Zanzibar Daima Online Na. 11

Embed Size (px)

Citation preview

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    1/14

    Toleo nambari 11/09 June 2014

    ZanzibarDaimaOnline

    SIASA. UCHUMI . MICHEZO. ELIMU . DINI. UTAMADUNI .KILIMO. BURUDANI.

    ListingFREE

    FACEBOOK/ZANZIBARPROPERTIES

    F WWW.ZANZIBARPROPERTIES .COMPANY

    W TIWITTER/ZANZIBARPROPERTIES

    T

    [email protected]

    a.Our Marketing is second to none.

    b. We advertise in all major portals.c. As well as being top search engines.d. we can give your property lets hugeexposure

    You will see the list of applicants we

    may have for your property and yourproperty will be uploaded to oursite and the portals there and thenbringing the delay to almost zilch.

    WHYCHOOSEUS?

    CALL US:+255773620202

    LANDLORDS

    ABOUTUSCOMPANY

    CALL US:+447588550153W W W . Z A N Z I B A R P R O P E R T Y .C O M P A N Y

    ZANZIBARPROPERTIESH O M E N O T A H O U S E

    www.zanzibarproperties.company

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    2/14

    VICE PRESIDENT ADVERTISINGBrian Mahoni

    VICE PRESIDENT Daima & BRANDBob Trembesi

    MARKETING MANAGERMatt Sloben

    COMMUNICATION MANAGERBrad Saragih

    COMMUNICATION COORDINATORBobby Barongan

    SENIOR MARKETING SPECIALISTFabio Contong

    EDITORIAL DIRECTORAlain Bogosiong

    ART DIRECTORKamituo Kusdi

    EDITOR AND PROJECT MANAGERLurah Kosnan

    SENIOR PROJECT EDITORMatt Koplak

    PROJECT COORDINATORJan Hasselbaink

    ASSOCIATE ART DIRECTORSteven Galonan

    SENIOR GRAPHIC DaimaERKim Kamandanu

    PHOTO COORDINATORLucas Lavale

    COPY EDITORSGeorge Bohamen

    PRODUCTION MANAGERKakeane Minggat

    PRODUCTION ASSISTANTBakari Sagna

    CONTRIBUTORSLara Sanusi, Silvian Gidali,

    Martin Lumer, George Sapulete

    www.magazine.com

    stylesmagazine Daima

    arida hili lina wasiwasi kwamba lile kun-

    di linalojitambulisha kama watetezi wa

    mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili

    visiwani Zanzibar ni mabaki ya wale

    waliopinga Maridhiano ya Wazanzibari

    tangu yalipoanza Novemba 2009 na ambao muda

    wote wamebakia kwenye nafasi ya kungojeamuda wa kulipiza kisasi chao kwa Maridhiano

    hayo.

    Hawa ni wanasiasa waliokuwa wakifaidika na

    mvurugano wa Wazanzibari, ambao wakiutumia

    kujikweza mbele ya wenzao wa Tanzania Bara na

    pia kuwatishia kwamba kama wasingeliwasaidia

    kusalia madarakani Zanzibar, basi nchi nzima in-

    gelikuwa kwenye zahama. Kundi hili, ambalo kwa

    siasa za Zanzibar limepachikwa jina la wahafid-

    hina, haliwakilishi kwa namna yoyote Zanzibar

    yenye ustawi na mustakabali mwema. Ni kundi la

    giza!

    Itakumbukwa kuwa kuelekea kuzinduliwa kwaBunge Maalum la Katiba, jarida hili lilitumia safu

    hii wito wa kuwataka wawakilishi wa Zanzibar

    kwenye Bunge hilo waende kama Wazanzibari na

    sio watetezi wa mirengo ya vyama vyao vya siasa.

    Hawakufanya hivyo.

    Walikwenda wakibeba ajenda finyu za vyama

    vyao, wakiwacha nyuma ajenda pana ya Zanzibar.

    Matokeo yake wakazitumia siku zote za awali ku-

    umbuana na kuiumbua Zanzibar. Wakajeruhiana

    na kuijeruhi nchi yao mbele ya macho ya walim-

    wengu. Jukwaa walilopaswa kulitumia kujitetea,

    ndilo waliloligeuza la medani ya kupigania.

    Wakaondoka wakiwa wanachiria damu, Zanzi-

    bar ikiwa taabani.

    Hivi sasa kundi hili la giza limeamua kuen-

    deleza mapambano yake dhidi ya Zanzibar

    ndani na nje ya Zanzibar. Jarida hili limepokeataarifa kwamba ule mpango wa kuiangamiza

    Serikali ya Umoja wa Kitaifa unaosimamiwa

    kijuujuu na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni

    (CCM), Salmin Awadh Salmin, umewiva. Kwam-

    ba wanataka kuhakikisha kuwa ndani ya kipin-

    di hiki kilichobakia kabla ya uchaguzi wa 2015,

    serikali hiyo inaporomoka, na kwamba baada

    ya uchaguzi huo, Zanzibar haitakuwa tena na

    haja ya kuwa nayo.

    Walio kwenye mpango huo kwa upande wa

    Zanzibar, kwa mara nyengine wanatumia

    mgongo na nguvu za Chama cha Mapinduzi

    (CCM) upande wa Bara. Wanawatisha kwamba

    uhai wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibarni sawa na kifo cha Muungano. Wanasema

    kwamba ili kuulinda Muungano, lazima serikali

    hiyo iuliwe.

    Lakini wasichokisema na ambacho Jarida hili

    linasikitika ikiwa CCM na serikali yake upan-

    de wa Tanzania Bara utakuwa haukijuwi ni

    kwamba kinachopiganiwa ni kulinda madaraka

    yao kwa gharama yoyote iwayo hata ikiwa

    gharama hiyo ni kuirejesha Zanzibar na, hivyo,

    Tanzania nzima nyuma.

    [Muhariri]Mohammed Ghassani

    Jarida hili linapenda kuonya na kutoa wito huu

    kwa wale wote wanaodhani kuwa Maridhiano

    ya Wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa

    ni kwa maslahi ya Chama cha Wananchi (CUF)

    na hasara kwa CCM tu. Tunawaambia kwamba

    Maridhiano haya ni ya Wazanzibari. Ni kwa ajiliyao, yalitokana na wao na ni miliki yao.

    Tunawataka waache kufikiri kwa matumbo yao

    na badala yake watumie vichwa vyao kuwaza

    nini itakuwa hatima ya Zanzibar nje ya Maridh-

    iano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kama wa-

    nadhani kurudi nyuma si kazi na wala hakuna

    maafa yoyote kwao na kwa maslahi yao, wajipe

    muda mdogo kuwafikiria wanasiasa kama wao

    katika nchi za Kenya, Liberia na Yugoslavia.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ina

    wasaa wa kutosha kama wao hawana wa kuji-

    funza.

    Zama zimebadilika. Wazanzibari wa 2001 sio

    tena wa 2014.

    J

    Viongozi wa Zanzibar

    fikirini mara mbili

    MHARIRI MKUUAhmed Rajab

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis

    Email: [email protected]

    COMMUNICATION MANAGERHassan M Khamis

    WAANDISHIJabir Idrissa

    Email: [email protected]

    Foum KimaraEmail: [email protected]

    Ally SalehEmail: [email protected]

    WASAMBAZAJImzalendo.net

    zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook

    MATANGAZOHassan M Khamis

    Simu: +44 7588550153Email: [email protected]

    WASIALIANA [email protected]

    JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective

    233 Convent WaySouthallUB2 5UH

    Nonnstr. 2553119 Bonn

    Germany

    www.zanzibardaima.net

    Zanzibar DaimaOnline

    Timu Yetu

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    3/14

    YALIYOMOTAARIFA

    Tunawaomba radhi wasomaji

    wetu kutokana na kusitishwa

    kwa machapisho ya makala

    yetu......

    ZANZIBAR NI NCHI YA KITU KIDOGO 11-14

    MAKADA WA CCM WANAIMBA NYIMBO MBAYA 07-10Matangazo 09 -10

    WAHAFIDHINA WA ZANZIBAR, IZIKENI HISTORIA CHAFU 02

    MGUU MBELE MGUU NYUMA 15-18

    DEMOKRASIA NA UKOMO WA UONGOZI 19-22Zanzibar, visiwa vya michezo 16

    TAARIFA 01

    11

    15

    01 Toleo la 11 Toleo la 11 02

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    4/14

    Wahafidhina Zanzibar, izikeni historia chafu kablahaijawazika nyinyi

    tazamo wa kihis-toria unaotumiwana wahafidhina waZanzibar kuhalalisha

    upinzani wao dhidi ya maridhia-no ya Wazanzibari miaka minnebaada a Serikali ya Umoja wa Ki-taifa, una mapungufu makubwa.Ikiwa hoja ni kwamba Chamacha Mapinduzi (CCM) na Cha-

    ma cha Wananchi (CUF), kamavyama viwili vikubwa na pekeevinavyoongoza siasa za Zanzi-bar, haviwezi tena kushirikianakuongoza kwa sababu ya tafautizilizojitokeza baina yao kuhusi-ana na Muundo wa Muungano,basi upungufu wa kwanza nikwamba hoja hii haiangalii his-

    toria katika uhalisia wake.

    Msukumo wa kihistoria ambao ndio uliozaamjengeko wa kijamii na kitamaduni wa Zanzibarunazungumza hadithi tafauti. Kwamba Wazan-zibari ni watu mchanganyiko na kwamba kupitiamchanganyiko huo ndipo maisha yao yanapok-wenda mbele katika kila nyanja iwe ya kisiasa,kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

    Kila mara, mwenendo wa siasa za nchi hii zili-podharau au kukandamiza dhati hii ya mchang-

    M

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    03 Toleo la 11 Toleo la 11 04

    anyiko, basi mustakabaliwa visiwa hivi ulitiwa re-hani na kuingizwa katika

    majaribu makubwa. Kwamfano, hakukuwa na hajaya kufanyika Mapinduziya 1964 ikiwa wafanyasiasa wa wakati huo, ku-toka pande zote, waliizin-gatia dhati hii.

    Pili, hata kwa kutumuiahayo hayo mapokezi ya

    historia wanayoyaaminiwahafidhina wetu, badohistoria hiyo si sehemu

    salama kwao kujifichia,maana ni gofu lililojaawoga, kujishuku na kuto-kujiamini. Bahati mbayakwao ni kuwa gofu hililina mlango mmoja tu wakutokea ambao umean-dikwa: Maridhiano naUmoja wa Kitaifa.

    Mwangwi unaosikikandani, kwa hakika unawa-fukuza wasikae gofuni

    humo. Ni mwangwi wamatendo yao. Kwa hivyo,ni ama kupita katikamlango huu au ni kuba-kia ndani ya jengo hilowakawa wamekwama nakuikwamisha nchi katikakhofu, woga na kutoku-

    jiamini kama ilivyokuwakabla ya 2010.

    Na

    Mohammed Ghassani

    Sehemu ya wananchiwa Zanzibar kisiwaniPemba ikijumuikana wenzao kwenyekampeni ya kuungamkono mapendekezo yaMuundo wa Muunganowa Serikali Tatu, tarehe

    1 Mei 2014 kwenyeUwanja wa GombaniKongwe, Chake Chake.

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    5/14

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    05 Toleo la 11 Toleo la 11 06

    na baadaye mikutanoyao ya hadhara baadaya Bunge hilo kuahirish-wa, utagundua kwambahuenda wahafidhina waZanzibar wanaona mauajiya 2001 yalikuwa ni ten-

    do la kistaarabu na, kwahivyo, la kutukuzwa nakurejewa tena na tena kilaikipatikana nafasi.

    Ndio maana ya kauli zaoza kuutetea Muunganowa serikali mbili na kuto-kuitoa nchi kwa kipandecha karatasi. Kundi hili ambalo kwa hakika sikubwa kama sauti yake

    inavyosikikana linanadikwamba Maridhiano ya2009 kilikuwa kitu kibayasana kwao na hivyo ni

    jambo la kuepukwa kadiriinavyowezekana.

    Kitu pekee kinachodhi-hirika kwenye haiba yawapingao Maridhiano yaZanzibar ni ukosefu waowa upeo wa kilimwengu.

    Zanzibar si nchi pekeeulimwenguni iliyowahikupitia historia iliyonayo.Ziko zilizopitia historiambaya zaidi. Pia SMZ si

    Nitafafanua. Kwanza,msimamo wa waha-fidhina hao wa kujidhanikwamba peke yao ndiowazalendo wenye haki yakuitawala Zanzibar unamakosa mengi ya kisay-

    ansi na hauwezi, hati-maye, kuifikisha Zanzibarpopote zaidi ya penyemfundo na mkwamomwengine wa kisiasa nakiuchumi.

    Kadiri wanavyotumiahistoria kuhalalisha ukaidiwao kwa Maridhianona Umoja wa Kitaifa,ndivyo wanavyokwenda

    wenyewe kwenye upandeusio sahihi wa historia,siasa na mustakabali wanchi ndivyo wanavyo-simamia upande sio wahoja.

    Zanzibar imeinuka paletu ilipojali mchanganyikowake na kila ilipopuuziahilo imeporomoka. Zanzi-bar ikiporomoka, wao na

    ahli zao pia hawatakuwasalama. Mwenye kutakasalama yake hataendeleakujifungia kwenye gofuhili la historia, maana

    serikali pekee iliyoingiamadarakani kwa vuruguza umwagaji damu nakuishia kuyatumia mada-raka hayo vibaya dhidi yawatu wake. Ziko zilizoku-wa kandamizi kuliko hiyo.

    Dunia imejaa mifanomingi. Utawala wa AdolfHitler uliwatendea unya-ma mkubwa Mayahudi karibuni nusu milioniwalitiwa katika kambiza mateso, wengi waowakafia humo na wenginewakakimbia nchi zao zauzawa. Lakini watawalawaliofuatia, kwa kujuwa

    machungu yanayobebwana ndugu za wahangahao na kuthamini mai-sha ya watu, wakaombaradhi na kufanya jitihadaza kuwashirikisha tenaMayahudi katika mfumowa maisha ya Ujerumanikisiasa, kiuchumi, kijamiina kitamaduni.

    Katika nchi ya Afrika

    Kusini, siku za ubaguziwa rangi zilisababishamachungu makubwa kwa

    jamii ya Waafrika weusi.Kitu cha mwanzo alichoki-

    ni kujihalalishia vitisho,woga na kutokujiami-ni. Mwenye mapenzi yakweli kwa Zanzibar, basihataupa mgongo mlangowa Maridhiano na Umojawa Kitaifa, maana ndio

    pekee utakaomtoa.

    Mwenye akili timamuZanzibar, hasa kiongozimwenye kundi la wafuasiatatafuta njia muafaka yakuifanya historia imsaidiekupiga hatua mbele kamakiongozi wa watu anayeji-amini. Na ni mwangwi ulewa kwenye gofu alimojif-ungia ndio unaomwambia

    hivyo. Ndio unaomfukuza:Toka humu. Pita kwenyemlango wa Maridhiano naUmoja wa Kitaifa, uendezako!

    Kwa vyovyote vile, mta-zamo wa kihistoria hau-wezi kuzalisha wahafidhi-na, maana busara yakeinasema kitu tafauti naunganganizi wa mambo

    yasiyokuwa na maana.Inasema kuwa kujuwatukuendako ni kwa kuju-wa tutokako na kupaele-wa tulipo. Na ili hilo lifan-

    fanya Nelson Mandela,baada ya kuingia mada-rakani, ilikuwa ni kuun-da Serikali ya Umoja waKitaifa na Tume ya Ukwelina Maridhiano. Leo hiimachungu yanazidi kuy-

    eyuka baina ya jamii hiimoja yenye mchangan-yiko kama wa Zanzibar.

    Hiyo ndiyo mifano yakuigwa Zanzibar. KamaHitler alivyofanya, unaziwa kutisha umeshafa-nyika Zanzibar. Kamamakaburu walivyofanya,ubaguzi wa hali ya juuushafanyika Zanzibar. Na

    haya yanaendelea hadisasa. Ni Maridhiano naUmoja wa Kitaifa tu ndiyoyaliyofungua nafsi zetu,kama alivyosema mu-ombolezi mmoja katikamazishi ya karibuni yaP. W. Botha kuwaambiaWaafrika Kusini: Bury thehistory, before the historyburies you, yaani izike-ni historia kabla historia

    haijawazikeni nyinyi.

    yike, ni lazima tukumbukena tujifunze kwa kukum-buka huko. Kwamba ikiwakuna mabaya yoyoteyaliyotutokezea, basitupate somo la kujifunzayasijirudie tena.

    Historia ya Zanzibar nishuhuda wa ubaguzi namatokeo yake maba-ya, kukiwemo kudidimiakiuchumi, kielimu nakisiasa. Ukaidi hausaidiikitu, maana hata ma-cho ya kawaida yanaonakwamba wenzetu wengiulimwenguni, waliokuwakama sisi, wameendelea

    kusonga mbele sana kwasababu kile kinachotukuz-wa Zanzibar, yaani uba-guzi, kinadharauliwahuko. Anayeamini hasa

    juu ya mtazamo wa his-toria anakuwa mtu wamwanzo kupingana naubaguzi. Kwa hivyo, mta-zamo wa kweli wa ki-historia huzalisha watuwenye uwezo wa kubadi-

    lika na sio vinganganizi.

    Ukiwasikiliza walivyoku-wa wakipwaga kwenyeBunge Maalum la Katiba

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    6/14

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    07 Toleola 11 Toleo la 11 08

    a Salmin Awadh Salmin kuibua raiyenye sura ya kiroja, si bure, baliana lake jambo. Kwamba atawas-ilisha hoja binafsi kwenye Baraza la

    Wawakilishi kutaka kushawishi wajumbekuridhia utashi wake wa kuitaka Serika-

    li ya Mapinduzi Zanzibar iitishe Kura yaMaoni kuwauliza wananchi kama wangaliwanairidhia Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK), ni wazi kuwa amedhamiria ubaya.

    Amedhamiria ubaya kwa Zanzibar nakwa watu wake walioko ndani ya nchiyao ambao wanachokipata hukitumia pia

    kwa kusaidia watu wa familia zao walio-ko Afrika ya Mashariki. Sehemu kubwa yawananchi hao wanahitaji amani, utulivu,umoja na mshikamano, mambo yanay-oenziwa na siasa za maridhiano zilizo-

    jengewa msingi mwaka 2009.

    Salmin ana akili timamu na anajua vizurimaana ya kile anachokipigania katika raiyake hiyo. Anajua fika kuwa kwa asli ya

    L

    ilivyopatikana, siyo tu SUKni kitu adhimu kwa nchi,bali pia kinapaswa kuen-ziwa na kulindwa kamamboni ya jicho.

    Huyu ni Mjumbe wa Bara-za la Wawakilishi an-ayewakilisha wananchi

    wa jimbo la Magomeni,mjini Unguja, akiwa piaMwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Baraza inay-osimamia sekta ya Uchu-mi na Fedha. Anashikiliapia wadhifa wa Mjumbewa Kamati Kuu ya Hal-mashauri Kuu ya Taifa ya

    Chama cha Mapinduzi(CC-CCM).

    Kiongozi wa hadhi hiihata siku moja haiweze-kani akatoa rai bila yakuwa ameitafakari kwakina. Siamini pia kwambaanapigania jambo ana-

    loliwaza peke yake. Hatakidogo.

    Kwa rai yake, atakuwa an-awakilisha makada kad-haa wa chama chao wenyemawazo yanayofanana,kushikana na kushikama-na. Hawa wana ajenda

    iliyojificha lakini ambayoinaonekana kuwa ni balaakwa nchi na watu wake.

    Niliposikia kupitia mkuta-no wa hadhara uliofanywana Umoja wa Vijana waCCM wiki iliyopita kwam-ba bado Salmin Awadh

    anayo nia ya kuwasili-sha hoja binafsi barazani,nimezidi kuamini kuwahawa makada wa CCMwamedhamiria kweli kui-tia nchi katika mtihani kwakuichezea amani iliyost-awi kutokana na siasa zamaridhiano.

    NaJabir Idriss Jabir

    Mwakilishi Vuai Shamsi Nahodha [Kushoto] na Muheshimiwa Salmin Awadh Salimin wakiwabadilishana mawazi

    Makada wa CCM wanaimba nyimbo mbaya

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    7/14

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    09 Toleo la 11 Toleo la 11 10

    Alipoamua kushindanana Spika Kificho, SalminAwadh alikuwa anajua pa-sipo shaka yoyote kuwayeye kama Mwenyeki-ti wa Kamati ya Kudumuya Baraza inayohusika naUchumi na Fedha, alikuwakatika kikao cha kamati yauongozi kilichoidhinishamsimamo uliomo kwenyewaraka huo.

    Alikuwa ndani ya kikaokuandaa msimamo. Aliku-wa katika timu ya kamatiya uongozi iliyoongozwana Spika Kificho kwendambele ya Tume ya Maba-

    diliko ya Katiba ya Jaji Jo-seph Warioba kuwasilishamsimamo huo kama ndiomaoni ya baraza kuhu-su kupatikana kwa katibampya.

    Na kumbukumbu za Bara-za zimethibitisha ukwe-li huo kwamba SalminAwadh alikuwa mmoja wawajumbe waliofuatana naSpika kuongoza msafa-ra wa kwenda kuwasili-sha waraka kwa Tume ya

    Salmin Awadh anasemayumo kwenye maandaliziya mwisho mwisho kui-kamilisha hoja yake kab-la ya kuifikisha mezanikwa Spika Pandu AmeirKificho ambaye akikutaimekidhi vigezo ataiwas-ilisha mbele ya Kamati yaUongozi ya Baraza kwamajadiliano.

    Kamati ya Uongozi ikiridhi-ka kuwa hoja hiyo inawezakuwasilishwa, ataruhusuiwasilishwe barazani. Ita-kapowasilishwa na iwa-po muwasilishaji ataung-wa mkono na tayari

    wawakilishi kutoka CCMwalishaahidi kuwa watai-unga mkono itajadiliwakwa nguvu na kupita.

    Ninavyojua siku zote,Baraza hupokea kwamikono mingi hoja binaf-si inayolenga kuongezauimara wa taifa na siyokuudhoofisha umoja namshikamano wa wanan-chi na taifa lao. Sasa je, hiihoja ya makada wa CCMinayotaka kuhoji serika-

    Warioba.Anajua pia kwamba yalemaoni yaliyomo kwenyewaraka, ndiyo yaleyalewaliyoyatoa wawakilishiwakati wa semina wali-yoandaliwa kujadili mus-takbali wa Zanzibar kati-ka ujio wa katiba mpya yaJamhuri ya Muungano.

    Alichokifanya SalminAwadh ni kufikiria zaidimaslahi ya chama chakekuliko maslahi mapana yaWazanzibari na nchi yao. Nihuyuhuyu aliyeanza kupi-ga jaramba akisema Zan-zibar haitaweza kuchangiagharama za Muungano na

    hivyo haistahili kutafutamamlaka kamili.

    Salmin Awadh akijinasibukufahamu vyema siri yahali ya kiuchumi ya Zan-zibar, anasema ina uchu-mi mdogo usiotosha kui-wezesha kujitegemea nakwa hivyo itahatarishafaida kubwa inayopata ki-uchumi kwa kushirikianana Serikali ya Muungano.

    Akasema kwamba itaku-

    li ya umoja iliyokuja kwashida sana, inawakilishamaoni ya walio wengi auni kitu cha kutaka kufu-rahisha watu wachachewenye malengo ya kifisa-di?

    Kwa jicho langu na wengiwanaofuatilia mwenen-do wa Salmin Awadh nawenzake katika miezi yahivi karibuni, siioni nia nje-ma ya makada hawa am-bao nawaita wahafidhi-na. Ni ujinga mtu kuaminikuwa hawa wanadhamiriakuimarisha umoja na kuz-idi kutandika misingi yamaridhiano kisiasa.

    Hebu turudishe nyumakidogo mti wa saa. SalminAwadh ambaye kwa kuwakwake muwakilishi piani Mjumbe wa BungeMaalum la Katiba, ndiyealiyeibua ushindani wa ki-toto dhidi ya Spika Kifichoakimshutumu kuandaawaraka unaoweka baya-na msimamo wa Barazala Wawakilishi kuhusu Ra-simu ya Katiba mpya.

    Alimsakama Kificho akise-ma waraka aliuandaayeye na wenzake bila yakushirikisha utaratibu wakikanuni wa kutoa warakanamna ile. Amesema hivi-hivi kuwa yeye hakushiri-ki na kwamba laiti ange,asingeupitisha warakahuo.

    Akasema yeye na wen-zake katika CCM hawawezikuwa sehemu ya warakahuo kwa sababu unapiga-nia mabadiliko ya mfumowa sasa wa Muunganowa Tanganyika na Zanzi-bar kutoka mfumo uliopowa Muungano wa Serikali

    mbili. Waraka unapiganiamfumo wa serikali tatu nakuipatia Zanzibar mamla-ka kamili.

    Salmin Awadh akasemakwa kuwa anajua sera yaCCM ni ya kutetea mfu-mo wa serikali mbili ka-tika mfumo ulioongeze-wa vionjo, asingethubutukushiriki kupitisha warakaunaokuja na mabadilikoambayo ni kinyume namaslahi ya chama chake.

    wa ni kosa na hasara kubwaZanzibar kutaka mfumo waMuungano wa Serikali Tatukwani utaisukuma katikakulazimika kuchangia kika-milifu gharama za kuende-sha Serikali ya Muungano.

    Salmin ameyasema yotehaya huku akishuhudiwana Shamsi Vuai Nahodha,Waziri Kiongozi kwa miakakumi wa Zanzibar. Picha il-iyojengeka ni kuwa wana-siasa hawa wanaunda kun-di mojawapo ya makada waCCM wanaotamani uraisna hayo kuwa ni maandal-izi ya kujenga mazingira yakuja kuchukua fomu kuta-

    ka ridhaa ya chama chaoutakapofika uchaguzi mkuuwa 2015.

    Hakika makada wa CCMwanatafuta urais kwagharama ya kuua umoja.Na kwa hali hiyo, wakipewanafasi ya kutekelezakile wanachokiandaa,wataipeleka Zanzibarupande siwo. Hiyo ndiyohofu yangu kubwa. Makadawa CCM wanaimba nyimbombaya.

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    8/14

    Zanzibar, nchi ya kitu kidogoZanzibar Daima Zanzibar Daima

    IJUI kama viongozi wakuu waSerikali ya Mapinduzi Zanzi-bar na wasaidizi wao wana-

    jua kuwa rushwa imetapa-kaa kwenye sekta ya utumishi waumma.

    Wala sijui kama wanajua kuwaukweli huo ndio hasa ulioisuku-

    ma serikali kuondoa uzito na kutunga sheriaya kupambana narushwa ikiwemo kuanzishamamlaka mahsusi kwa jukumu hilo.

    Basi kama hawajui, huo ndio ukweli na ukwelimtupu. Katika utumishi wa umma kuna rushwana athari zake zinaonekana wazi.

    Wananchi wanalalamika hawapati huduma

    s

    Barabara ya Wete-Konde ikiwa imeendelea kujengwa kwa zaidi ya mwaka wa tano sasa,huku pakiwa hapana dalili ya kumalizika kwa karibu. Matokeo yake wananchi wanaoishikando ya barabara hiyo na watumiaji wake wanaambulia kuwa wahanga wa vumbi na hivyoafya zao kuwa hatarini

    11 Toleo la11 Toleo la 11 12

    hii na ile; wanalalamikakwamba wanakwamish-wa na ofisa huyu na yule;wanalalamika kunyimwa

    haki zao mpaka watoe kitukidogo (KK).

    Hivi karibuni, waziri an-ayehusika na utumishi waumma na utawala bora,Haji Omar Kheri, aliliam-bia Baraza la Wawakilishikuwa mipango inakamil-ishwa ya kuanzisha mam-

    laka ya kupambana narushwa.

    Malalamiko ya wanan-

    chi sasa yamekuwa ya-kibebwa kwa ukakamavumkubwa na wajumbe waBaraza hilo chombomahsusi cha Zanzibar kwaajili ya kutunga sheria nakuisimamia Serikali.

    Wajumbe kila wanapoi-pata nafasi wakati wa

    mijadala, wanalalamikakwa kueleza malalamikoya wananchi. Wanatajana mifano ya malalamiko

    hayo; wanataja shida wa-nazopata wananchi katikakupata huduma.

    Kuna malalamiko ya mao-fisa wakubwa, wa katina wadogo, kujiingizakwenye mienendo ya ku-fuja mali ya umma, fedhana vifaa.

    Kutoka kwaMwandishi Wetu

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    9/14

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    13 Toleo la 11 Toleo la 11 14

    Ufujaji unafanywa kwanjia mbalimbali. Utakutaofisa wa wizara au taasisiya serikali anatajwa kwakutumia vibaya gari yaserikali. Labda anaende-sha gari aliyopewa kiofi-

    si mpaka usiku, ambaosi muda wa kazi, na hanakibali.

    Au anatumia gari ya ofisikwa kazi zake binafsi, tenapengine ni shughuli za bi-ashara. Yawezekana ana-fanya hivyo kwa kutumiamafuta yaliyonunuliwakwa fedha za serikali.

    Utasikia ofisa mwingineanatajwa kushiriki kupan-ga, kutekeleza na kun-ufaika na mpango wa kuu-za gari ya serikali kinyumena taratibu.Waweza kusikia ofisa am-eidhinisha malipo ya gariya Sh. 150 milioni lakinithamani halisi ya gari in-ayonunuliwa ni Sh. 100milioni.

    Wakati fulani ofisa mmojakatika Idara ya Uvuvi ali-idhinisha malipo ya Sh. 47milioni ya gari iliyotumika

    ambayo bei yake halisi ili-kuwa ni Sh. 22 milioni. Kwaufupi, ofisa huyu alitumiafedha nyingi kununua garikongwe, ununuzi usiotaki-wa kisheria serikalini.

    Utasikia jengo la seri-kali limekodishwa kwamwekezaji au mtu binafsitu pasina kufuatwa utara-tibu wa manunuzi unaohi-taji sheria ifuatwe na kilaanayetaka aombe rasmi.

    Katika siku za mwanzomwanzo, Rais Dk. Ali Mo-hamed Shein alipokuwaakizuru mikoani kukagua

    shughuli za maendeleo,alikutana na malalamikomengi ya migogoro ya ar-dhi.

    Rais akasikika akisemawale maofisa wa serikaliwaliosababisha migogorohiyo, waishughulikie waowenyewe mpaka imal-izike.

    Huko nyuma, kuliwahi

    kubainika kwamba mao-fisa wa Idara ya Ardhi naUsajili, walijigawia viwan-

    ja viwili mpaka vitatu kila

    mmoja vya kujenga nyum-ba ambavyo vilivyokusud-iwa kugaiwa kwa wanan-chi wenye shida.

    Zipo tuhuma kwambaofisa mmoja katika Idara

    ya Ujenzi na Utengene-zaji Barabara (UUB) iliyochini ya Wizara ya Miun-dombinu na Mawasiliano,ameigeuza mitambo yaujenzi ambayo ni ya seri-kali, kuwa ni mali yake naanaikodisha kwa wajenzi(wakandarasi) wa baraba-ra.

    Bado wananchi hawajasa-

    hau namna mawaziri kad-haa wa serikali iliyopitana waliopo walivyohusi-ka kukodisha majengo yaserikali kinyume cha she-ria.

    Wapo maofisa wa serikaliwanatuhumiwa kutumiamadaraka vibaya. Pengineni kwa kufukuza watumi-shi wenzao bila ya kuzin-gatia kanuni za utumishi,

    ikiwemo kumpa mtumishimtuhumiwa nafasi ya ku-

    jitetea kabla ya kumuadhi-bu.

    Wapo viongozi serikaliniwamegawa zabuni kwanjia ya upendeleo baadaya kupata malipo haramukwa waliopewa zabunihusika.

    Bali wapo watendaji wal-iotumika kuvuruga ucha-guzi na hivyo kusababishawagombea walioshindwakutangazwa washindi.Tena, katika mwenendokama huo, matokeo yauvurugaji huo yamesaba-bisha fadhaa kubwa katikanchi ikiwemo machafukona vifo vya raia waliokuwawakipinga uvurugaji.

    Kuna utamaduni unaokuaZanzibar wa viongozi waserikali kudharau amri zamahakama na hivyo ku-sababisha wale waliopa-ta manufaa kutokana naamri hizo kukosa haki zao.

    Mfano mzuri wa uovuhuu, ni uamuzi wa kesiya uvamizi wa shambala mzee Abdalla Shar-

    iff wa Shakani, Wilaya yaMagharibi, Unguja, am-baye pamoja na kushindakesi mwaka 1993, ute-

    kelezaji wa hukumu hau-jafanyika. Mpaka anafari-ki dunia 2011, haki yakehakuipata.

    Mara kadhaa polisiwametafuta visingizio vya

    kutotekeleza hukumu hiyohuku mazingira yakione-sha wazi kuwa wamepatamaelekezo ya wakubwaserikalini.

    Hukumu ya kesi hiyo yamadai imewakumba vi-ongozi mbalimbali waan-damizi serikalini na wa-fanyabiashara wenyeuswahiba na viongozi

    wakuu wa serikali na Cha-ma Cha Mapinduzi (CCM).

    Imekuwa ni mtindo kwamiaka mingi sasa Zanzi-bar, maofisa wa serikalikuruhusu wafanyabiasha-ra kuingiza nchini vyakulavibovu na kuuzwa.

    Wakati fulani, mfanya-biashara mmoja anayea-giza mchele, sukari na

    unga wa ngano, alivunjakufuli za ghala ambamomchele mbovu ulifungiwana serikali na kufanikiwa

    kuutorosha nje ya kisiwacha Unguja ambako uliuz-wa.

    Inasemekana baada yakuzungushwa, uliuzwakisiwani Pemba amba-

    ko sasa kuna wagonjwawengi wa saratani (kan-sa) mpaka kuwashangazamadaktari wa HospitaliKuu ya Kansa nchini Ocean Road Hospital.

    Madaktari wanajiuliza in-akuaje wagonjwa wen-gi wa saratani wanaofikaOcean Road Cancer Cen-tre kutoka Zanzibar, idadi

    kubwa ya hata asilimia 80wanatoka kisiwani Pem-ba.

    Wenzetu hawa wameku-wa wakilazimishwa ku-tumia mchele huo huo wakila siku ambao haufikiikiwango kinachokubalikakiafya kwa sababu hawa-na njia nyingine ya kubad-ilisha. Unapokuwa mtu wakipato kidogo, unakula kile

    kilicho mbele yako hunauchaguzi.

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    10/14

    Mguu mbele mguu nyuma, lazima

    Katiba Mpya ipatikane

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    uyasimulia yaliyoji-ri katika mijadala yaBunge Maalum laKatiba, ambalo kwa

    sasa limeahirishwa kupitaBunge la Bajeti, kutakuwa nikujirudia, kwani yalishuhudi-wa, yalisikika na kuzungumz-wa nchi nzima na nje ya mi-paka yake kwa wanaofuatilia

    siasa za Tanzania. Kuna yaliyofu-rahisha, na yaliyokirihisha.Nilivutiwa sana na mchakatomzima huu tangu na baada yaRais Jakaya Kikwete kukabidhi-wa Rasimu ya Pili ya Tume yakukusanya maoni kuhusu Katibampya ya Jaji Joseph Warioba nabaadaye Rais kuwateuwa wa-

    jumbe 201 kujiunga na wabungewa Bunge la Muungano na wa-

    jumbe wa Baraza la WawakilishiZanzibar kuunda Bunge hiloMaalum.

    Hatua hizo zote zilibua hisia zamatumaini kwa wananchi wapande zote mbili Tanganyikana Zanzibar kwamba hatimayesasa kuna njia ya kuzitatua zilezinazotajwa kuwa kero za mu-ungano, si kwa jengine zaidi ya

    kuuimarisha na kuupa mtaza-mo mpya kulingana na wakatina mabadiliko, miaka 50 tangukuundwa kwake.

    Watanzania waliposikia RaisKikwete atalifungua rasmiBunge Maalum la Katiba tayarikuanza kazi, macho na masikioya watanzania yakaelekezwabungeni mjini Dodoma, kwa

    15 Toleo la 11 Toleo la 11 16

    K

    hotuba iliyotarajiwa kuwa yakihistoria. Mimi nikitegemeaingekuwa sawa na ile wakati ali-powahutubia viongozi wa vyamavya kisiasa siku chache kabla yakutangazwa majina ya wajumbewa bunge maalum la katiba.Akikamilisha hotuba ile Rais Kik-wete alisema alichukuwa akitoani rai tu hana na maelekezo walamajibu na jibu wanalo wao, yeyenasubiri majibu kama wanavyomajibu Watanzania wote. Ilikuwahotuba ya matumaini.

    Lakini hotuba ya Rais Kikwetebungeni bila ya kutafuna mane-no kinyume ilizusha mgawanyikowa fikra na mitazamo, kuanziabungeni kwenyewe kati ya wa-

    jumbe wa bunge hilo maalumla katiba kutoka Chama tawala

    cha Mapinduzi CCM na wale wavyama vya upinzani isipokuwa tuTLP cha Augostino Mrema nahata ndani ya jamii ya Watanza-nia.Kilichotarajiwa sicho kilichot-

    okea

    Wengi walitarajia ingekuwa fupina yenye wasia-maneno yenye

    NaMohammed Abdurahman

    Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na Mbunge wa Singida MheshimiwaTundu Lisuu, wakiwa kwenye viwanja vya Gombani Pemba

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    11/14

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    12/14

    Demokrasia ina uhusiano gani na ukomo wa uongozina ugombeaji?

    Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad.

    oja kati ya lawama kub-wa zinazoelekezwa kwaupinzani katika Jamhuriya Muungano wa Tanza-nia ni kwa viongozi wake

    wakuu kuendelea kugombea nafasi zaokwa muda mrefu. Wakosoaji wao wa-

    M

    nawaambia kuwa huu si muonekano wademokrasia bali ni uimla unaojificha ndani

    ya upinzani.

    Kabla ya kuendelea mbali, niweke wazikwamba mimi ni muumini wa demokrasiaya uwazi na ukomo, lakini hili halina maa-na na wala si kweli kwamba ukomo ndiodemokrasia na kinyume chake ni uimla ama usultani kama wengine walivyoupa-gaza jina. Nitalifafanua hili kwa ushahidi.Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja

    kumekuwa na matukio yanayohusianana dhana hii ya ukomo na demokrasia.

    Kwa mfano, Chama cha Demokrasia naMaendeleo (CHADEMA) kiliwatimua Dk.Kitila Mkumbo na kumbebesha lawamakali mbunge wake wa Kigoma Kaskazi-ni, Zitto Kabwe. Nyuma ya hapo, Chamacha Wananchi (CUF) nacho kikamtimuambunge wake wa Wawi, Hamad RashidMohamed, na wenzake.

    Hao wote waliofukuzwa CUF na CHADE-

    Zanzibar Daima Zanzibar Daima

    19Toleo la 11 Toleo la 11 20

    NaFoum Kimara

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    13/14

  • 8/12/2019 Zanzibar Daima Online Na. 11

    14/14

    Zanzibar Daima

    23 Toleo la 11 Toleo la 11 24

    ilinufaika na simulizi za babu

    yangu, Juma Mzee Jimba, tu-

    lipokuwa tukitembea nyum-

    bani kwake Kwa Karagosi

    (Mwembetanga), tukitokea Dar es Sa-

    laam tulikokuwa tukiishi. Akinielezea

    historia ya magwiji wa Kriketi, gofu,

    kandanda (mwenyewe akiita Futboli)

    tangu miaka ya 1940 hadi 1960 waki-

    wemo kina Marehemu Ahmed Iddi Mjasiri, Shaaban

    Antar, Bwan Smati (Smart), Mohamed Aoud Mfaran-

    sa, Kassim bin Mussa, Hijja Saleh Abdulmajham na

    wengineo. Orodha ni ndefu na kila mmoja alikuwa na

    fani na kipaji chake.

    Abdulmajham ni mmoja wa wachezaji waliokuwa na

    kipaji cha hali ya juu na aliiwakilisha Zanzibar katika

    timu za taifa za michezo mitatu: Kandanda, Hoki na

    N

    Zanzibar Daima

    Timu ya Zanzibat baada ya kuchukua kombe la Mashindano ya Gossage mwanzoni mwa miaka ya 1960

    tunajuwa tutaka fainali!

    Katika ngazi ya vilabu vikub-

    wa wakati huo, mpira ulikuwa

    na msisimko wa aina yake.

    Ushindani mkubwa ukiwa

    kati ya Vikokotoni na Malindi

    na Miembeni na Kikwajuni.

    Vyengine ni Mwembeladu

    na Kisimajongoo iliyokujakufa baadaye.

    Kwa ujumla wake, michezo

    ikitiliwa maanani mashuleni

    ikiwemo ile ya riadha. Ura-

    ki wa vilabu vya michezo

    Tanganyika na Zanzibar uli-

    changia zaidi katika kuipa

    umuhimu michezo na hasa

    baada ya Muungano. Safari

    za kupeana zamu za waka-

    ti wa Sikukuu za Pasaka

    zilikuwa na shauku ya ki-

    pekee - Miembeni Sports

    Club walikuwa na udugu naYoung Africans, Kikwajuni

    na Sunderland (sasa Sim-

    ba), Vikokotoni na Malindi na

    Cosmopolitan.

    Hizo ni zama ambazo timu

    za Tanganyika zikiazima

    wachezaji kutoka Unguja

    zinapokabiliana na mash-

    indano. Nakumbuka Yan-

    ga ikimkodisana Hijja Saleh

    aliyekuwa wingi wa kulia

    na Cosmopolitan kuwatege-

    mea Abdulmajham kuche-

    za nafasi yoyote isipoku-wa mlinda mlango: kuanzia

    ulinzi, kiungo hadi mshambu-

    liaji na Mohamed Kassim ku-

    toka Malindi katika nafasi ya

    mshambuliaji wa kulia. Hayo

    yaliendelea hata baadaye.

    Kwa mfano, mtoto wa mare-

    hemu Hijja Saleh, Saleh

    Hijja, aliwahi kujiunga na

    Yanga miaka ya 1980 na

    Cosmo ilikuwa na Joseph

    Kazi, mchezaji maarufu wa

    kiungo kutoka KMKM na

    Mansab Abubakar, mlinzi

    wa kati kutoka Malindi. Wote

    waliwahi kwa kipindi kire-

    fu kuichezea timu ya taifa

    ya Zanzibar. Abdul Mutiy

    Ajmi alijiunga na Cosmopo l-itan. Mutiy alikuwa ni mlin-

    da mlango wa aina yake na

    wa kutegemewa hata katika

    Timu ya Taifa ya Tanzania.

    Miongoni mwa michuano in-

    ayokumbukwa akiwa langoni

    ni ule wa Kombe la Afrika dhidi

    ya Madagascar ambapo Tan-

    zania iliyowajumuisha akina

    Hemed Seif, Abdulmajham,

    Mohamed Kassim, Mwana

    Abushiri, Mustafa Choteka,

    Kitwana Manara na Abdullah

    Luo, ilishinda mabao 3-2.

    Udugu baina ya vilabu vya mi-

    chezo Bara na Visiwani uli-

    kuwepo pia katika fani

    nyengine kama vilabu vya

    Hoki, ambapo wenyeji wa

    timu ya mchanganyiko ya

    Hoki ya Zanzibar ilikuwa na

    ushirikiano na Bantu ya Dar

    es Salaam na pia vilabu vya

    taarab ambapo kutoka Zan-

    zibar ni pamoja na Akhwan

    Swafa (Malindi) na Dar es

    Salaam ni Egyptian MusicalClub, Zanzibar Extra na Al-

    Watan.

    Hayo ni ya wakati wa

    kuelekea uhuru na Mapin-

    duzi. Safari ijayo, tutaangalia

    michezo visiwani Zanzibar

    baada ya Mapinduzi.

    Kriketi. Mchezaji mwengine

    ni Marehemu Zaghaloul Ajmi.

    Mnamo miaka hiyo ya enzi

    ya ukoloni, Zanzibar iliku-

    wa pekee kwenye kanda ya

    Afrika ya Masharikiiliyokuwa

    ikijulikana kwa ustadi katika

    fani tafauti za michezo na

    kuchuana na timu za uge-nini zilizokuwa zikika kwa

    matembezi, iwe wanamaji wa

    Uingereza, wacheza Kriket

    kutoka Bara Hindi na kadha-

    lika. Huo ulikuwa ni wakati

    ambapo michezo ilipewa ki-

    paumbele na ilikuwa sehemu

    ya mtalaa mashuleni na jamii

    kwa jumla.

    Mapema miaka ya 1960, mi-

    chezo - na hasa kabumbu

    - ilishamiri zaidi Afrika ya

    Mashariki nzima na hasa

    chini ya yale mashindanomaarufu ya kila mwaka ku-

    wania kombe lililojulikana

    kama Gossage. Mashinda-

    no hayo yalizihusisha nchi

    nne za Afrika ya Mashariki -

    Kenya, Uganda, Tanganyika

    na Zanzibar.

    Wakati Uganda ikivuma kwa

    akina Ouma na Masajagge;

    Kenya kwa akina Kadenge

    na Moses Wabwai, Sungu-

    ra na Ali Kajo; Tanganyika

    kwa akina Mbwana Abushi-

    ri, Hemed Seif, Kibunzi naJohn Lymo; Zanzibar ilivu-

    ma kwa akina Abdulmajham,

    Mohamed Kassim na Mussa

    Bakari. Inasemekana kuwa

    wakati mashindano hayo ya

    Gossage, daima Uganda iki-

    omba isiumane na Zanzibar,

    kwani kilikuwa ni kikwazo

    kwao. Waganda walikuwa na

    usemi: Tukiifunga Zanzibar,

    Zanzibar, visiwa

    vya michezoNaMwanamichezo Wetu