21
Imani ya Wamennonite Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT) Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2014

Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

  • Upload
    others

  • View
    113

  • Download
    5

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT)

Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2014

Page 2: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

2

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Yaliyomo

Utangulizi 3

Menno Simons 3

Sura ya 1 Mianzo 5

Sura ya 2 Imani Yashirikishanayo Madhehebu Mengine (sehemu ya 1) 7

Sura ya 3 Imani Yashirikishanayo Madhehebu Mengine (sehemu ya 2) 9

Sura ya 4 Kanisa na Serikali 10

Sura ya 5 Maisha ya Kanisa 12

Sura ya 6 Ibada ya Kanisa 14

Sura ya 7 Maisha ya Kikristo 15

Sura ya 8 “Maneno Magumu” ya Yesu 17

Sura ya 9 Kuwa Mwanafunzi wa Yesu 18

Sura ya 10 Imani ya Wamennonite Duniani 20

Mikazo Kuu katika Imani ya Wamennonite 21

Page 3: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

3

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Utangulizi

Somo hili limetoka katika kitabu “What Mennonites Believe” (“Imani ya Wamennonite”), kilichoandikwa na John C. Wenger. Kilibadilishwa kwa ajili ya masomo ya T.E.E. (Theological Education by Extension) na Mchungaji Victor Dorsch kwa ajili ya makanisa ya Mennonite katika Afrika Mashariki, hasa Kanisa la Mennonite Tanzania na Kenya Mennonite Church.

Kitabu kilibadilishwa kwa kibali cha Mennonite Board of Missions, Elkhart, Indiana, USA, shirika lililochapisha kitabu.

Masomo yaliandaliwa zaidi na kupangwa katika masomo 10 na Mchungaji Joseph Bontrager. Waliotafsiri katika Kiswahili ni Mrs. Rhoda Mtoka na Mch. Joseph Bontrager.

Tunaamini somo hili litaleta faida kwa makanisa yetu kwa kueleza misingi ya dhehebu la Mennonite na kuelekeza waamini kurudi kwa neno la Mungu kama msingi wa imani yetu.

“Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.”

1 Wakorintho 3:11

Menno Simons (1496-1561)

Menno Simons alizaliwa mwaka 1496. Aliwekewa mikono kuwa kasisi katika kanisa la

Katoliki mwaka 1524 akiwa na umri wa miaka 28. Kwa taarifa yake, aliishi maisha ya amani

na raha, ingawa ulikuwa ni wakati wa mabadiliko.

Wakati huo katika nchi ya Ujerumani, mtawa kwa jina ameitwa Martin Luther alikuwa

alishaleta masuko katika kanisa la Katoliki. Alikuwa ametamka mashaka yake kuhusu

mafundisho yao mengine na kuhusu matendo mabaya ya viongozi wa kanisa kinyume cha

mafundisho ya Biblia. Pia mwaka 1525 katika nchi ya Uswissi, lilitokea kundi la watu huko

Zurich waliofundisha ubatizo juu ya ungamo wa imani yao. Walijitahidi kuijenga imani yao

juu ya Biblia tu na kuufuata mfano wa Yesu katika maisha yao, mbele ya desturi za kanisa na

amri za serikali.

Katika nchi ya Uholanzi nyakati zile kulikuwepo mashindano kuhusu dini, na kulikuwepo pia

mashindano katika roho ya Menno. Kanisa lilikaza hali ya mkate na divai katika misa,

kwamba ni mwili na damu ya Yesu halisi. Wengine walikuwa wanafundisha mkate na divai

kuwa mifano tu ya mauti ya Bwana. Hata Menno alikuwa na mashaka mapema wakati akiwa

bado kasisi, mashaka yake yalimsumbua. Akanza kulisoma Agano Jipya na akakuta ya

kwamba mafundisho juu ya Meza ya Bwana yanasisitiza maana ya Kristo aliyekufa, wala si

mkate na divai yenyewe.

Halafu, katika kijiji jirani, kulitokea mambo yaliyofanya mashaka ya Menno kuzidi. Mshonaji

jina lake Sicke Freerks, aliuawa kwa kukatwa kichwa kwa sababu alikuwa amebatizwa tena

akiwa mtu mzima kufuatana na imani yake. Kanisa lilifundisha kwamba watoto wachanga

wabatizwe ili wao pia wapate wokovu, si lazima waamini wenyewe. Menno akayachunguza

Page 4: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

4

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Maandiko tena ili kuelewa ni nani abatizwe, akagundua kuwa si watoto wadogo bali

wanaoamini wabatizwe.

Wakati huo wote, Menno aliendelea kuwa kasisi katika kijiji chake cha nyumbani cha

Witmarsum, Uholanzi . Alipata kujulikana na kuheshimika kwa ajili ya mahubiri na ustahili

wake. Lakini maswali yake na mashaka yake yakazidi.

Tarehe 30 Januari 1536, Menno alitangaza katika ushirika wake kuwa imani yake ilikuwa

imebadilika, jambo lililosababisha kuacha ukasisi. Ilimbidi ajifiche kwa sababu ya hatari

katika kuachana na kanisa. Alijiunga na kundi dogo la Waanabatisti, wakiongozwa na Obbe

Philips, akiendelea kuchunguza Maandiko. Baadaye walimwomba kushika uongozi, akaweka

katika maombi huku akisubiri mwongozo wa Mungu. Walipomrudia tena, alikubali na

kuwekewa mikono.

Kwa miaka 25, Menno alijitahidi kukusanya na kuunganisha makundi mbalimbali ya

Waanabatisti wakati wa mateso na hatari nyingi. Akamwoa mke kwa jina la Gertrude. Akawa

hana nyumba yake akihama huku na huko pamoja na jamaa yake, kwa vile wakuu wa serikali

walitangaza thawabu ya pesa na kusamehewa makosa kwa yeyote atakayetoa taarifa

kuhusu mahali alipo ili akamatwe.

Menno aliandika vitabu na kuingia katika majadiliano mengi. Mafundisho yake na ushauri

wake ulileta umoja na msimamo kati ya makundi mbalimbali ya Waanabatisti, hivyo

wakaanza kuitwa “Wamenno.” Miaka yake ya mwisho aliishi kwa usalama lakini katika hali

ya umaskini. Baadaye akapatwa na ugonjwa uliodhaniwa kuwa kiharusi, uliomsababisha

kutembea na fimbo na kujiita kilema. Menno alifarika 31 Januari, 1561, akiwa umri wa miaka

65.

kutoka Gospel Herald, March 3, 1993, na kutafsiriwa na J. Bontrager, 2013

Page 5: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

5

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 1: Mianzo (Historia Fupi) Uswisi, 1525

Mnamo Januari 21, 1525, siku ya Jumamosi jioni, katika mji wa Zurich, Uswisi, kundi la vijana wa kiume wapatao 15, walikusanyika ndani ya nyumba, kwa ajili ya kujifunza Biblia, maombi na mjadala juu ya imani. Miongoni mwao, vijana watatu, ambao ni Feliz Manz, Conrad Grebel, na George Blaurock, walitokea baadaye, kuwa viongozi muhimu katika mshikamano mpya uliotegemewa kuleta matengenezo kanisani. Ghafla, George alisimama na kumwendea Conrad na kusema, “Nibatize mimi. Nibatize mimi kwa jina la Mungu pamoja na ubatizo wa kweli wa Kikristo.” Ombi lake lilileta mshangao kwa wengine. Walijiuliza kwa nini atake ubatizo, wakati aliishabatizwa miaka mingi iliyopita akiwa mtoto. Conrad hakuwa na mamlaka kutoka kanisani ya kubatiza, na ilikuwa ni kinyume cha sheria kumbatiza tena mtu yeyote, aliyekwishabatizwa. Mamlaka ya serikali yaliweza kutoa faini, kuwafukuza kutoka mjini au hata kifo kwa kuvunja sheria.

George alipiga magoti mbele ya Conrad akisubiri. Conrad alienda jikoni, akachukua kikombe na kukijaza maji, na kumbatiza George kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wengine pia, ndani ya chumba wakataka wabatizwe, na ndipo George akawabatiza kila mmoja wao. Mwanahistoria wa awali aliandika, “Katika hofu kuu ya Mungu, ndipo kwa pamoja walijitoa kikamilifu kwa Bwana. Walijithibitishia wenyewe kwa kila mmoja wao juu ya huduma za injili, na kuanza kufundisha juu ya imani na kuitunza.”

Hapo baadaye, watu waliosisitiza kubatizwa tena, waliitwa “Waanabatisti,” neno la Kilatino lenye maana ya “kubatizwa tena.” Wenyewe walijiita kuwa, “Ndugu wa Kiswisi” (yaani, “Swiss Brethren”).

Uholanzi, 1536

Katika muda kama huo, ambapo ubatizo ulikuwa unafanyika Zurich, viongozi wengine katika Ujerumani na Uholanzi, walianza kutafiti maandiko na kuhoji mamlaka ya Kanisa la Kirumu. Menno Simons alikuwa ni kuhani wa Kirumi, Uholanzi. Menno alihangaika kuelewa mafundisho ya Biblia ikilinganishwa na mapokeo ya Kanisa la Kirumi. Alisoma baadhi ya maandishi ya Luther, yaliyoelezea kwamba, maandiko yanapaswa kuwa na mamlaka juu ya desturi na mapokeo ya Kanisa, na akaanza kuhubiri kutoka ndani ya Biblia. Menno alipoona Waanabatisti wakiteswa na kuuawa kwa ajili ya imani yao, alianza kuhisi kuwa na hatia, ya kuendelea katika maisha yake ya kuridhika kama kuhani, wakati wengine wakijitolea uhai wao. Mnamo Januari 1533, Menno alimwomba Mungu, kumsamehe dhambi zake zote, kumuumbia ndani yake moyo safi, na kumpatia hekima, roho na ujasiri katika maisha mapya ndani ya Kristo. Menno aliacha ukuhani na akaanza kuwafundisha waumini wapya wa Waanabatisti, na kuwasaidia kupanhilia maisha yao ya kikanisa. Baada ya hapo, maisha mengi aliyoishi Menno yalikuwa ni ya kusafiri na kujificha ili kukwepa kukamatwa na mamlaka ya serikali. Lakini, kutokana na uongozi wake, makanisa mapya yakaanza kujulikana kama “wafuasi wa Menno,” au “WaMennonite.”

Mateso

Kule kujaribu kufuata mafundisho ya Agano Jipya juu ya wokovu, ubatizo na kanisa kulifanya Waanabatisti waingie katika mgogoro na maafisa wa kanisa na serikali. Utaratibu wa kuwabatiza watu wazima, na kukataa kubatiza watoto, ulitangazwa kuwa siyo halali. Aidha, Waanabatisti walielewa vizuri sana kuwa, utii wao wa hali ya juu kabisa, ulikuwa ni kwa Mungu, na siyo kwa serikali, hili likawa ni chukizo zaidi kwa mamlaka. Matokeo yake, serikali

Page 6: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

6

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

na kanisa la serikali wakafanya kazi kwa pamoja ili kujaribu kuuangamiza mshikamano mpya wa kidini. Wengi walifungwa; wengi pia walihukumiwa kifo kwa kunyongwa. Felix Manz alikuwa wa kwanza kufa. Alikamatwa na kufungwa mara nyingi kwa ajili ya kuhubiri na kubatiza. Hatimaye, mwaka 1526, Manz alihukumiwa kifo cha kuzamishwa majini. Alituhumiwa kwa kuanzisha kanisa tofauti, akifundisha kuwa Mkristo hatakiwi kutumia upanga (vita), na kubatiza mara ya pili tena. Januari 5, 1527, miaka miwili tu, baada ya ubatizo wa kwanza, Manz alipelekwa Mto Limmat, huko Zurich, alifungwa mikono na miguu na kusukumwa ndani ya mto. Maneno yake ya mwisho yalikuwa, “Mikononi mwako, Bwana, naiweka roho yangu.”

Wengi wao walipitia mwisho wao sawa na huo, lakini, pamoja na mateso, Uanabatisti ulienea kwa kasi miongoni mwa watu. Baadhi walizamishwa majini, wengine waliunguzwa katika moto. Mmoja wa watawala aliwaua Wanabatisti 350, lakini aliona jitihada zake zilikuwa bure. Akasema, “Nitafanya nini? Kadiri ninavyozidi kuua, ndivyo idadi yao inavyozidi kuongezeka.”

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Andika orodha ya mafundisho ambayo Wanabatisti wa kale walijaribu kurejesha Kanisani.

2. Neno “Mennonite” limetokea wapi?

3. Kwa nini mamlaka ya Biblia ilikuwa ya muhimu zaidi ya mapokeo kwa Wanabatisti wa kale?

4. Kwa nini mafundisho ya ubatizo yalikuwa ya muhimu kwa Wanabatisti wa kale?

5. Je! Unafikiri tunapaswa kubatiza upya watu wanaojiunga na dhehebu letu hata kama walikwisha batizwa wangali wachanga katika madhehebu yao?

Page 7: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

7

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 2: Imani Yashirikishanayo Madhehebu Mengine (sehemu ya 1)

Kuanzia siku ya Pentekosti ,madhehebu na makanisa mengi yameanzishwa ulimwenguni kote. Dhehebu ni kundi la watu walio Wakristo wanaokubaliana juu ya mapokeo/imani fulani yaliyowekwa na kujengwa katika misingi ya Biblia. Wakati mwingine tunasahau ni jinsi gani tunavyoshirikishana na Wakristo wengine katika ukweli wa kibiblia.

Wamennonite wanajaribu kufuata na kuishi katika mafunzo ya Yesu, kama yanavyopatikana katika Agano Jipya. Kutokana na msisitizo juu ya Kristo na Biblia, Wamennonite wanayo mambo mengi yanayofanana na makundi mengine ya Kikristo.

1. Mungu Muumbaji (Mwanzo 1). Mungu aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Mungu aliumba ulimwengu na akauita ni “mwema.” Mungu atujua sisi, anatupenda na kutuongoza.

2. Tumeumbwa kwa Mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27). Kwa vile, tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, tunaweza kuwa na ushirika na Mungu, tunaweza kechagua, mema au mabaya, tunaweza kupenda na kuishi milele. Mungu alimwuumba mwanamume na mwanamke-Adamu na Hawa.

3. Mwanadamu alitenda dhambi (Mwanzo 3). Adamu na Hawa hawakubaki katika hali ya kutokuwa na dhambi, waliyokuwa wameumbwa nayo, wakiwa katika ushirika na Mungu. Dhambi ilitokana na mahangaiko kati ya mema na mabaya, kati ya Mungu na Shetani, nyoka. Adamu na Hawa walichagua kumuasi Mungu aliyewaumba, na kumtii nyoka. Hali halisi ya dhambi ni kuvunjika kwa mahusiano baina ya Mungu na kila mmoja wetu, na wala siyo matendo au maneno mabaya tu. Matokeo ya uasi, ikawa kifo. Kwa matokeo ya uasi wa Adamu na Hawa, vizazi vyao vyote vikawa vyenye dhambi na kuhusika katika huu uasi, na uasi unaendelea katika mioyo na fikra za wanadamu wote. (Warumi 5: 19)

4. Mpango wa Mungu wa Ukombozi na Uhuisho (Yohana 3:16) Kwa sababu ya upendo aliokuwa nao Mungu kwa watu aliowaumba, Mungu alifanya njia ya kuwaokoa, kutoka katika kifo, na akawahuisha wawe na ushirika pamoja naye tena na kila mmoja wao. “ Wokovu” huu, ulipatikana wakati Yesu, alipokuja kama mwanadamu, akafa kwa ajili ya dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo wake kutoka kwa wafu. Vitabu vinne vya Injili na Matendo ya Mitume vinaelezea kwa uwazi juu ya kukamilika kwa mpango huu wa ukombozi.

5. Ufunuo wa Mungu (Waebrania 1: 1-2). Agano la Kale ni hadithi ya Waisraeli, wateule wa Mungu wa kuonyesha upendo na uwezo wa Mungu kwa mataifa, na kuandaa kwa ujioa wa Masihi, “Aliye na Upako” wa kushinda uovu na kurejesha tena ushirika pamoja na Mungu Muumbaji. Ufunuo wa Agano la Kale ulipitia katika maneno ya manabii, kupitia Sheria ya Kiyahudi na hadithi ya upendo wa Mungu na uweza wake kwa Wanaisraeli. Agano la Kale lilikuwa ni “Kivuli” cha wokovu wa kweli na maandalizi ya ujio wake Yesu Masihi.

6. Roho Mtakatifu (Yohana 16:13). Roho Mtakatifu ni Mungu pamoja nasi leo, akifanya kazi ya ukombozi ndani ya kila mtu. Roho Mtakatifu anatuonyesha kuwa sisi ni wenye dhambi, anatukaribisha kumwanini Bwana Yesu Kristo na kutuletea maisha mapya (Yohana 3:5-6). Roho Mtakatifu anamwongoza muumini mpya kukua katika maisha yake ya kiroho na kuwezesha huduma ya ujenzi wa kanisa. (Waefeso 4:11-14)

Page 8: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

8

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

7. Biblia (2 Timotheo 3:16). Biblia ni Neno la Mungu lililoandikwa. Roho Mtakatifu anatumia Neno la Mungu kuleta hukumu ya dhambi, huzuni ya dhambi, toba kutoka dhambini, na uaminifu/imani katika Kristo. Biblia iliandikwa na watu. Inatuonesha jinsi watu wa Mungu walivyoamini na kutii katika nyakati mbalimbali ndani ya historia yao. Bado, ni Neno la Mungu, limetolewa kwa watu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Biblia ni mwongozo wa Wakiristo kwa ajili ya imani, utii, upendo na utakatifu.

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Soma kila fundisho 1 hadi 7.

2. Andika ujumbe mfupi kwa kuelezea kwa nini ni muhimu kwetu.

3. Ni fundisho lipi ambalo unapata shida kutekeleza katika maisha yako?

4. Je! Unaona mafundisho fulani ungependa yasisitizwe zaidi katika makanisa yetu? Ni yapi? Eleza.

Page 9: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

9

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 3: Imani Yashirikishanayo Madhehebu Mengine (sehemu ya 2)

8. Wokovu Kupitia Imani (Waefeso 2: 8-9). Wokovu ni hali ya kuwa mzima kiroho na kamili tayari kwa kuwa na amani na Mungu. Kazi ya wokovu kamili tayari kwa wale tunaoamini dhambi zetu zilisamehewa, “tumehesabiwa haki kwa imani”, tumefanywa kuwa haki mbele za Mungu. Matokeo ya wokovu ni matendo mema yaitwayo “Kuenenda katika upya wa uzima”.(Warumi 6:3-4)

9. Kanisa (Mathayo 18:20). Kanisa ni kundi la watu wanaomwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi, na wanao wito katika habari njema, kupitia toba ya dhambi na kuwa na imani katika Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja kwa ibada na kutiana moyo kwa nia moja. Kanisa ni watu waliozaliwa upya tena kwa Roho Mtakatifu.

10. Maombi (Mathayo 6: 9-13). Biblia inafundisha Wakiristo kuomba katika jina la Kiristo. Mungu anasikia na kujibu maombi yetu, ingawa mara nyingi anaweza asijibu kwa njia ile tunayoitaka. Wakiristo huomba kwa ajili ya utakatifu mkuu, uongozi wa kanisa, na kwa wale ambao hawajampokea Yesu, mahitaji ya kila siku, uponyaji kutokana na wasiwasi, hofu, chuki, kinyongo, na mahusiano mabaya na uponyaji wa kimwili. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuomba kwamba Ufalme wa Mungu uje duniani.

11. Maisha Matakatifu (Waefeso 2:10). Matendo mema hayaleti wokovu, bali matendo mema ni matokeo ya wokovu. Imani iokoayo, pia huleta utakatifu, wa moyo na uzima. Yesu ni mfano wetu wa maisha ya utakatifu. Katika maisha ya Yesu ya utakatifu, maneno yake ya huruma yalisikika na pia matendo yake ya upendo katika huduma yalionekana.

12. Ibada. Mungu anayo hamu kuwa watu wake wote wamwabudu yeye “katika roho,” kwa watu binafsi na katika makundi (Waebrania 10:24-25). Mungu Muumbaji, na Mpaji wa vitu vyote, anastahili tumwabudu. Ibada ya Kikristo inajenga imani na utii kwa mapenzi ya Mungu.

13. Kurudi tena kwa Kristo (Yohana 14:2-3). Tegemeo maalum la kanisa ni kurudi kwa Yesu tena katika uweza na utukufu mkuu. Ndipo, atakapofufua wafu na kuhukumu ulimwengu. Atamchukua bibi-arusi wake, kanisa, kuingia katika utukufu wa milele mbinguni. Agano Jipya kinafundisha kwamba kila mtu aliye na baraka za matumaini haya hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu (1 Yohana 3:3).

14. Mungu anawatuma watu wake ulimwenguni (Mathayo 28:19-20). Wakristo wanaamini kuwa watu wote kwa asili ni wenye dhambi mbele za Mungu, wameasi sheria za Mungu, na kupungukiwa na mapenzi ya Mungu, kwa sababu ya kutoweka kwa mahusiano pamoja na Mungu. Kanisa linalo ujumbe wa wokovu unaotakiwa kwa watu wote, kila mahali ulimwenguni, na linatumwa kutangaza matendo ya Mungu kwa wale ambao hawajasikia bado.

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Soma kila fundisho kuanzia 8 hadi 14.

2. Andika ujumbe mfupi kuelezea kwa nini ni muhimu kwetu.

3. Ni fundisho lipi ambalo unapata shida kutekeleza katika maisha yako?

4. Je! Unaona mafundisho fulani ungependa yasisitizwe zaidi katika makanisa yetu? Ni yapi? Eleza.

Page 10: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

10

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 4: Kanisa na Serikali

Watu wa Matengenezo na Waanabatisti wa karne ya 16, waliweka msingi wa kurudi katika Ukristo wa Agano Jipya. Moja ya mafundisho muhimu sana kwa Waanabatisti yalihusu hali ya kanisa na lengo lake katika ulimwengu. Walifundisha kwamba ni lazima kanisa na serikali vitenganishwe.

Hali ya serikali. serikali imewekwa na Mungu. Mungu anasimika na kuondoa wafalme na falme (Danieli 2:2) na anawapa mamlaka ya kutawala (Yohana 19:11). Biblia inafundisha kuamba, Wakristo ni lazima watii mamlaka za serikali (Waarumi 13:1-7; 1 Petro 2:13-14). Ufalme wa Mungu ni tofauti na falme (serikali) za ulimwengu huu. Uwezekano upo wa falme hizi kuingia katika mgogoro na wenzake. Tunaamuriwa kuheshimu na kutii sheria za nchi, lakini serikali inapotutaka sisi kufanya jambo ambalo ni kinyume na neno la Mungu, ndipo hapo linapokuwa jukumu letu kumtii Mungu kwanza (Matendo 5:29). Kazi za serikali ni kusimamia sheria na utaratibu katika nchi ambayo imeundwa na wote, Wakristo na wasio Wakristo. Waumini wa Kikristo wanaishi kama raia wa nchi husika, lakini utii wa msingi ni kwa Yesu Kristo.

Hali ya Kanisa. Kanisa ni ushirika katika upendo, ambapo wanaume na wanawake humpenda Bwana na kila mmoja miongoni mwao. Wakristo hutii sheria na kuishi kwa haki, kwa sababu tamani yao ya ndani ya mioyo yao, ni kumpendeza Kristo, na si kwa sababu ya hofu ya kuadhibiwa. Waumini wa awali walifundisha kwamba “Kristo ni Bwana,” wakitumia neno sawa na lile alilotumia mtawala wa Kirumi kwake binafsi, hivyo hilo likasababisha mateso. Waanabatisti wakaamua kwamba, ili kuwa wafuasi wa Mfalme wa Amani walitakiwa kukubali kuteswa, kwa ajili ya Yesu. Walitakiwa kuwasamehe watu kama Yesu alivyofundisha; na walitakiwa kupenda kama alivyopenda Yesu. Waliamini kuwa wasingeweza kuwa mapolisi au wapiganaji ili kuzuia uhalifu, kama serikali ilivyowataka wafanye. Aidha, waliamini kwamba ili kufuata mafundisho ya Warumi 1, walihitaji upendo wa Mungu umiminwe katika mioyo yao, kama ilivyoelezwa katika Warumi 5:5.

Mlinganisho kati ya kanisa na serekali ya nchi. Kutokano na imani ya Waanabatisti-Wamennonite, zifuatazo ni tofauti zilizoko kati ya kanisa na serikali.

Tumezaliwa chini ya serikali ya nchi yetu. Twaingia kanisani kupitia kuzaliwa upya.

Serikali inajumuisha watu wote, wema na wabaya. Kanisani ni wale “wanaotembea katika ufufuo,” kama alivyosema Michael Sattler. Sattler alikuwa ni mmoja wa Waanabatisti wa kwanza kabisa.

Dhumuni la serikali linajumuisha kusimamia sheria na utaratibu. Dhumini la kanisa ni uinjilisti na malezi ya Kikristo.

Serikali inatawala kufuata sheria na kanuni na “upanga” au bunduki. Kanisa limejengwa juu ya neno la Mungu, ambalo ni “upanga” wa kiroho, na Roho Mtakatifu wa Mungu kuwabadilisha na kuwaongoza wafuasi wake.

Serikali inaweza kutumia faini na vifungo, na katika baadhi ya matukio, hata kifo hutolewa, kama njia ya kudhibiti jamii. Njia pekee inayotumiwa na kanisa ni kumtenga mhusika kutoka katika kundi (Mathayo 18:15-17; 1 Wakorintho 5:13).

Kichwa cha serikali ni mwanadamu. Kichwa cha kanisa ni Bwana Yesu Kristo.

Page 11: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

11

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Serikali itafikia ukomo wake wakati wa kurudi tena Kristo. Kanisa, “bibi-arusi” wa Kristo, ataendelea kuishi milele pamoja na Kristo mbinguni.

Waanabatisti wa Uswisi na Uholanzi, wakijulikana sasa kama Wamennonite, walikuwa ni kanisa la amani la kwanza kwa nyakati hizi za sasa. Waliamini, waliitwa kuwa waletao amani, na hivyo wasingeweza kufanya kazi ya kipolisi au kwenda vitani kwa ajili ya serikali, kwa sababu ilihusisha matumizi ya ubabe na wakati mwingine uuaji. Madhehebu mengine machache pia yalichukua msimamo huo wa kanisa la amani, likiwemo Jamii ya Marafiki (Quakers).

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Kwa jinsi gani Ufalme wa Mungu unatofautiana na falme za ulimwengu huu.

2. Unavyoona, kwa jinsi gani na katika mambo gani Wakristo wanapaswa kuhusiana na falme za ulimwengu huu?

3. Je! Unaamini Wakristo leo wanahitajika kupitia mateso katika safari zao za kumfuata Kristo kama Bwana wao?

4. Je! Unaamini Wakristo wanaweza kutumika kama polisi au wanajeshi? Eleza jibu lako.

5. Je! Kuna masuala ambayo sisi viongozi wakristo tungepaswa kutoa kama changamoto dhidi ya serikali yetu hata kama itatusababishia mateso?

Page 12: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

12

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 5: Maisha ya Kanisa

Uongozi wa kanisa. Kwa vile Waanabatisti walisoma neno la Mungu, waligundua kuwa Bwana alielekeza kila kanisa liwe na wachungaji, wajulikanao kama waangalizi, au wazee, katika Agano Jipya (Matendo 14:23; 20:28). Wachungaji hawa hawakuwa juu ya ndugu na dada waliomo makanisani. Bali baada ya maombi mengi, kanisa liliwachagua, likawawekea mikono juu yao, na kuwaagiza kuwa wachungaji waaminifu wa “kondoo” wa Bwana. Mara nyingi watu hawa walitajwa kama wachungaji, wahubiri, au watumishi wa Bwana. Walitakiwa kuangalia kanisa na kuwalisha waumini wao na kuwalisha chakula kinono chenye utajiri wa neno la Mungu.

Agano Jipya, pia, linataja mashemasi, kama katika Wafilipi 1:1. Karama za kiroho zinazotakiwa kwa waangalizi na mashemasi zimetolewa katika 1 Timotheo sura ya 3. Baadhi ya tafsiri za Biblia zimekwepa tafsiri ya “askofu” kwa sababu ya cheo na uweza, vilivyoambatishwa kwa neno “askofu” katika historia ya kanisa kwa kuzidi inavyostahili, na wamependelea kutumia neno la “mwangalizi.” Waangalizi wanayo majukumu makuu mawili. Wanakuwa ni wasimamizi wa kazi za wachungaji na kusimamia hudumu ya mafunzo.

Katika makanisa mengi ya Wamennonite, mashemasi walitumika katika kuhakikisha juu ya upatikanaji wa mahitaji ya kimwili na ya kifedha kwa waumini ndani ya kanisa (Matendo 6:1-7). Walisaidia kulinda hali ya furaha na amani ndani ya kanisa, na kuangalia hasa, kama kuna mahitaji yoyote ya kifedha miongoni mwa yatima na wajane.

Muundo wa kanisa. Agano Jipya haelezi picha halisi wa muundo wa kanisa. Inaonekana waumini walijiunda katika makanisa ya mitaa na kuteua viongozi wao. Lakini katika nyakati hizo za mwanzo, kazi kubwa iliyofanywa na kanisa, ni juu ya utatuzi wa mahitaji ya waumini, na waliwezeshwa na maisha ya kiroho ya waumini , siyo kwa muundo.

Makanisa ya Kimennonite hayana chombo chenye muundo cha ulimwengu kinachodhibiti maisha yao. Mkutano wa Wamennonite wa Ulimwengu (Mennonite World Conference) ni ushirika wa makanisa ya Wamennonite-Waanabatisti duniani, unaojumlisha waumini waliobatizwa 1.7 milioni, kutoka katika mikutano (conference) 243, na wanaotoka nchi 83.

Kwa kawaida, makanisa ya Kimennonite hujiundia mikutano (conferences) katika maeneo yao, kimsingi ni ushirika, ambapo viongozi wanakutana pamoja kutiana moyo na nguvu, kusaidiana wao kwa wao katika matatizo yanayowakabili na kufikiria namna nzuri ya kuimarisha makanisa katika imani. Mikutano hii yaweza kuunda bodi na kamati ya kuendesha huduma mbalimbali na mipango ya kimisheni. Mfumo wa bodi na kamati zinazoundwa hutofautiana kutoka kundi moja la Wamennonite hadi lingine, na kutoka nchi moja hadi nyingine. Lengo la mikutano na bodi ni kusaidia makanisa kutekeleza majukumu yake, wala siyo kudhibiti kanisa. Waanabatisti walijaribu kukwepa ofisi ndani ya kanisa ambazo zinatawala wengine, bali kutoa huduma. Hawakutaka kurudi tena katika aina ya kanisa la utawala walikokuwa wametoka muda mfupi tu uliopita.

Nidhamu ya kanisa (Mathayo 18:15-20). Tangu mwanzoni, Wamennonite wanaamini kwamba ni lazima Wakristo wasaidiane kufanya yale yanayompendeza Mungu, na kukwepa yale yasiyomtii Mungu. Hii ndiyo huitwa nidhamu ya kanisa. Nidhamu ya kanisa inatakiwa kuwasaidia watu kuwa waaminifu zaidi, mashaidi wafaao, na wanafunzi wa Yesu. Yesu alifundisha wanafunzi wake, kuwa, nidhamu ni kazi ya jamii ya Kikristo, na lengo lake ni urejesho.

Page 13: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

13

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Mashahidi. “Mtakuwa mashahidi” (Matendo 1:8) alisema Yesu kwa wanafunzi wake, muda mfupi kabla ya Kupaa Mbinguni. Wakati kanisa la mwanzoni lilipoanza kusambaratika kwa sababu ya mateso, bado walishuhudia matendo ya Mungu ndani ya Yesu Kristo popote pale walipoenda, na injili ikaenea katika ulimwengu wote. Mitume, akiwamo Paulo, walisafiri kwenda maeneo mengine wakitangaza habari njema ili injili ienee ulimwengu wote kwa Wayahudi na Mataifa, katika sehemu zingine za ulimwengu, zinazojulikana leo hii kama Ulaya, Asia, na Afrika. Katika karne ya 16, Waanabatisti walichukulia maneno ya Yesu kwa umuhimu wa hali ya juu sana, “Enendeni mkawafundishe mataifa yote.” Ufaulu wao katika uinjilisti ilikuwa ni moja ya sababu ya kuteswa sana kwao.

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Viongozi gani tofauti wanatajwa kwenye Agano Jipya?

2. Agano jipya inataja uongozi ambao kwa wakati mwingine hutafsiriwa kama “ Askofu” na mwingine hutafsiriwa “mwangalizi”. Ni neno lipi unafikiri tulitumie? Kwa nini ufikiri hivyo?

3. Je! Unakubali kwamba uongozi kanisani sio kuwatawala wengine bali ni utumishi? Kwa nini waamini hivyo?

4. Elezea hatua za nidhamu kanisani kwa mujibu wa Yesu katika Mathayo 18:15-20. Je! Unadhani kwamba hatua hii itaweza kuhifadhi utakatifu ndani ya Kanisa?

5. Kanisa letu lapaswa kufanya nini kushuhudia kwa uaminifu katika ulimwengu huu?

Page 14: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

14

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 6: Ibada ya Kanisa

Matendo kadhaa ya ibada yanayofanyika katika Kanisa la Mennonite ni kama alama zionekanazo kwa ajili ya waumini, kuhusu imani na maisha yao katika Yesu Kristo. Hayo matendo makuu ni ubatizo wa wanaoamini, mesa ya Bwana, na kutawadhana miguu.

Ubatizo wa maji. Wanabatisti walielewa kuwa, Biblia inafundisha kwamba, ubatizo hauleti wokovu, bali ni mwitikio wa imani ya mtu binafsi, katika moyo wake, tendo la kimwili linaloonyesha mithili ya ukweli wa kiroho. Walisisitizia kuwabatiza tena wale waliobatizwa utotoni, kwa kuwa sasa wanatangaza imani yao kwa Yesu kama ni njia ya wokovu. Imani yao kuhusu watu wazima lazima wabatizwe tena, ikawaletea jina “anabatisti” maana yake, “aliyebatizwa tena.” Ubatizo ni mfano wa mambo yafuatayo:

1. Ubatizo ni alama ya kiroho ya kusafishwa kutoka dhambini. 2. Ubatizo ni alama ya toba/kutubu (Matendo 2:38). 3. Ubatizo ni alama ya kifo chetu kwa dhambi na ufufuo katika upya wa uzima ndani ya

Kristo (Warumi 6:34) 4. Ubatizo ni kiapo au agano pamoja na Mungu ya kutembea ndani ya Kristo, hivyo

unatakiwa uamuzi binafsi wa kweli kweli. 5. Ubatizo ni alama ya ubatizo wetu wa Roho Mtakitifu, anayetuwezesha kushuhudia

Kristo na habari zake njema za injili.

Waanabaptisti walituhumiwa kuwachagulia watoto adhabu ya milele kwa kukataa kuwabatiza. Lakini wao waliamini kuwa watoto wadogo wamejumuishwa katika wokovu hadi hapo watakapoweza kutambua dhambi zao, na kufanya uamuzi wa mema au mabaya.

Meza ya Bwana (Luka 22:7-20; 1 Wakorintho 11:23-33)

Meza ya Bwana ilianza wakati Yesu akisherekea ukombozi wa Wayahudi pamoja na wanafunzi wake, kukumbuka ukombozi wa Waisraeli kutoka Misri na kondoo wa Pasaka akichinjwa kwa ajili yao. Yesu alikuwa tayari kutimiliza kondoo wa Pasaka, kuchinjwa, “mara moja kwa wote”. Yesu alipokuwa akila chakula cha Pasaka, alichukua mkate na akasema, “Huu ndio mwili wangu unatolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivyo kwa ukumbusho wangu.” Ndipo alichukua kikombe na kusema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu”. Mkate ulikuwa wa kawaida na kikombe kilikuwa na mvinyo wa kawaida, lakini Yesu alivioonyesha kama alama za mwili wake na damu. Kuanzia hapo, meza ya Bwana kimekuwa ni sherehe muhimu sana na ukumbusho wa kifo cha Yesu.

Kutawadhana Miguu (Yohana 13:1-17)

Wakati wa chakula cha Pasaka, Yesu aliondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni, na akaanza kuwatawadha wanafunzi wake 12 miguu. Ndipo akawaambia watatakiwa kufuata mfano wake wa kutawadhana wao kwa wao. Wammenonite walio wengi wa leo, wanafuata maneno ya Yesu, wanatawadhana miguu kama ishara ya mwendelezo wa Yesu kusafisha waumini na Wakiristo, kuonyesha heshima kwa mitume wenzao na utayari wa kuhudumiana kila mmoja.

Maswali ya kuchunguza na majadiliano 1. Andika maelezo mafupi kuhusu uelewa wako wa Ubatizo wa maji. Kwa nini tunabatiza?

Kwa jinsi gani inamsaidia anayebatizwa? 2. Andika maelezo mafupi kuhusu Meza ya Bwana. Kwa nini tunaifanya? Kwa jinsi gani

inawasaidia wanaoishiriki? 3. Je! Unafikiri tunapaswa kutawadha miguu katika makanisa ya leo? Kwa jinsi gani

itatusaidia?

Page 15: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

15

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 7: Maisha ya Kikristo

Wanabatisti waliamini kuwa wokovu wa kila siku wa Mkristo unaweza kuonekana katika maisha yake kutokana na neema ya Mungu tu. Kwa imani, kila Mkristo anaweza kupata ushindi wa Yesu pale Kalvari na katika ufufuo.

Ushindi wa Yesu pale Kalvari (Waebrania 2:14-15)

Maneno haya katika Waebrania, yanasema kuwa, Yesu akawa mwanadamu, ili kipitia mauti yake, amharibu Ibilishi aliyekuwa na nguvu za mauti, na kututoa katika utumwa wa dhambi. Msalaba una maana zaidi ya kuleta tu amani kati ya Mungu na mwanadamu. Una maana ya kumpinga na kumshinda Shetani pamoja na jeshi lake! Kifo cha Kristo msalabani kinawezesha waumini kuponywa kiroho na kutembea katika ushindi dhidi ya ulimwengu, mwili na mwovu shetani.

Upendo wa Mungu “wamiminwa katika mioyo yetu” (Warumi 5:5)

Hatuwezi kuishi katika mafundisho ya Agano Jipya kwa nguvu zetu wenyewe. Siyo kawaida, kwa asili ya mwanadamu kusahau mabaya, kuwasamehe wale wanaotuchukia, na kuendelea kupenda mtu aliyetusaliti. Na kwa sababu si rahisi kwa Mkristo kufanya hivi, Mungu Roho Mtakatifu ndiye amiminaye upendo wake ndani ya mioyo yetu. Upendo huu wa kiuungu unatuwezesha Wakristo kusamehe, kuonyesha upendo hata kwa adui zetu, kuendelea kuwa na matumaini mema pale tulipokatishwa tamaa, kurudisha mema kwa mabaya. Msaada wa Mungu na neema kila mara utahitajika ili mtu aweze kutembea katika upendo na utakatifu. Ni lazima mtu aipokee neema yote ya Mungu, kama anataka kutembelea “katika ufufuo.”

Kukua katika neema

Petro aliwatia moyo waumini, akisema, “kueni katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2 Petro 3:18). Yafuatayo ni maneno ya ushauri ya kutusaidia sisi kukomaa ndani ya Kristo na “kukua katika neema.”

a) Itoeni miili yenu kikamilifu kwa Mungu, kila siku (Warumi 12:1).

b) Soma na kujifunza neno la Mungu kila siku (Zaburi 1:2; 2 Timotheo 2:15).

c) Omba kila wakati, kwa kuabudu, kuombea, na kushukuru (Waefeso 6:18).

d) Umtegemee Mungu akupatie nafasi za kushirikisha wengine habari za Mungu na wema na wokovu wake, ili kutimiza agizo lile kuu, “Enendeni ulimenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15-16).

e) Uwe na ushirika na waumini wengine (Wakolosai 3:16-17).

f) Shiriki katika kusanyiko la Wakristo katika ibada (Waebrania 10:25).

g) Pinga majaribio ya ulimwengu, ya mwili na ya mwovu Shetani, yanayotuvuta kufikiri au kufanya yale tunayojua kuwa kinyume cha mapenzi ya Mungu (Yakobo 4:7).

h) Mshukuru Mungu kila siku kwa kutuita kuingia katika ufalme wake, kwa kutupatia baraka nyingi, na kwa kuzidi kutusamehe dhambi zetu (Waefeso 5:20; 1 Wathesalonike 5:18).

i) Toa sadaka na matoleo yako kwa Bwana kwa uaminifu. Uwe wakili mwaminifu kwa yale yote uliyo nayo na kwa yote jinsi ulivyo (2 Korintho 9:6-8).

Page 16: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

16

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

j) Fanya mema kwa njia yoyote ile iwezekanavyo: yaani, kuonyesha huruma kwa wale wenye mahitaji, kuwasamehe wale ambao ni wakorofi, na kutafuta kuleta amani na haki kati ya watu wote (Mathayo 22:34-40).

k) Uwe na mpango wa kutunza maisha yako, kama kipindi cha kufanya kazi, kipindi cha mapumziko, kipindi cha kuburudisha roho yako. Kula chakula bora na kutumia dawa kwa kiasi.

l) Mwamini Mungu akutunze na kukuongoza katika huduma yake (1 Petro 5:6-7).

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Elezea jinsi gani wokovu unaleta utofauti ndani ya maisha yetu ya kila siku.

2. Unafikiri ni kwa nini ilimpasa Yesu kuwa mwanadamu ili kuleta wokovu?

3. Vitu vipi vinavyoweza kuzuia upendo wa Mungu kumiminika ndani ya roho zetu?

4. Andika orodha ya vitu ambavyo vinaonyesha mtu “kukua katika neema”.

5. Soma orodha ya “kukua katika neema”. Andika vitu vitatu vinavyoweza kukusaidia wewe mwenyewe kukua katika neema.

Page 17: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

17

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 8: “Maneno Magumu” ya Yesu

Waanabatisti waliamini yale mafundisho ya Yesu yaliyoitwa “maneno magumu.” Yanaitwa “magumu” kwa sababu yanadai wanafunzi kuachana na desturi zao ili kumfuata Yesu. Na kweli, ni vigumu sana kuyatii.

Tusishtaki mahakamani. Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasiende mahakamani, bali kufanya upatanishi nje ya mahakama (Mathayo 5:26-27; 1 Corintho 6:1-8).

Tusiape. Yesu aliwaambia wanafunzi, “msiape kabisa” (Mathayo 5:33-36), kwa sababu viapo na nyapo zote mbele ya Mungu ni ubatili. Yesu alisema hakuna sababu ya kuimarisha au kutetea ushahidi wetu kwa kuapa.

Tusilipize kisasi. Yesu alisema, “Msishindane na mtu mwovu” (Mathayo 5:38). Yesu alipinga kulipiza kisasi kwa mtu anayetutendea mabaya. Alitufundisha kwamba ni vibaya kutumia sheria kulipiza yule aliyetutendea hayo mabaya. Kutokana na kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu, upendo wetu uwe mkubwa sana kiasi kwamba tusitake kulipiza kabisa.

Tusidai heshima ya cheo. Yesu alituonya tusidai majina ya heshima, kama Rabi, au Baba (Mathayo 23:8-12). Yesu alisemea wale wanaodai kuitwa jina fulani kwa ajili ya cheo chao. Wengine wanahisi kama unawadharau au unawachukia usipowaita kwa jina la cheo chao. Yesu anatushauri kuepuka majina hayo. Uridhike kuitwa kwa jina lako tu. Waanabatisti wa awali na hata Wamennonite wengine sasa wanajaribu kufuata neno hilo kwa kutumia maneno ya Agano Jipya kama vile ndugu au dada, na hata kwa wale walioitwa kuwa wachungaji, mashemasi, au maaskofu. Tunajaribu kulifanya kanisa kuwa ni familia yenye upendo kwa ndugu na dada, badala ya kuwa mahali pa kusifu vyeo.

Msijiwekee hazina duniani. Yesu alionya juu ya kujiwekea hazina duniani (Mathayo 6:19). Yesu anatutaka tuweke hazina zetu mbinguni. Anatuonya juu ya hatari kuwa mali yetu tuliyo nayo inaweza kututawala na mwisho tumsahau Mungu. Kutegemea hazina tuliyo nayo hapa duniani inaweza kuleta uharibifu. Lakini, tukiweka hazina zetu mbinguni na kujenga ufalme wa Mungu, italeta baraka na afya ya kiroho. Njia mojawapo ya kuweka hazina zetu mbinguni ni kuwasaidia wenye haja (Luka 18:22). Wakristo wa kwanza walijazwa sana upendo wa Mungu ukawafanya kuwa na mali yao yote kwa ushirika (Matendo 2:44-45).

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Ni maneno magumu yapi ambayo hayafai sisi kuyatekeleza kwetu leo?

2. Je! Kuna uwezekano wa kutii “neno gumu” katika maana yake ya ndani hata kama hatutatekeleza jinsi alivyosema Yesu? Toa mfano.

Page 18: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

18

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 9: Kuwa Mwanafunzi wa Yesu

Mungu anadai tuwe waaminifu katika maisha yetu ya kila siku. Wakati mwingine, hali hii huitwa “uanafunzi,” ama kujifunza maana ya kuwa mwanafunzi. Mwanafunzi ni yule anayepokea maelekezo kutoka kwa mwingine, kama wanafunzi walivyopokea kwa Yesu.

Uaminifu katika Kuteswa. Mwana wa Mungu akawa mwanadamu ili aweze kutufunulia Mungu na mapenzi yake. Kama mwanadamu, alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote bila kutenda dhambi (Waebrania 4:5). Yesu alikuwa mwaminifu kwa Mungu. Hakushindwa na Shetani na majaribu yake.

Utii wa Yesu kwa Babaye ulisababisha ateseke. Utabiri katika Isaya 53 unaeleza Masihi kama Mtumishi aliyeteseka, atakayebeba masikitiko yetu, atakayekufa kwa dhambi zetu, na ambaye kwa njia ya mateso yake anaweza kutukomboa sisi na ulimwengu wote.

Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa aina ya ufalme alikuwa analijienga. Walifikiri angejenga tena ufalme wa kisiasa wa Israeli. Baada ya Pentekoste walielewa kuwa Yesu alikuja kuanzisha ufalme wa kiroho kupitia mateso na kifo chake.

Kujenga Maisha juu ya upendo. Yesu alitumwa na Baba kujenga kanisa la Yesu Kristo. Lakini hakuweza kujenga ufalme wake kwa kumwaangamiza adui kwa upanga. Aliwashinda adui zake kwa njia ya kuteswa kwa ajili yao. Upendo ni kiini cha injili. Upendo ulimleta Yesu ulimwenguni kuwa Mwokozi wetu ((Yohana 3:16). Pia, upendo ni kiini cha maisha ya kikristo. Yesu aliwaambia wanafunzi kwamba, amri yake mpya ni upendo, na kwamba watu watawatambua kuwa ni wanafunzi wake, wakiwa na upendo wao kwa wao (Yohana 13:34-35).

Kubeba Msalaba. Yesu alisema mtu yeyote akitaka kumfuata lazima “ajitwike msalaba wake na amfuate” (Luka 9:23-24). Anayeamua kumfuata Yesu unajaa hamu ya kumfuata, na kujikana nafsi yake (yaani matamanio yake) na kuhiari kuambatana na Yesu hata kama italeta mateso.

Ufunuo Mpya. Siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwajilia wanafunzi (Matendo 2:1-4). Hii iliwapa uelewa mpya wa kwa nini Yesu alikuja duniani. Sasa, hawakutaka ukombozi wa kisiasa, badala yake, walizungumzia habari njema za injili alizoleta Yesu. Roho Mtakatifu aliwawezesha waumini kuishi maisha ya ushindi, dhidi ya dhambi, na kuwa na mahusiano na Mungu.

Yesu Mfano Wetu. Sisi, kama wanafunzi wa Yesu, tunaitwa kuteseka, kama Yesu alivyoteseka. Hata hivyo, tunaahidiwa uzima na nyumba ya milele mbinguni, wakati maisha ya hapa duniani yakikoma (1 Petro 4:13; Wafilipi 3:10-11). Mateso ya hapa na utukufu wetu ujao vinaenda pamoja katika maisha ya mwanafunzi. Kwa uhakika, ni matumaini ya utukufu ujao yatuwezeshayo kustahimili mateso yoyote ya sasa yanayotujia. Hatuahidiwi maisha bila matatizo pale tunapochagua kuwa mwanafunzi.

Kujitwika Misalaba Yetu. Yesu alisema mtu yeyote akitaka kumfuata, lazima “ajitwike msalaba wake na amfuate” (Luke 9:23-24). Mafundisho kuhusu kubeba msalaba na kumfuata Yesu ni ya kimsingi katika imani ya Waanabatisti. Maandiko yote ya Waanabatisti wa awali yanakaza fundisho hilo. Yesu akaonya wanafunzi wake kwamba, “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi” (Yohana 15:18). Waliona mateso kama kawaida katika kumfuata Yesu. Paulo na Barnaba

Page 19: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

19

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

walionya waamini katika makanisa mapya kwamba wategemee kupata mateso (Matendo 14:22). Waanabatisti wa karne ya 16 waliokufa kwa ajili ya imani yao walizidi watu 5,000.

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Eleza maana ya “Uanafunzi”

2. Kwa jinsi gani tunaweza kuwa wanafunzi wa Yesu?

3. Je! Unafikiri tunaweza kuwa wanafunzi wa kweli wa Yesu endapo hatutateseka kama alivyoteseka?

4. Uliposoma somo hili pamoja na vifungu vya biblia, je! Roho Mtakatifu alikuonyesha sehemu maishani mwako ambako unaweza kuwa mwanafunzi bora wa Yesu?

Page 20: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

20

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Sura ya 10: Imani ya Wamennonite Duniani

Yafuatayo yalikubalika katika mkutano wa Mennonite World Conference (Ushirika wa Wamennonite Duniani), kuwa ni imani inayounganisha Wamennonite wote duniani .

Imani tunayoshiriki. Kwa neema ya Mungu, tunatafuta kuishi na kutangaza habari njema za mapatano katika Yesu Kristo. Kama sehemu ya mwili wa Kristo, wakati wote na mahali pote tunayashika yafuatayo kuwa kitovu cha imani na mazoea yetu:

1. Mungu anajulikana kwetu kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Muumbaji anayetafuta kurejesha ubinadamu kutoka hali ya kuanguka, kwa kuwaita watu kuwa waaminifu katika ushirika, ibada, huduma, na ushahidi.

2. Yesu ni Mwana wa Mungu. Kupitia maisha na mafunzo yake, msalaba na ufufuo wake, alituonyesha jinsi ya kuwa wanafunzi waaminifu, aliukomboa ulimwengu, na kutupatia uzima wa milele.

3. Kanisa ni jamii ya wale ambao kwa uwezo wa Roho wa Mungu wameacha dhambi, wamekubali kwamba Yesu Kristo ni Bwana, wamebatizwa juu ya ungamo la imani yao, na wanamfuata Kristo katika maisha yao.

4. Tunakubali Biblia kuwa na mamlaka kwa imani na maisha yetu. Tunaifafanua Biblia kwa kushauriana tukiongozwa na Roho Mtakitifu na katika nuru ya Yesu Kristo ili tujue mapenzi ya Mungu na kumtii.

5. Roho wa Yesu anatuwezesha kuamini Mungu katika nyanja zote za maisha na hivyo kuwaleta amani ambao hukataa vurugu, na kuwapenda adui zetu, na kutafuta haki kwa watu wote, na kushirikisha mali zetu kwa wengine wenye mahitaji.

6. Tunakutana mara kwa mara kuabudu, kusherehekea Meza ya Bwana, na kusikia Neno la Mungu, na kusaidiana kutii.

7. Kama ushirika wa watu wa imani duniani, tunavuka mipaka ya taifa, kabila, lugha, na hali ya maisha. Tunataka kuishi katika ulimwengu bila kukubaliana na nguvu za uovu, tunashuhudia neema ya Mungu kwa kuwahudumia wengine, tukitunza uumbaji na kukaribisha watu wote kumjua Yesu Kristo kuwa Mwokozi na Bwana.

Imani hiyo yetu inatiwa nguvu kutoka kwa imani ya Wanabaptisti wa karne ya 16, waliokuwa mfano wa kumfuata Yesu Kristo. Tunataka kutembea katika jina lake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, hali tukingojea kurudi kwake Yesu na kutimizwa kwa Ufalme wa Mungu.

Yamekubaliwa na Baraza la Utendaji, Ushirika wa Wamennonite Duniani (Mennonite World Conference), 15 Machi, 2006

Maswali ya kuchunguza na majadiliano

1. Je! Unakubaliana na vifungu hivyo vya imani? Kipi ungependa kujadili zaidi?

2. Je! Kuna neno au fundisho lo lote zaidi ambalo ni muhimu kusaidia kanisa la Afrika kuwa na uaminifu zaidi kwa Injili?

3. Kwa njia zipi unaweza kushirikisha tawi lako itikadi(imani) hizi kwa kuwasaidia kuwa waumini waaminifu?

Page 21: Imani ya Wamennonite - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level1/Imani-ya-Wamennonite.pdf · dhambi za watu wote, na akashinda nguvu za dhambi na Shetani, kuppitia ufufuo

21

Imani ya Wamennonite

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

Mikazo Kuu katika Imani ya Wamennonite:

(Iliyowatenganisha na makanisa mengine katika karne ya 16)

1. Biblia inamshuhudia Yesu, ambaye ni msingi wa imani na maisha yetu. Yohana 5:39

2. Maisha ya kikristo ni kumfuata Yesu. Marko 8:34

3. Sheria ya Kristo ni upendo.

Kupendana. Yohana 13:34-35

Kupenda maadui. Mathayo 5:44

Kupenda watu wote. Yohana 3:16

4. Wakristo ni watu wa amani. Warumi 12:8; 1 Wakorintho 7:15

5. Kanisa ni ushirikiano wa waaminio. Matendo 2:42-47

6. Matendo ya ibada ya kanisa ni ishara na ukumbusho wa kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini.

Ubatizo wa kweli ni kusafishwa na kupewa uzima wa kiroho. Ubatizo kwa maji ni ishara ya ubatizo huo. 1 Petro 3:21

Mesa ya Bwana ni ukumbusho wa kifo chake Yesu. Luka 22:19

7. Waamini wote watumwa katika kazi ya injili. Mathayo 28:18-20; Yohana 20:21

8. Uongozi ni utumishi. Marko 10:43-45

9. Maisha ya kikristo huleta mateso. 2 Wakorintho 1:5; Wafilipi 3:10

10. Kutenganisha kanisa na serikali. Mamlaka ya serikali inatoka kwa Mungu, lakini msingi na makusudi yake ni tofauti na kanisa; mwanafunzi wa Yesu hutii Mungu kuliko mamlako zote. Matendo 5:29

Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 1 Wakorintho 3:11