafuta protini nambu dume yeye hutumia zaidi juisi ya maua. Kuweza kujua umriwa maisha ya viumbe mbalimbalihusaidia katika kupambana naokuweza kuwaangamiza.

    Wanadamu nao kujulikana kwa

    wastani wanaishi umri wa miakamingapi inategemea wanapoishikwa mfano nchi tajiri kutokana

    na maisha yao kutononoka huishimaisha ya miaka mingi kukiamfano 70 kwa wastani na nchi zakimaskini watu huishi watani wamiaka ya 40na 50.

     Tumeweza kuona Hudhudwanakisha maisha yaokukia umri wa miaka 10, kwawalivyokuwa sio waharibifu, kwahio Hudhud mwanadamu sio aduiwake mkubwa. Viumbe ambaohuwa ni maadui kwa binadamuidadi yao hupungua kutokana navita baina ya mwanadamu na haoviumbe.

    Chambuzi za Huduhud kitaalamuWataalamu wanamhesabu

    Hudhud kama ni mnyama nakumuweka katika ukoo Upupidaena jina la kitaalamu anajulikanakama Upupa epops.

    Hudhud ni katika ndege wa kalewanaofahamika katika Historia.Yupo duniani kwa zaidi ya miakaalfu na Zaidi. Umbo lake ni la katilisozidi centimeter 25 na uzito wakehauzidi baina ya gramu 46 na 89.Unapokuwa kwenye msitu katikamaeneo wanapopatikana, ni rahisisana kujua aliaye kama ni Hudhud

     Hudhud akiwa anatafuta chajio

    kwa mlio wa kufwatana Oop OopOop ingawa kina Jogoo mwitu naohufanana kimlio, lakini Hudhudanapolia hufwatanisha kiasi maratatu akapumzika kisha kaendelezakulia Oop Oop Oop.

    Uonekanaji wakeKama huko kabla tulivyoelezea

    kuonekana kwake zaidi huonekanakatika mabara matatu ikiwa bara laUlaya, Asia na Afrika ya Kaskazini.Hudhud waliopo Ulaya, huhamanyakati za baridi na kuhamia baraniAfrika wakati wa bara la Afrikawao hubakia nyakati za kiangazi na

    kipupwe pasi kuhama. Uhamaji waHudhud kwenda masafa marefukutoka Ulaya hadi kuka Afrikakwa utaaalmu wa Sayansi kuwezakugundua hivi sasa ni kielelezokinachotufahamisha pale MtumeSuleiman alipokagua majeshi yakeakiwa Hudhud haonekani. Hudhudalikuwa sehemu za Saba huko niYemen na Mtume Suleiman alikuwa Jerusalem. Hii ni ithibati ya yaleyaliolezwa kwenye Qur’an na Bibiliahayana towa.

    Mahusiano yake na MwanadamuHuyu ni ndege wa kale kwa hio

    mwanadamu yupo karibu naye,kwenye Qur’an kaelezewa kwenye

    Surat Al-Naml 27:20-22 katikaBaibilia katajwa kwenye Taurat,Leviticus 11:13-19 na kwenyeDeuteronomy 14:18.

    Wamisri wa kale wakimtukuzana wakimuona kuwa ni mtakatifuna hata kuchorwa kwenye makaburiyao. Huko Uajemi huonekana kamaalama ya thamani na kumuweka

    kama ni kiongozi wa ndege wote.Katika kitabu Mantiq al-Tayrna Aar, kitabu chenye maanaMkutano wa Ndege utaona namnaHudhud alivyotukuzwa kuwa yupo juu kuliko ndege wa aina yoyoteyule.

    Baadhi ya nchi za Ulayahumuona Hudhud ni mwizina katika zile nchi za Kaskaziniza Ulaya zijulikanazo kamaScandanivia, Hudhud ni uchuroakilia huwa kila mtu anatetetemekakuona kama anabashiria vita. Watuwa Estonia wakimsikia Analia,hujua kuna vifo vitatokea nahubashiri kuwa anapolia hutokeavifo vingi vya ng’ombe.

    Wayunani wa kale wakimwitamfalme wa ndege. Wayahudi katikamwaka wa 2008 walimtukuz nakumfanya alama ya nchi yao. HukoAfrika Kusini katika Chuo Kikuucha Johannesburg, nembo ya Chuohicho ina picha ya Hudhud. HukoUjerumani kwenye Manispaaya Armstedt, wao katika makotiyao wameweka beji ya Hudhudwakati nchini Morocco huuzwasokoni ikiwa ni dawa kwa maradhimbalimbali, ingawa Serikali inapigamarufuku lakini ukenda katikamaduka ya Morocco utamkutaHudhud anauzwa akiwa mzimaau mabaki yatokanayo na ndegehuyu huuzwa na kutokosekanawanunuaji.

     Hudhud tumuenzi au

    tumuangamize? Jawabu unayowewe. Fawtana na mie katikamakala hizi wanyama waliotajwakatika Qur’an. Atakayofwatia nimbwa.

    WAENGEREZA wamewezakumtambua na kumpa hifadhi Hudhud katika karne ya 18

    ANNUUR NEW.indd 13 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    14/20

    14  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016MAKALA/MASHAIRI

    TUFUNGENI SHAABANRajabu i ukingoni, aula kukujuzeni,Na Shabani i njiani, kesho kutwa si mwakani,Mbeleye ni Ramadhani, si baidi kwa mizani,Shabani imewadia, tujiandae kufunga.

    Muhammad adinani, alikifunga Shabani,

    Pima wake uthamani, ujisaili kwanini,Thuma ujitathimini, kwa RAHMANI unani,Shabani imewadia, tujiandae kufunga.

    Hakuacha asilani, kuifunga maishani,Siku moja 'sijedhani, bali wote karibuni,Mimi nawe kulikoni, kutoifunga Shabani,Shabani imewadia, tujiandae kufunga.

    Twaridhika tuna nini, nijuzeni ikhiwani,Kulikoni na kwanini, tusiifunge Shabani,Tumgeze adinani, kwa kuifunga Shabani,Shabani imewadia, tujiandae kufunga.

    Haya shime waumini, wa Bara na Visiwani,Tutie nia moyoni, ya kuifunga Shabani,Ya ILAHI tuauni, tujeifunga Shabani,Shabani imewadia, tujiandae kufunga.  ABUU NYAMKOMOGI

    Riziki nakupongeza, kwa uloinena kweli,Kadhia ulodokeza, si ya puya ni ya kweli,Hukutaka kuchagiza, kwa kuipamba kwa kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Ni haki uloeleza, kwa kila mpenda kweli,Kwa hilo anokubeza, si mwingine mcha kweli,Aso na njema ruwaza, ila ya kupinga kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Hukutaka kwendekeza, habari ziso za kweli,Au umma kuukwaza, kwa kuipindua kweli,Ama dira kupoteza, kwa kuikiuka kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Hukutaka kwao 'izza', kwa kukengeusha kweli,Wala kujipendekeza, kwa wapinzani wa kweli,Ukweli ukawajuza, lengo isimame kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Kuna wataokubeza, kwa kuitongoa kweli,Pamwe na kwa kuuliza, Bungeni jambo la kweli,Mengi watahanikiza, dhidiyo yaso ya kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    MDINI nakueleza, watakuita kwa kweli,Mambo uloyauliza, wajibu kama si kweli,Wasanze kuhanikiza, dhidi yako yaso kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Ninotaka kukujuza, kwa kuitongoa kweli,Maadui 'meongeza, kosalo kulonga kweli!

    Kwa ulimwengu wa giza, adui msema kweli!RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Adharusi endeleza, dhidi ya wakana kweli,Wasaka tonge na 'feza', na vyeo viso vya kweli,Hata wakikupuuza, ALLAH shahidi wa kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    Akudumishe MUWEZA, katika kunena kweli,Pamwe na kuwahimiza, wengine kunena kweli,Mwisho ninakupongeza, kwa kuitangaza kweli,RIZIKI 'menena KWELI, MASHEKHE kosalo nini?

    ABUU NYAMKOMOGI

    SWADAKTA, MBUNGE WA MAFIA!(MH.RIZIKI BINT SHAHARI)

    Kutoka kibanda cha miti

    hadi Kituo cha elimu SinzaInatoka Uk. 20ambao walifanya juhudi zao kwakujitolea mali nguvuzao na kufanikishauwepo wa Masjid Nurna kuendelezwa mpakasasa.

    Hata kama Msikitihuo wa matope ulihitajifundi, lakini waowenyewe waliwezakujitoa na kuwezakuujenga kwa ajiliya kupata sehemu

    ya kufanyia ibada nakusomeshea watotowao kwani Madrasapia ilikuwepo tokeaawali.” Anaeleza ImamMalange.

    Mbali ya kusajili,timu hiyo ya uongozipia ilifatilia namnaya umilikishwaji waardhi hiyo kisheriakwa ajili ya shuhughulimbalimbali za kidini,hali ilikwenda hivyokidogo dogo mpakamiaka ya 1990s.

    “Hapakuwa nautaratibu ulio bora

    katika mikakatiya uongozo lakinitunaweza kusemakwamba kwa wakatihuo ndio ilikuwakiwango chao kwakadri walivyo jaaliwana kuweza kusimamiahatua hizo na kuwekamsingi imara wa kituona mpaka sasa kukiahivi kilivyo.” AnaelezaImam Malange.

    Mwaka 1993,upana wa shughuli zakiharakati Msikitinihapo katika sekta yaelimu ziliongezeka

    zaidi kutoka Madrasampaka Shule ya Awali(Nursery School), nailipoka mwaka 2002,kituo kilipiga hatuazaidi kwa kuanzishaShule ya Msingi(Primary School).

    Kwa ujumla vituovyote vinne vyaelimu chimbuko lakeni Madrast Ikhlasi,iliyoanza miaka hiyosambamba na Masjid

    Nur, lakini baadaezilikuja kuunganana Madrasat Islahiya Sheikh Mituro,ambayo aliihamishiaMsikitini kutokanyumbani kwakeilipokuwa awali baada ya kuongea nauongozi wa Msikiti, ilikuunganisha Madrasahizo.

    Imamu Malange,anasema kwa maeneohaya ya Sinza kwamiaka hiyo ya 1980s,Madrsa hiyo ya Al-Marhum Shkh HamisiSaidi Mituro, ilikuwamaarufu zaidi na vijanawengi wa Kiislamu wahapo Sinza, wamepitiakatika Madrasa hiyo.

    “Nakumbuka wakatiShule ya Msingiipo darasa la nne,tukapiga hatua zaidiya kuanzisha Shule yaSekondari, hiyo ilikuwani mwaka 2005, naShule zote hizo mpakasasa zinaendeleakutoa elimu kwa

    vijana wa Kiislamu nazikiwa katika usajilikamili wa Serikali.”Amethibitisha ImamMalange.

    Mbali na kuendeshaShule hizo, lakiniMasjid Nur, chiniya Jumuiya hiyo yaWaislamu Sinza,tayari ina Chuo chaUalimu, na uongoziupo katika hatua zamwisho kukamilishausajili kupitia NACTE, baada ya kukamilishamaelekezo muhimuwaliyopewa.

    “Ni matumaini yetundani ya mwezi watano, mwaka huu, kozindogo ndogo zitakuwazimeanza kama vilemafunzo ya Kompyuta,Ualimu ngazi yaShule za awali, naikapo mwezi wa tisamwaka huu, tutakuwatumeanza kutoa elimuya Ualimu ngazi yaDiploma kwa ngazi yaShule ya Msingi.

    Hata hivyo ImamuMalange, anauelezeamgogoro wa mwaka1997, wa kiuongoziuliyoukumba Msikitinihuo kama ilivyokuwaada kwa miaka hiyokwa suala la mivutanoya kiuongozi katikaMisikiti mbalimbalihususani Jijini Dar esSalaam, ilikuwa ni lakawaida.

    Anasema hali hiyoilisababishwa zaidi na

    toauti za kimtazamo nakra hususani katikasuala zima la utawalana matumizi ya Misikiti jambo ambalo lilikuwalikisababisha kuibukakwa mivutano hiyo.

    Hata hivyo anaelezakuwa mgogoro huokatika Msikiti waoumebaki kama historiaya kukia mafanikio.

    “Kupitia mgogorowetu hapa Msikitini,ambao mvutanomkubwa ulikuwa

     baiana ya Wazee naVijana, nimewezakujifunza kwambavijana peke yao bilakupata kra za wazeewenye busara inawezaikawa tabu kidogokukia mafanikiokwani wakatimwingine vijana jazbazinatawala mmno,lakini uwepo wa wazeehuwa wanapoza preshahivyo mwisho wasiku manasikilizana”.Anasema ImamuMalange.

    “Kwa kuwathaminiWazee, liliundwaBaraza maalum lawazee wa Msikiti,wakiwemo waasisiwa Msikiti wa awalikabisa, ambaowanatupa kra zao nasisi vijana tunasimamiana kufatilia malengo namikakati ya Jumuiya naMasjid.” AnabaianishaImamu Malange.

    ANNUUR NEW.indd 14 5/

  • 8/17/2019 ANNUUR 1228d.pdf

    15/20

    15  AN-NUUR

    SHAABAN 1437, IJUMAA MEI 6 - 12, 2016Makala/Tangazo

    Inatoka Uk. 8

    Zana za mapigano zamuokoa

    Balqis Chelang’at Chepkwony

    makubwa makubwa aumashirika ya bima.

    Hii ilidhihirika ukweli wakepale makampuni mbalimbaliyalipoanza kumgombania,wakianzia na kima cha chini

    cha mshahara cha Kshs 40 000(takriban 482 $ au Tshs 748,300)kwa mwezi wakati huo.

    Ingawa alikuwa hayuposawa kifedha wakati huo, Balqisalikataa kazi zote hizo kwasababu aliamini kufanya kazikatika makampuni ya bima namabenki hayo ya kibiashara,ilikuwa ni haram kwa sheria zaKiislamu.

    “Kha! Atakuwa kashaanzakuwa mwehu!,” Hivyondivyo walivyosema raki nandugu. Lakini kwa upandewake, ilikuwa ni makosana kinyume cha maadili(unethical) kufanya kazi katikamashirika yanayoendekezariba yakipingana na maneno yaMwenyezi Mungu: “MwenyeziMungu ameihalalisha biasharana ameiharimisha riba.…”[Q2:275].

    Alikuwa na yakini kuwaakijitenga na kitu kwa ajili yaAllah (sw), basi MwenyeziMungu atamdia na kitu kingine

     bora kuliko alichokiacha. Alifatamaneno ya Mtume Muhammadkwa nguvu zote.

    “Huwezi kuacha chochotekwa ajili ya Allah, aliyetukuka,ila atakupa kingine bora badalayake.”

    Balqis alipozwa moyona mafundisho ya Uislamuyaliyompa faraja, tumaini nanguvu: “Enyi watu, muogopeni

    Mola wenu, na muwe na kiasikatika kutafuta maisha yadunia, kwani hakuna rohoitakayoondoka bila kupokeavyote ilivyokadiriwa, hata kamavinachelewa. Hivyo muogopeniAllah na mumche, muwe nakiasi katika kutafuta rizki;chukua lile lililoruhusiwa nauwache lililokatazwa.”

    Badala yake, Balqis akaamuakufanya kazi katika kampuniya ukaguzi wa mahesabuiliyoko huko Nairobi, karibuna barabara iitwayo MombasaRoad. Hapo alikuwa akilipwaKshs 10,000 (takriban 120 $au Tshs 187,000) kwa mwezi.Kutoka katika mshahara huo,

    alitenga Kshs 2500 (takriban 30 $au Tshs 46,760) kulipia chumbahuko Eastleigh, sehemu iliyopokiunga cha jiji la Nairobi.

    Ukiachilia mbali gharamanyengine kama matibabu,mshahara wa Balqis haukuwaukimtosha ila yeye aliendeleakuvumilia.

    Baada ya mwezi, akapatakazi nyengine kama msarifu(bursar) wa Shule ya Sekondariya WAMY (WAMY High School)akipokea kiasi cha shilingi zaKenya 20 000 (takriban 241 $ auTshs 374,000).

    Balqis Chelang’at Chepkwony

    Alifanya kazi hapo kwa miezimiwili kabla ya ahadi ya Mungukutimia kwake. Alipokea simuasiyoitegemea. “Naongea naCheleng’at?…,” Mpigaji alihoji.

    “Je, unaweza kujipanga kwaajili ya usaili (interview) wa kaziosini kwetu.”

    Akapata kazi nzuri hapoakiwa mhasibu wa kampuni yamafuta ya Hass (Hass PetroleumCompany) hapo Nairobi.Kampuni hiyo imestawi AfrikaMashariki nzima na maenenoya maziwa makuu na inazidikupanua huduma zake sehemunyenginezo.

    Balqis aliita kampuni hii kama baraka kutoka kwa Allah, kwanindio kampuni pekee Kenyainayotenganisha wafanyakaziwake wa kiume na wa kike nainaruhusu wanawake kuvaamavazi yao ya kidini, ikiwemoniqab (kuziba uso). Kampunipia, imetenga nafasi kwa ajiliya swala na katika nyakati hizowafanyakazi wanaruhusiwakusimamisha kazi zao ili waendekuswali.

    Mshahara wa kuanzia ulikuwamara dufu ya alichokuwaakipokea katika shule yaWAMY. Sanjari na hilo, kampuniimempa mkopo usio na ribaambao amenuia kuutumia kwaajili ya kununua mahali pakuishi Nairobi.

    Kwa sasa, mshahara wake wakila mwezi si chini ya Kshs 130000 (takriban 1,546 $ au Tshs 2,431, 510). Sasa anaelewa vizuri

    zaidi ule usemi wa Mtumekuwa:

    “Huwezi kuacha jambo kwaajili ya Allah, aliyetukuka ilayeye atakupa lengine bora

     badala yake.”Alikataa kufanya kazi katika

    mashirika yanayoenda kwa riba,kwa ajili ya khofu kwa Allahna sasa anafanya kazi katikakampuni inayoruhusu mazingiraya Kiislamu.

    Kulingana na msomi mkubwaaitwae Sheikh MuhammadSwaleh al-Uthaymeen, anatoataarifa ya Ucha Mungu.

     “Al-Muaqun (WachajiMungu) ni wale ambaowanajilinda na adhabu ya Allahkwa kufanya yale aliyoamrishaMwenyezi Mungu na kujiepushana yale aliyoyakataza.”

    Wenye bidii watapata njiaya kufanikisha ndoto zao kwauwepesi kama wakimtegemeaMungu (sio kumtegea). Vituunavyotaka kuwa navyo kamakazi nzuri, nyumba nzuri,gari zuri, mke mwema, utajirina mengineyo yanapatakanakiurahisi iwapo utajiegemezakwenye uchaMungu.Qur’an haikuacha hilo: “Naanayemwogopa [anayemcha]Mwenyezi Mungu, (MwenyeziMungu) humfanyia mambo yakekuwa mepesi.”[Q 65:4].

    Hata njia yako kuelekeapeponi itafanywa rahisi na huundio ufanisi mkubwa na wakweli.

    Mafanikio kwa hivyoyanakiwa kwa daraja ya

    kumtambua Mwenyezi Munguna kufuata maamrisho yake.Ndoto zako zote zitatimia kamaunamtumaini yeye kupitiaucha Mungu wako, na Yeyeatakusahilishia njia yako na hofuna mashaka yote yatakuondokakichwani mwako.

    Ili kujenga daraja kati yamafanikio na wewe, uchaMungu lazima uzingatiwe.Kuwa mcha Mungukunamaanisha kuitafuta dini yahaki, kujua maamrisho (halal naya haram) ya Mungu yaliyopokatika maandiko matakatifu yahiyo dini ya kweli, na kuyafanyiakazi. Kuna ambao wamepatamafanikio bila ya kuwa wachaMungu. Haya “mafanikio” yakidunia hayatamsaidia akhera.

    “Je, kuna faida gani mtukuupata ulimwengu wote nakuyapoteza maisha yake?”[Marko 8:36].

    Balqis sasa ameolewa, naamejaaliwa kupata watotowawili wa kiume. Wanandoa

    hao walifurahi kumpa mtotowao wa kwanza jina laMuhammad. Tarehe 30 Januari2010, Nairobi, alizaliwa mtotomwingine. Balqis alibarikiwakuwa na mtoto wa pili, na siku7 baada ya kujifungua, mtotoakaitwa rasmi jina la Ahmad.

    Balqis sio mpenzi pekee waMtume Muhammad. Gazetila The Times linaripoti kuwa“Muhammad kwa sasa ni jinala pili maarufu baada ya Jackkwa kupewa watoto wa kiumeUingereza na linatazamiwakushika namba moja ikapomwanzoni mwa mwaka kesho,uchunguzi wa The Timesumegundua.

    Na Januari 2005, makala yaThe Guardian ilisema kwamba:

    “Huko Brussels, Mohammedlimekuwa jina maarufu zaidikwa watoto wote wanaozaliwakwa miaka minne iliyopita.”

    Pamoja na hilo, katika kitabuReligion on the Rise, Hofmannanasema: “…kwa miaka kadhaasasa, ‘