26
1 EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA KONDE DIOCESE MBEYA WESTEN DISTRICT FOREST PARISH P.O.BOX 894 MBEYA – TANZANIA. Tel. +255252504304.Mob. 0784 315 945. Email:[email protected] TAARIFA YA KAZI YA MCHUNGAJI KWA MWAKA 2015 (JANUARI – DESEMBA). 1.0. UTANGULIZI:- “Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-Ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia”. 1Sam. 7:12. Wapendwa Watumishi wenzangu, Wapendwa Viongozi wa Vitengo, Wapendwa Wajumbe wa Halmashauri ya Usharika na Wapendwa Wakristo wenzangu wote. Mwanzo wa yote nawiwa kumshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kuuona mwaka huu mpya wa 2016. Tunayo sababu ya kuungana na mtunzi wa Zaburi ya 92: 1-2 akisema “Ni neno jema kumshukuru BWANA na kuliimbia jina lako Ee uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku”. Aidha, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiandaa taarifa hii ikiwa ni matokeo ya kazi kubwa ambayo Mungu ametupa neema ya kuifanya kwa mwaka wote uliopita wa 2015. Nawashukuru wote kwa utumishi wenu mbele ya Mungu wetu. 2.0. UONGOZI WA USHARIKA. Usharika unaongozwa na Mchg. Felix Mbogela akisaidiwa na Mtheol. Ambonisye Kajange (Mwanafunzi wa Uchungaji aliye mazoezini), Mwinj. Anyitike Mwasakujonga, Mwinj. Aminiel Lazaro, Bi. Ndigwako Gerson Mwakyulu ambaye ni Katibu Mtunza Hazina na Bi. Joyce Magoba ambaye ni Parish Worker. 3.0. TAKWIMU ZA WAKRISTO. Usharika una jumla ya Wakristo 1799 (Me 694, Ke 1105). Kati ya hao Wakristo watu wazima ni 1244 (Me. 467, Ke. 777), na Wakristo watoto ni 526 (Wav.216, Was. 310). Aidha, waliobatizwa mwaka 2015 ni 67 (Me. 21, Ke. 46). Kati ya hao watu wazima ni 6 (Me. 1, Ke. 5) na watoto ni 61 (Wav. 20, Was. 41). Waliorudi kundini pamoja na waliojiunga na dhehebu letu ni 30 (Me. 9, Ke. 21). Wanafunzi wa Kipaimara waliobarikiwa walikuwa 41 (Wav.14 Was. 27). Walioshiriki Meza ya Bwana walikuwa 2041 (Me. 824, Ke. 1217). Wakristo waliohama ni 50 (Me. 24, Ke. 26) na waliohamia ni 78 (Me. 29, Ke. 49). Aidha, ndoa zilizofungwa ni 12 na ndoa 1 ilibarikiwa.

EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

  • Upload
    others

  • View
    44

  • Download
    0

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

1

EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA KONDE DIOCESE

MBEYA WESTEN DISTRICT FOREST PARISH

P.O.BOX 894 MBEYA – TANZANIA. Tel. +255252504304.Mob. 0784 315 945. Email:[email protected]

TAARIFA YA KAZI YA MCHUNGAJI KWA MWAKA 2015 (JANUARI – DESEMBA). 1.0. UTANGULIZI:-

“Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-Ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia”. 1Sam. 7:12.

Wapendwa Watumishi wenzangu, Wapendwa Viongozi wa Vitengo, Wapendwa Wajumbe wa Halmashauri ya Usharika na Wapendwa Wakristo wenzangu wote. Mwanzo wa yote nawiwa kumshukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kuuona mwaka huu mpya wa 2016. Tunayo sababu ya kuungana na mtunzi wa Zaburi ya 92: 1-2 akisema “Ni neno jema kumshukuru BWANA na kuliimbia jina lako Ee uliye juu. Kuzitangaza rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku”. Aidha, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiandaa taarifa hii ikiwa ni matokeo ya kazi kubwa ambayo Mungu ametupa neema ya kuifanya kwa mwaka wote uliopita wa 2015. Nawashukuru wote kwa utumishi wenu mbele ya Mungu wetu.

2.0. UONGOZI WA USHARIKA. Usharika unaongozwa na Mchg. Felix Mbogela akisaidiwa na Mtheol. Ambonisye Kajange (Mwanafunzi wa Uchungaji aliye mazoezini), Mwinj. Anyitike Mwasakujonga, Mwinj. Aminiel Lazaro, Bi. Ndigwako Gerson Mwakyulu ambaye ni Katibu Mtunza Hazina na Bi. Joyce Magoba ambaye ni Parish Worker.

3.0. TAKWIMU ZA WAKRISTO. Usharika una jumla ya Wakristo 1799 (Me 694, Ke 1105). Kati ya hao Wakristo watu wazima ni 1244 (Me. 467, Ke. 777), na Wakristo watoto ni 526 (Wav.216, Was. 310). Aidha, waliobatizwa mwaka 2015 ni 67 (Me. 21, Ke. 46). Kati ya hao watu wazima ni 6 (Me. 1, Ke. 5) na watoto ni 61 (Wav. 20, Was. 41). Waliorudi kundini pamoja na waliojiunga na dhehebu letu ni 30 (Me. 9, Ke. 21). Wanafunzi wa Kipaimara waliobarikiwa walikuwa 41 (Wav.14 Was. 27). Walioshiriki Meza ya Bwana walikuwa 2041 (Me. 824, Ke. 1217). Wakristo waliohama ni 50 (Me. 24, Ke. 26) na waliohamia ni 78 (Me. 29, Ke. 49). Aidha, ndoa zilizofungwa ni 12 na ndoa 1 ilibarikiwa.

Page 2: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

2

4.0. TANZIA. Ninasikitika kuwajulisha kuwa mwaka uliopita wa 2015, Wakristo wenzetu nane walifariki dunia. Kati ya hao wanaume ni wawili na wanawake ni sita. Naomba niwatambue kwa majina watumishi wa Mungu hawa waliotutangulia. Nao ni hawa wafuatao:- 1. Tusajigwe Kyonya kutoka Kijiji cha Ilala aliyefariki tarehe 30/01/2015. 2. Aneth Kasape kutoka Kijiji cha Meta aliyefariki tarehe 11/02/2015. 3. Joyce Masorini kutoka Kijiji cha Usalama aliyefariki tarehe 08/02/2015. 4. Godwin Mwakatobe kutoka Kijiji cha Maanga aliyefariki tarehe 16/07/2015. 5. Mrs. Mwakyoma kutoka Kijiji cha Meta aliyefariki tarehe 05/11/2015. 6. Rahabu Fungo kutoka Kijiji cha Maanga aliyefariki tarehe 07/11/2015. 7. Elia Mwafyela kutoka Kijiji cha Maanga aliyefariki tarehe 11/11/2015. 8. Lupakisyo Mbapa kutoka Kijiji cha Sinde aliyefariki tarehe 19/11/2015.

Yesu Kristo anasema “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi,

ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hata kufa kabisa hata milele. Je unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni”. Yohana 11: 25-27.

Naomba tusimame na tumwombe Mungu afanyike faraja kwa familia za wapendwa hawa na Kanisa kwa ujumla.

5.0. VITENGO VYA USHARIKA.

Usharika una Vitengo Vinne. Vitengo hivyo ni Wanawake na Watoto, Malezi ya Vijana, Muziki na Elimu ya Kikristo. Usharika pia una huduma ya MOMs na Faragha ya Usharika. Aidha, Usharika una kwaya tano nazo ni Uinjilisti, Kwaya Kuu, Hosiana, Vijana na Safina.

6.0. MITAA NA VIJIJI VYA USHARIKA. Usharika una Mitaa miwili na Vijiji kumi na mbili. Mitaa na Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo:- 6.1. Mtaa wa Sinde una Vijiji vitano vya Sinde, Ilolo, Ilala, Ilamba na Maanga. 6.2. Mtaa wa Forest una Vijiji saba, navyo ni Forest, Forest Mpya, Meta, Usalama,

Magereza, Mzumbe na TIA.

Usharika uko katika mpango wa kuanzisha Kijiji kingine cha SAUT. Kijiji hiki kitajumuisha wanafunzi wanaosoma katika Chuo Kikuu cha SAUT tawi la hapa Mbeya kama ilivyo kwa vyuo vya Mzumbe na TIA.

Aidha, Usharika unalea na kutunza Mtaa wa misioni wa Mjele. Mtaa huu unongozwa na Mwinj. Paulina Simchimba Mwaipungu.

Page 3: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

3

7.0. HUDUMA ZA KIROHO. Mwaka ulipita wa 2015 umekuwa wa baraka sana katika Usharika wetu. Pamoja na huduma mbalimbali za kiroho zilizofanyika, tumepata pia neema ya kufanya semina zipatazo kumi za Neno la Mungu kama ifuatavyo hapa chini:-

- Semina juu ya Missioni iliyoendeshwa na Baba Askofu Dkt. Israel-Peter Mwakyolile tarehe 21/03/2015.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika tarehe 26/04-03/05/2015, iliyoendeshwa na Mchg. Adam Hajj kutoka Nairobi.

- Semina kwa wanandoa (Faragha ya wanandoa) iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa Wanawake na Watoto wa Dayosisi Bi. Alice Mtui tarehe 16-19/07/2015.

- Semina ya Vijana katika juma la sikukuu ya Vijana iliyofanyika tarehe 23-26/07/2015, iliyoendeshwa na Ndg. Mujuni Kyaruzi akisaidiana na na Ndg. Martin Mwankenja.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika tarehe 08-09/08/2015, iliyoendeshwa na Mchg. Zakayo Malekwa akisaidiana na Ndg. Nuhu Mkirumi kutoka Arusha.

- Semina kuhusu sheria na haki za Wanawake na Watoto iliyofanyika kuelekea sikukuu ya Wanawake tarehe 04-06/09/2015, iliyoongozwa na Mchg. Ikupilika Mwakisimba ambaye ni Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Konde.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika tarehe 10-13/09/2015, iliyoendeshwa na Mwinj. John Athuman kutoka Manyara.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika tarehe 04-08/11/2015, iliyondeshwa na Mchg. Jacob Mwakatobe.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika tarehe 22-29/11/2015, iliyoendeshwa na Mchg. Adam Hajj kutoka Nairobi.

- Semina ya Neno la Mungu iliyofanyika katika juma la Krismasi tarehe 20-27/12/2015, iliyoendeshwa na Mwinj. Danstan Mtoi kutoka Dar es Salaam.

Aidha, huduma nyingine za kiroho zilizofanyika ni kama hizi zifuatazo:-

Tumeshiriki kwa kuwawezesha vijana wetu wa University Students Christian

Fellowship (USCF) wa Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya katika Outreach Programe yao iliyofanyika tarehe 15-22/02/2015 katika kijiji cha Mavanga kilichopo Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe.

Nimefanya Ibada ya pamoja na Watoto wa shule ya jumapili na kutoa mafundisho kwao tarehe 08/03/2015.

Tumefanya Ibada ya kuwasimika kazini Viongozi wa Idara ya Wanawake na Watoto na Idara ya Muziki tarehe 22/03/2015.

Tumefanya Ibada ya kuwasimika kazini Wazee wapya wa vijiji vya Mzumbe na T.I.A na kuwaaga waliomaliza kipindi chao tarere 24/05/2015.

Tumeshiriki kwa kuwezesha kambi ya vijana iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Umoja wa kujisomea Biblia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mwinj. Bryceson Mwakisembeja tarehe 10-14/06/2015.

Page 4: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

4

Tumefanya Ibada ya kukumbuka miaka 37 tangu Ulutheri uingie katika Jiji la Mbeya iliyoongozwa na Mchg. Mmenye Mwasampeta ambaye ndiye muasisi wa Ulutheri hapa jijini tarehe 09/08/2015.

Tumefanya Ibada ya kumsimika kazini Katibu Mtunza Hazina wa Usharika na Parish Worker tarehe 13/09/2015.

Tumeshiriki Ibada zote za Kijimbo zilizopangwa pamoja na vikao vyote vya Kijimbo na Kidayoasisi vilivyohitaji ushiriki wetu.

Tumefanya Ibada ya kuwabariki wanafunzi wa Kipaimara tarehe 05/12/2015. Kwa kushirikiana na wenzetu wa Usharika wa Bethania, tumefanikiwa kujenga

nyumba ya mtumishi katika Mtaa wetu wa Missioni wa Mjele. Tumefanya Ibada za maombi maalum kwa makundi mbalimbali katika Ibada za kila

mwisho wa mwezi. Tumefanya mikesha miwili ya maombi. Mmoja ulikuwa maalumu kwa ajili ya

kuombea uchaguzi Mkuu wa nchi na ule wa Mkuu wa Kanisa. Aidha, mwingine ulikuwa kwa ajili ya kuuaga mwaka 2015 na kuupokea mwaka mpya wa 2016 uliofanyika tarehe 31/12/2015.

8.0. WAGENI WALIOFIKA USHARIKANI KWA MWAKA 2015. Mwaka uliopita wa 2015, Mungu ametupa neema ya kuwapokea wageni kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kwaya zipatazo sita kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Dayosisi yetu. Wageni waliofika ni wengi sana, lakini kwa niaba ya wote naomba niwatambue hawa wafuatao hapa chini:-

Tumempokea Ndg. Ambokile Mwasomola kutoka Usharika wa Sinai aliyefika kwa huduma ya mafundisho na maombi katika Ibada 11/01/2015.

Kupitia kwaya ya Hosiana, tumepokea ugeni wa kwaya ya Betheli kutoka Usharika wa Njisi-Boder tarehe 18/01/2015.

Tumempokea NKM-FMM wa KKKT-Dayosisi ya Konde Mchg. Edward Meshack Njinga aliyefika kwa huduma ya Neno na Maombi tarehe 25/01/2015.

Tumempokea Ndg. Gary Lewis kutoka New Orleans, Louisiana huko Marekani na mwenyeji wake Mwl. Humphrey Kabalika. Waliofika kuelezea umuhimu wa huduma ya The Gideons Iternational katika shule, vyuo na magereza.

Tumempokea Mchg. Ruth Kabibi Mwalwega aliyefika kwa huduma ya Neno na Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015.

Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana Jimbo la Mbeya Magharibi, waliofika kwa lengo la kukutana na Vijana wa Usharika tarehe 01/02/2015.

Tumempokea Mchg. Nsokigwe Mwalusamba wa Usharika wa Uyole pamoja na ujumbe wa watu nane alioongozana nao kwa ajili ya kujifunza namna tunavyoendesha kazi ya ujenzi wa Kanisa tarehe 01/02/2015.

Tumempokea Bi. Alice Henry Mtui ambaye ni NKM-HJMK na Mkurugenzi wa Wanawake na Watoto wa Dayosisi, aliyefika kwa mafundisho tarehe 08/02/2015.

Page 5: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

5

Aidha alifika tena kwa huduma ya Neno katika Ibada ya Ijumaa Kuu tarehe 03/04/2015 na kwa mafundisho katika faragha ya wanandoa tarehe 16-19/07/2015.

Tumepokea wanafunzi wa UKWATA kutoka sekondari ya Kidugala waliofika kwa huduma ya Uinjilisti tarehe 07-08/02/2015.

Kupitia kwaya ya Uinjilisti, tumepokea ugeni wa kwaya ya Shangilieni kutoka Kanisa la Anglikana Arusha wakiongozwa na Rev. Fr. Martin Kadama pamoja na mwenyeji wao Rev. Fr. Abraham Ponera ambaye ni kiongozi wa Vijana wa Kanisa la Anglikana hapa Mbeya, waliofika kushiriki Ibada na tamasha la miaka nane ya kuanzishwa kwa kwaya yetu ya Uinjilisti tarehe 15/02/2015.

Tumempokea Dkt. Stanley Chattanda aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka nane ya kuanzishwa kwa kwaya ya Uinjilisti.

Tumempokea Mzee Issa Simon kutoka Kandete aliyefika kwa huduma ya Neno katika Ibada ya tarehe 22/02/2015.

Tumempokea Mchg. Erasto Mwaipopo (marehemu sasa) aliyefika kwa huduma ya Neno na Maombi katika Ibada ya tarehe 01/03/2015.

Tumempokea Mchg. Elisha Mwasakifwa aliyefika kwa mafundisho ya matoleo kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na kuzindua mpango wa pili wa ujenzi kwa njia ya kadi maalumu katika Ibada ya tarehe 15/03/2015. Aidha alifika tena kwa huduma ya Sakramenti ya Meza ya Bwana Alhamisi ya tarere 02/04/2015 na katika Ibada ya Pasaka kwa huduma ya Neno tarehe 05/04/2015.

Tumempokea Mchg. Njekwingila Mwasyoge aliyefika kwa huduma ya Ubatizo katika Ibada ya Jumatatu ya Pasaka tarehe 06/04/2015. Aidha alifika tena kwa kazi ya Elimu ya Kikristo Usharikani tarehe 06/06/2015.

Tumempokea Baba Askofu Dkt. Israel-Peter Mwakyolile aliyefika kutoa mafundisho juu ya Missioni tarehe 21/03/2015. Aidha alifika tena pamoja na wageni kutoka Ujerumani waliotembelea Usharika wetu tarehe 11/11/2015.

Tumempokea Mkurugenzi wa Malezi ya Vijana wa KKKT-Dayosisi ya Konde Mchg. Lusajano Sanga aliyefika kwa huduma ya Neno na Maombi katika Ibada ya tarehe 19/04/2015. Aidha alifika tena kwa huduma ya Neno na Maombi kwenye Ibada ya Sikukuu ya Usharika tarehe 28/06/2015 na kwa huduma ya Neno na Sakramenti ya Meza ya Bwana katika Ibada ya tarehe 23/08/2015.

Tumempokea Mchg. Adam Hajj kutoka Nairobi aliyeongozana na Mchg. Godlisten Nkya wa Usharika wa Ubungo waliofika kwenye semina ya Neno la Mungu ya tarehe 26/04-03/05/2015. Aidha alifika tena kwa semina nyingine tarehe 22-29/11/2015.

Tumempokea Ndg. Aminiel Issa aliyefika kwa huduma ya Neno tarehe 22/11/2015. Tumempokea Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Rosemary Staki Senyamule aliyefika

kwenye Ibada na Semina ya Neno la Mungu tarehe 03/05/2015. Tumempokea Baba Askofu Msataafu Shadrack Manyiewa kutoka Makete aliyefika

kwenye Ibada ya shukrani ya pekee kwa mjukuu wake tarehe 10/05/2015. Tumempokea Mwl. Furaha Mwaikeke aliyefika kwa huduma ya Neno katika Ibada ya

tarehe 10/05/2015.

Page 6: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

6

Tumempokea Mkuu wa Jimbo Mchg. Andindilile Mwakibutu pamoja na Wachungaji wa Jimbo la Mbeya Magharibi waliofika kwenye kikao chao cha Wachungaji tarehe 19/05/2015. Aidha alifika tena kufungua na kufunga semina ya tarehe 26/04-03/05/2015 na ile ya tarehe 22/-29/11/2015. Alishiriki na kuhudumu Neno katika Ibada ya tarehe 18/10/2015 ya kuombea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015.

Tumempokea Baba Askofu Dkt. Joseph P. Bvumbwe wa Kanisa la Kiijili la Kilutheri Malawi (KKKM) pamoja na ujumbe wa watu sita waliofika tarehe 30/05/2015.

Tumempokea Mchg. Samson Mwakisu kutoka Chuo cha Biblia Matema aliyefika kwa huduma ya Neno na Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 24/05/2015.

Tumempokea Mchg. Mariam Kyomo Numbi aliyefika kwa huduma ya Neno na Maombi katika Ibada ya tarehe 31/05/2015.

Tumempokea Baba Askofu James Almasi aliyefika kwa huduma ya kufungisha ndoa ya Mwinj. Bryceson Mwakisembeja na Rhoida Kalinga tarehe 07/07/2015.

Tumempokea Mchg. Amos Sanga wa Usharika wa Songwe Viwandani aliyefika kwa huduma ya Neno katika Ibada ya tarehe 12/07/2015.

Kupitia kwaya ya Uinjilisti, tumepokea Kwaya kutoka Kanisa la Sabato-Mabatini, waliotembelea Usharika wetu na kushiriki Ibada tarehe 12/07/2015.

Tumempokea Mchg. Benjamin Mwaisumo wa Usharika wa Manow akiongoza kwaya ya Vijana ya Usharika huo waliofika Usharikani kwetu tarehe 01-02/08/2015.

Tumempokea Mchg. Zakayo Malekwa aliyeongozana na Ndg. Nuhu Mkirumi kutoka Arusha waliofika kwa huduma ya Semina ya Neno la Mungu tarehe 08-09/08/2015.

Tumempokea Mchg. Lugano Mwakasege aliyefika kuhamasisha sikukuu ya Jimbo kwenye Ibada ya tarehe 16/08/2015.

Tumempokea Mtheol. Ambonisye Kajange aliyepangwa na Dayosisi kufanya mazoezi yake ya Uchungaji hapa Usharikani tarehe 02/09/2015.

Tumempokea Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Konde Mchg. Ikupilika Mwakisimba aliyefika kwenye semina iliyohusu sheria na haki za Wanawake na Watoto wakati wa sikukuu ya Wanawake tarehe 04-06/09/2015. Aidha alifika tena kwa huduma ya ubarikio wa Kipaimara tarehe 05/12/2015.

Tumempokea Mchg. Ambakisye Lusekelo wa Usharika wa Temboni wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani akiongoza Kwaya Kuu ya Usharika wake waliotembelea Usharika wetu tarehe 11-13/09/2015.

Tumempokea Mwinj. John Athuman kutoka Manyara aliyefika kwa huduma ya semina ya Neno la Mungu tarehe 10-13/09/2015.

Tumempokea Mchg. Jacob Mwakatobe aliyefika kwa huduma ya Neno na Sakramenti ya Meza ya Bwana katika Ibada ya tarehe 01/11/2015. Aidha alifika tena kwa huduma ya semina ya Neno la Mungu tarehe 04-08/11/2015.

Tumempokea Msaidizi wa Askofu Dean Geoffrey Mwakihaba aliyefika kufungisha ndoa ya Ndg. Joshua Mwasandube na Furahini Willium tarehe 07/11/2015.

Tumepokea kwaya ya Mwimbieni Bwana kutoka Usharika wa Engarenarok wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati kule Arusha tarehe 08-11/10/2015.

Page 7: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

7

Tumempokea Ndg. Danstan Mtoi kutoka Dar es salaam aliyefika kwa huduma ya semina ya Neno la Mungu katika juma la Krismasi tarehe 20-27/12/2015. Neno la Mungu katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati linasema “Basi,

mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri”. Kumb. 10:19.

9.0. HALI YA MATOLEO (SADAKA) YA USHARIKA KWA MWAKA 2015. Matoleo ninayoyaelezea hapa ni yale ya rasilimali tu, yaani yale yanayohusika na makato ya %. Matoleo hayo ni Ulezi, Ahadi, Shukrani, Shukrani ya Pekee, Zaka, Mavuno, Sikukuu ya Usharika, Pasaka na Krismasi. Tunamshukuru Mungu kwani hali ya utoaji kwa mwaka 2015 imeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2014. Mwaka huu wa 2015 kuna ongezeko la Tsh. 13,088,050= ambalo ni sawa na 13.8%.

Hapa chini ni taarifa ya matoleo hayo kwa miaka miwili ya 2014 na 2015.

NA MAELEZO 2014 2015 TOFAUTI ONG/PUNG % 01 ULEZI 856,500= 954,600= 98,100= ONGEZEKO 10.2

02 AHADI 18,562,350= 23,503,400= 4,941,050= ONGEZEKO 21.0

03 SHUKRANI 11,362,300= 12,868,700= 1,506,400= ONGEZEKO 11.7 04 S/PEKEE 6,434,100= 10,194,900= 3,760,800= ONGEZEKO 36.8

05 ZAKA 14,237,300= 17,172,500= 2,935,200= ONGEZEKO 17.0 06 MAVUNO 7,983,150= 8,227,250= 244,100= ONGEZEKO 2.9

07 S/USHARIKA 4,025,650= 3,810,850= 214,800= PUNGUFU 5.6 08 PASAKA 6,198,300= 6,374,400= 176,100= ONGEZEKO 2.7

09 KRISMASI 12,036,450= 11,677,550= 358,900= PUNGUFU 3.07

10 JUMLA 81,696,100= 94,784,150= 13,088,050= ONGEZEKO 13.8

Taarifa kamili ya mapato na matumizi ya Usharika kwa mwaka 2015 imeandaliwa na Katibu Mtunza Hazina.

Napenda kutumia fursa hii kuishukuru Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya

Usharika iliyo chini ya Uongozi wa Ndg. Given Ngajilo ambaye ni Mwenyekiti na Ndg. Erick Sichinga ambaye ni Katibu, kwa kazi yao kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha kuwa hali ya usalama wa Hazina yetu inakuwa nzuri wakati wote. Ukweli natiwa moyo sana na utumishi wa watumishi wa Mungu hawa sanjari na moyo wao wa upendo, upole na huruma kwa Watumishi na kwa Usharika wao kwa ujumla.

Aidha, kipekee namshukuru sana Katibu Mtunza Hazina wa Usharika Bi. Ndigwako Gerson Mwakyulu kwa utumishi wake mahiri katika kutunza Hazina ya Usharika na uandikaji mzuri wa vitabu vya fedha. Namshukuru kwa moyo wake aliojaliwa wa kujituma, bidii, upendo na huruma. Aidha, namshukuru kwa ushirikiano na ushauri

Page 8: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

8

mzuri anaonipa wakati wote, hakika amefanyika baraka katika huduma yangu. Natambua ugumu na uzito wa kazi aliyokabidhiwa, hata hivyo ajue kuwa Mungu ndiye aliyemwita na kumuweka katika huduma hii, hivyo amtazame yeye naye atakuwa pamoja naye wakati wote.

Nawashukuru wajumbe wa kamati ya kuhesabu sadaka kwa kazi yao kubwa na nzito wanayoifanya kila Jumapili. Watumishi hawa wanafanya kazi hii kwa moyo wa kupenda pasipo kuchoka wala manung’uniko. Mungu awabariki sana.

Kwa namna ya pekee, ninamshukuru Mzee Dreck Mwakipesile kwa huduma yake kubwa anayoifanya ya kuandaa bahasha na kutoa taarifa kila mwaka juu ya utumiaji wa bahasha. Ukweli kazi anayoifanya ni kubwa na nzito. Namshukuru kwa kujitoa kwake na kujituma kwa bidii kwa kazi hii. Sina lugha itoshayo zaidi ya kusema Mungu ambariki sana.

Namshukuru Parish Worker wetu Bi. Joyce Magoba. Ni ukweli usiopingika kwamba

pamoja na kazi nyingi alizonazo za kutunza Ofisi na mambo mengine ya kiibada, lakini pia anafanya kazi kubwa na nzito ya kuhakikisha kila bahasha ya Mkristo inakaa mahali pake na anaipata kirahisi. Mungu ambariki kwa utumishi wake.

Aidha, ninatambua changamoto inayojitokeza mara kwa mara ya upotevu na uchanganywaji wa bahasha za sadaka hali inayopelekea usumbufu kwa baadhi ya Wakristo. Jambo hili tunalifanyia kazi mwaka huu wa 2016 ili kupunguza kama sio kuuondoa kabisa usumbufu huu.

10.0. MIRADI. Usharika unaendesha na kusimamia miradi kadhaa ya uchumi na ya ujenzi. Hapa chini

ni orodha ya miradi hiyo:- 10.1. Miradi ya Uchumi.

Nyumba ya kukodisha (Mbeya records studio). Nyumba hii inakodishwa kwa Tsh. 60,000= Hivyo kwa mwaka tunapata jumla ya Tsh. 720,000=.

Shule ya Awali (wamekodi jengo). Mmiliki wa shule hii analipia Tsh. 20,000= kwa mwezi. Hivyo kwa mwaka ni Tsh. 240,000=.

Viti vya kukodisha.

Viti hivi ni vya plastiki, hadi sasa vimebakia 196 baada ya 54 kuvunjika. Viti hivi vinakodishwa kwa Tsh. 300= kwa kila kimoja. Kwa mwaka 2015, mradi huu umeingiza jumla ya Tsh. 119,500=.

Page 9: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

9

10.2. Mradi wa Ujenzi. Kutokana na ongezeko kubwa la waumini, Usharika uliamua kujenga Kanisa kubwa ili kukidhi hitaji hilo. Jengo hilo la Ibada linajumisha Ofisi mbalimbali, ukumbi wa mikutano na vitega uchumi vingine. Tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha katika hatua hii tunayoiona sasa. Jengo hili linajengwa kwa nguvu zetu wenyewe bila msaada wowote kutoka marafiki wa nje ya nchi. Tunamshukuru Mungu aliyeweka nia hii ya utumishi ndani yetu. Nafurahi kuwafahamisha kwamba mpaka hatua hii tuliyofikia hatudaiwi fedha yoyote wala kifaa chochote. Kwa mwaka huu wa 2015, sadaka ya Ujenzi imeonekana kupungua kidogo ukilinganisha na mwaka 2014. Upungufu huo ni wa Tsh. 15,245,050= ambao ni sawa na 15.2%. Hapa chini ni taarifa ya matoleo hayo ya ujenzi kwa miaka miwili ya 2014 na 2015.

NA MAELEZO 2014 2015 TOFAUTI ONG/PUNG % 01 BAHASHA 7,920,600= 7,540,700= 379,900= PUNGUFU 5.0

02 MICHANGO 107,345,050= 92,479,900= 14,865,150= PUNGUFU 16.0

03 JUMLA 115,265,650= 100,020,600= 15,245,050= PUNGUFU 15.2

Natumia nafasi hii kuishukuru Kamati ya Ujenzi chini ya uongozi wa Ndg. Habakuki Mushi ambaye ni Mwenyekiti akisaidiana na Eng. Patson Isote Mwakaje ambaye ni Katibu. Wao na wajumbe wenzao wanafanya kazi kwa juhudi kubwa na kwa weledi wa hali ya juu. Mungu wanayemtumikia awakumbuke kwa sadaka yao hii.

Aidha, nawashukuru kipekee wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo na Ujenzi chini ya uongozi wa Ndg. Given Ngajilo ambaye ni Makamu Mwenyekiti na Ndg. Mjuni Kyaruzi ambaye ni Katibu Mtunza Hazina wa Kamati. Kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa Mungu hawa inaonekana dhahili na inampa Mungu utukufu. Mungu wa mbinguni awabariki kwa utumishi wao huu.

Kipekee ninawashukuru wataalamu wetu Eng. Patson Isote Mwakaje, Eng. Alnod Kashula na Eng. Israel Mayage kwa kazi kubwa wanayoifanya. Mungu anaiona sadaka yao hii na aendelee kufanyika baraka kwao siku hata siku.

Nawashukuru mafundi wote kwa kazi yao nzuri ya kujenga Hekalu hili. Namwomba Mungu azidi kuwafunika kwa ulinzi wake mpaka mwisho wa kazi hii.

Nawashukuru Wakristo wenzangu mnaoendelea kujitoa kwa sadaka zenu, maombi na ushauri mbalimbali kwa kazi hii ya ujenzi wa Hekalu la BWANA. Nawasihi katika Jina la Yesu Kristo, tusichoke tuendelee kujitoa maana shughuli hii yatuhusu sisi sote.

Page 10: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

10

Katika kitabu cha Mwanzo 42:1, Mzee Yakobo aliwauliza wanawe akisema “Kwa nini

mnatazamana? Na katika kitabu cha Nahumu 1:9, Nabii Nahumu anauliza akisema “Mnawaza nini juu ya BWANA? Lakini ndipo katika kitabu cha Nabii Hagai 1:8, Mungu anasema “Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana”.

Naamini sisi sote katika umoja wetu hatutatazamana wala hatutawaza kwa kuchoka, kulegea, kukata tamaa, ama kuzimia moyo. Bali tutapanda milimani, tutaleta miti na tutaijenga nyumba hii ya Bwana mpaka ifikie utimilifu wake. Naye Mungu ataifurahia na atatukuzwa kwa kazi ya mikono yetu nasi tutabarikiwa na kufanikiwa katika yale tuyaombayo na “yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili”. (Nahumu 1:9).

11.0. MALI NYINGINE ZA USHARIKA. Usharika umejaliwa kuwa na mali nyingine kadhaa kama ifuatavyo:-

11.1. Gari aina ya Toyota Hilux T 495 ATB (Double Cerbin) linalotumiwa na

Mchungaji. 11.2. Gari aina ya Toyota Coaster T 209 BFA linalomilikiwa na Usharika kupitia Kwaya

ya Uinjilisti. 11.3. Gari aina ya Mitsubishi Canter T 205 DCE ambalo pia linamilikiwa na Usharika

kupitia Kwaya ya Uinjilisti. 11.4. Vyombo mbalimbali vya muziki vinavyomilikiwa na Usharika kupitia kwaya zake

za Hosiana, Safina, Kwaya Kuu, Vijana na Uinjilisti. 11.5. Viwanja viwili vilivyopo eneo la Itezi (vimepimwa na hati tunazo). 11.6. Viwanja viwili vilivyopo hapa Forest, ambapo kimoja kimejengwa Jengo la Ibada

na kingine kimejengwa nyumba ya Mtumishi (vimepimwa na hati tunazo). 11.7. Kiwanja kimoja kilichopo eneo la Ilolo (bado hakijapimwa).

12.0. UHUSIANO NA MARAFIKI WA NJE YA NCHI.

Mambo yote ya uhusiano na marafiki wetu wa nje ya Nchi yanaratibiwa na kamati yetu ya Uhusiano inayoongozwa na Mwl. Meleckzedek Nyagawa ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hii. Marafiki tunaohusiana nao ni wale wa Usharika wa Zion Lutheran Church, East Petersburg wa kule Marekani. Mwaka 2015, marafiki wetu hawa wametupatia msaada wa jumla ya Tsh. 1,694,950=.

Page 11: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

11

13.0. OFISI ZA IDARA ZA USHARIKA. 13.1. Idara ya Wanawake na Watoto.

Idara hii inaongozwa na Mrs. Rhoda Mgaya ambaye ni Katibu akisaidiana na Mrs. Suma Mwaisango ambaye ni Mwenyekiti. Katika utangulizi wake, Katibu anamshukuru Mungu kwa kumjalia uzima na afya na kumwezesha kuifanya kazi hii aliyomkabidhi kupitia Wanawake wa Forest na anasema “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. Filp. 4:13. Katika mwaka wa 2015, Idara imefanya haya yafuatayo:-

- Wameshiriki kongamano la Dayosisi lililofanyika katika Chuo cha MUST na walichangia kongamano hilo kiasi cha Tsh. 460,400=. Lakini baadhi ya waliotakiwa kuhudhuria hawakufika.

- Wameshiriki tamasha la Watoto katika Usharika wa Nzovwe. Watoto wetu walishika nafasi ya tano kwa ngonjera, uimbaji na somo la Biblia.

- Idara imefanikiwa kuwashonea watoto sare aina ya suti, ingawa sio wote. - Wananwake katika Usharika wamenunua sare aina ya Tshert zilizotengenezwa

na Idara ya Wanawake Kidayosisi. - Wameshiriki pamoja na Wanawake wenzao hapa Jijini Mbeya kwenye sikukuu

ya maombi iliyofanyika katika Usharika wa Betheli. - Wamempokea Katibu wa Wanawake na Watoto wa Dayosisi aliyetembelea

Usharika wetu. - Wameadhimisha sikukuu ya Wanawake mwezi Septemba 2015, maadhimisho

hayo yalikwenda sambamba na semina iliyohusu sheria ya ndoa na haki za Wanawake na Watoto iliyofanyika tarehe 4-6/9/2015.

- Wameadhimisha sikukuu ya Watoto kwa njia ya kuandaa chakula na kutoa zawadi kwa walimu wa Watoto.

- Wameendelea kuwa na Ibada za kila jumatano na baada ya Ibada wanakuwa na huduma ya kuombea mambo yaliyopo Usharikani na hata katika familia zao.

- Wamekuwa na mradi wa kuoka mikate ingawa sasa umesimamishwa kutokana na maendeleo yake kutokuwa mazuri.

- Mradi wa VICOBA umeendelea vizuri, tayari awamu ya kwanza imekamilika na wanachama wamegawana hisa zao na sasa wanaendelea na awamu nyingine.

Changamoto za Idara hii.

Wanawake katika Usharika wetu ni wengi sana, lakini wanaoshiriki kwenye ibada na hata kwenye semina zinazoandaliwa ni wachache sana. Katibu anawaomba wanawake wote katika Usharika kushirikiana pamoja katika kuujenga mwili wa Kristo.

Uhaba wa vyumba vya kufundishia watoto wetu. Idadi ya watoto wanaohudhuria mafundisho ni kubwa na wanajifunzia katika chumba kimoja tena kisicho na ubora. Aidha umri wao unatofautiana na wanachanganywa pamoja hali isiyoleta tija katika ufundishaji.

Page 12: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

12

Malengo ya Idara kwa mwaka 2016. - Kupitia michango itakayotolewa katika sikukuu ya maombi ya mwaka huu,

wamelenga kutoa huduma kwa yatima, wajane na wasiojiweza waliopo katika Usharika wetu. Aidha, watatoa huduma kwa shule ya watoto walemavu ya Katumba.

- Wamepanga kununua Television (TV) kwa ajili ya watoto wetu wa shule ya jumapili.

- Wanatarajia kununua bajaji kama mradi wa Idara, michango kwa ajili ya mradi huu ni kwa kila kijiji.

- Watoto watarekodi mkanda wao wa nyimbo na kuuingiza sokoni. - Maadhimisho ya sikukuu ya Watoto yataambatana na semina kwa walimu wao. - Wataanzisha mradi wa VICOBA na ni maalumu kwa ajili ya Wajane tu. Huu ni

mpango kutoka Dayosisi. - Watoto watashiriki tamasha lao Kijimbo linalotarajiwa kuwa mwezi Julai 2016.

13.2. Idara ya Malezi ya Vijana.

Idara hii inaongozwa na Ndg. Nelson Mbugi ambaye ni Katibu. Idara hii ndiyo yenye dhamana ya malezi kwa Vijana hapa Usharikani. Kwa kawaida wahusika na Idara hii ni Vijana wote walio chini ya miaka 45. Aidha, Katibu anawashukuru sana Washarika wote kwa ushirikiano waliounesha na kujitoa kwao kusaidia majukumu ya Idara hii. Kipekee anawashukuru walezi wa Idara ambao ni Ndg. Erick Sichinga, Patson Isote, Mwinj. Bryceson Mwakisembeja na Mr & Mrs Mujuni Kyaruzi kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuilea Idara hii. Kwa mwaka 2015, Idara imefanya yafuatayo hapa chini:-

- Wameshiriki vikao vyote vya Jimbo pamoja na kutoa michango yote waliyopangiwa.

- Wameshiriki ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Mtaa wa Missioni wa Mjele kwa kutoa mifuko kumi ya sementi.

Malengo ya Idara kwa mwaka 2016. Kwa mwaka 2016 kitengo kimelenga kufanya yafuatayo:-

- Katika sikukuu ya Vijana itakayofanyika tarehe 30/07/2016, wameazimia kuwa na juma la Vijana litakaloambatana na semina kwa Vijana na watakuwa pia na wageni kutoka Hananasifu kule Dar es Salaam.

- Wamepanga kutembelea Usharika wa Kihesa kule Iringa mwezi Novemba 2016. - Aidha wamepanga pia kuwatembelea wafungwa magerezani.

Page 13: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

13

Kwaya ya Vijana. Kwaya hii inaongozwa na Ndg. Gwamaka Joshua ambaye ni Katibu akisaidiana na Ndg. Frank Philip ambaye ni Mwenyekiti.

Malengo ya Kwaya kwa mwaka 2016.

- Kwaya ina mpango wa kuzindua “audio album” tarehe 20/03/2016. - Kufungua akauti benki kwa ajili ya kutunza fedha za Kwaya. - Kuwa na sikukuu ya kutimiza miaka nane tangu kuanzishwa kwake. Sikukuu

hiyo itafanyika tarehe 31/01/2016 na itaambatana na tamasha la uimbaji. - Katika sikukuu ya Vijana, Kwaya inategemea kualika Kwaya kati ya hizi

zifuatazo:-

Kwaya ya Manukato kutoka FPTC Nkuhungu Dodoma. Kwaya ya Vijana Usharika wa Kipawa Dar es Salaam. Kwaya ya Watoto wa Mungu Hananasif Dar es Salaam.

- Kwaya inatarajia kusafiri kwenda Usharika wa Tunduma, Usharika wa Mwakaleli

na Usharika wa Iringa Mjini. Aidha Kwaya inatarajia kwenda eneo la utalii la Kaporogwe kule Tukuyu.

13.3. Idara ya Muziki.

Idara hii inaongozwa na Mwl. Benedict E. Mwaijande ambaye ni Katibu akisaidiwa na Ndg. Evans Chattanda ambaye ni Mwenyekiti. Idara inaongoza Kwaya nne zilizo chini ya uangalizi wake. Kwaya hizo ni Uinjilisti, Safina, Hosiana, na Kwaya Kuu. Aidha Idara hii pia inaongoza kikundi cha kusifu na kuabudu kilicho chini ya uongozi wa Ndg. Edmund Temu akisaidiana na Bi. Edith Mboggo. Katika mwaka 2015 Idara hii imefanya yafuatayo:-

- Katibu amezitembelea kwaya zote zilizo chini yake ili kuwatia moyo na kufahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili.

- Katibu ameshirikiana na kwaya zote zilizo chini ya uangalizi wake katika kuandaa na kuadhimisha sikukuu za kuanzishwa kwa kwaya hizo zilizofanyika kwa nyakati tofauti tofauti.

- Wameshiriki tamasha lililoandaliwa na Jimbo kwa njia ya kwaya ya pamoja lililofanyikia katika Usharika wa Nzovwe.

- Katibu wa Kitengo aliandaa na kusimamia ratiba ya kwaya zetu kuhudumu kwenye Ibada.

- Katibu amehamasisha na kuimarisha kwaya ya pamoja. - Amekuwa pia akishirikiana kwa karibu na kikundi cha kusifu na kuabudu katika

huduma yao.

Page 14: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

14

- Amesimamia na kushirikiana na waimbaji katika maadhimisho ya sikukuu ya Muziki (Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kantate Domino) iliyofanyika tarehe 03/05/2015.

- Ameshirikiana kwa ukaribu na kwaya katika kupokea ugeni wa kwaya kutoka Sharika za Temboni kule Dar es Salaam na Engarenarok kule Arusha zilizotembelea Usharika wetu.

- Ameanzisha mchakato wa awali wa kununua sare za kwaya ya pamoja. - Idara imeshiriki katika matukio yote yaliyohusu Idara hii Kijimbo na Kidayosisi.

Changamoto za Idara hii. Katika mwaka 2015, Idara imekabiliana na changamoto zifuatazo:-

Ushiriki hafifu wa waimbaji katika kwaya ya pamoja. Baadhi ya waimbaji katika kwaya kutoshiriki ipasavyo katika semina za Neno la

Mungu zilizofanyika hapa Usharikani. Ushirikiano hafifu miongoni mwa kwaya zetu. Kudumaa kwa kiwango cha uimbaji kwa baadhi ya kwaya zetu. Kutokea kwa miingiliano ya matukio mbalimbali baina ya kwaya zetu. Hii ni

kutokana na uwingi wa kwaya zilizopo. Kukosekana kwa sare ya kwaya ya pamoja. Kukosekana kwa vyombo vya Muziki vya Usharika.

Malengo ya Idara kwa mwaka 2016. Idara hii inakusudia kufanya mambo mbalimbali kwa mwaka huu wa 2016. Miongoni mwa mambo hayo ni kama ifuatavyo:-

- Kufanikisha sikukuu ya uimbaji (KANTATE). - Kununua sare ya kwaya ya pamoja aina ya majoho. - Kuandaa semina mbili kwa ajili ya waimbaji na washarika wote. - Kufanya ziara za mara kwa mara kwenye kwaya zetu. - Kupokea taarifa za vikao vya kwaya kila baada ya miezi mitatu. - Kupeleka wanafunzi wasipopungua wawili kwa kozi ya Muziki. - Kupokea ugeni wa kwaya kutoka ndani na nje ya Dayosisi. - Kushiriki tamasha la Jimbo na mashindano ya uimbaji. - Kuhamasisha umoja na mshikamano miongoni mwa kwaya zetu. - Kushirikiana na kwaya zote katika maadhimisho ya sikukuu zao. - Kuushauri uongozi wa Usharika juu ya umuhimu wa kununua vyombo vikubwa

vya muziki. - Kuzielekeza kwaya zote juu ya umuhimu wa umoja na mshikamano katika

kumwimbia Mungu. - Kuandaa siku maalum kwa washarika ili waweze kutoa maoni yao kuhusiana na

hali ya uimbaji katika Usharika wetu.

Page 15: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

15

Kwaya ya Uinjilisti. Moto wa Kwaya: “Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”. Zaburi 150:6. Kiongozi wa kwaya hii ni Ndg. Peter Mwasandube ambaye ni Katibu akisaidiana na Ndg. Mathias Mbwanji ambaye ni Mwenyekiti. Kwaya inatoa shukrani kwa Wachungaji wote waliopita hapa Usharikani katika kipindi chote cha uhai wa Kwaya hii, nao ni Mchg. Geoffrey Mwakihaba (kwa sasa ni Msaidizi wa Askofu), Mchg. Lutengano Mwambene (marehemu sasa, apumzike kwa amani) na Mchg. Felix Mbogela aliyepo sasa. Wachungaji hawa wamefanyika baraka kwa Kwaya yetu kwa malezi yao mazuri. Aidha, shukrani za pekee ziwaendee Walezi wetu ambao ni Mrs. Rhoda Mgaya, Mhe. Upendo Sanga, Ndg. Benson Mrema, Ndg. Given Ngajilo na Eng. Patson Isote kwa kazi yao nzuri ya kuilea Kwaya. Katika mwaka 2015, kwaya imefanya yafuatayo:-

- Wamehamasisha watu wengi kujiunga na kwaya kutoka waimbaji 85 waliokuwepo na kufikia 91.

- Kwaya ilisafiri kwenda Jiji la Tanga katika Usharika wa Kana katika juma la Pasaka ya 2015.

- Walisafiri pia kwenda eneo la Shinzingo katika Kanisa la Babtisti. - Kwaya inamshukuru Mungu kwani Wanakwaya walio vyuoni kwa masomo

mbalimbali wanaendelea vizuri na wengine wamehitimu na kufaulu vizuri na baadhi yao wameajiriwa tayari.

- Kwaya imeendelea kuuza CD zao kwa mafanikio makubwa na kupata fedha kwa ajili ya maendeleo ya Kwaya.

Changamoto za Kwaya.

Uchumi wa Kwaya haujawa mzuri sana, hii ni kutokana na gari yao aina ya Coaster ambalo ndilo mhimili mkubwa wa uchumi wa kwaya kutopata safari nyingi. Lakini pia gari lao aina ya Canter kupata ajali hivyo kukwamisha mipango mingi kwani fedha nyingi zilitumika katika matengenezo.

Malengo ya Kwaya kwa mwaka 2016.

- Mwaka huu Kwaya ina mpango wa kukamilisha ununuzi wa vyombo vya vikubwa na vya kisasa vya muziki ili kuendana na hadhi ya Kanisa.

- Kuinua uchumi wa Kwaya kwa kuibua miradi mbalimbali na kuondokana na kutegemea mradi wa aina moja tu.

- Kuendelea kuwaombea na kuwatia moyo wanakwaya ambao hawajafunga ama hawajabariki ndoa zao, waweze kuzipeleka ndoa zao madhabahuni ili zipate uhalali wa kimadhabahu. Aidha wale ambao bado hawajapata wenzi, Mungu akakutane na haja hizo za mioyo yao.

Page 16: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

16

Kwaya ya Safina. Kwaya inaongozwa na Ndg. Simon Shalua ambaye ni Katibu akisaidiana na Ndg. Giliad Shang’a ambaye ni Mwenyekiti. Katika mwaka 2015 kwaya imefanya yafuatayo:-

- Wamefanya sikukuu ya kwaya iliyoambatana na tamasha. - Wamefanikiwa kushona sare nyingine ya Kwaya. - Wamefanya ziara katika Sharika za Iwambi, Sayuni, Bethania na Usharika wa

Kambasegela uliopo katika Jimbo la Kusini.

Malengo ya Kwaya kwa mwaka 2016. - Kwaya itafanya huduma ndani ya Jimbo mara tatu, nje ya Jimbo mara mbili na

nje ya Dayosisi mara moja na hiyo itakuwa mwezi Juni 2016. - Kwaya itaadhimisha sikukuu yake mwezi Juni 2016 pamoja na kuwa na

tamasha. - Mwaka 2016, kwaya imepanga kununua gari dogo litakalogharimu Tsh.

10,000,000= na tayari wanazo Tsh. 1,180,000=

Kwaya Kuu. Kwaya hii inaongozwa na Mrs. Hilda Kalinga Mwakasitu ambaye ni Katibu akisaidiana na Ndg. Twijulege Mwasyeba ambaye ni Mwenyekiti. Kwaya ina jumla ya waimbaji wapatao 30 lakini walio hai ni 20 (Me 6 na Ke 24). Katika mwaka 2015, Kwaya imefanya yafuatayo:-

- Wamefanya maadhimisho ya sikukuu ya kuanzishwa kwa Kwaya, siku ambayo iliambatana na tamasha la uimbaji. Lengo la sikukuu hiyo ilikuwa ni kupata fedha kwa ajili ya kununua Camera (Shooting Camera) kama mradi wa Kwaya.

Changamoto za Kwaya. Kwaya bado inakabiliwa mahudhurio hafifu ya waimbaji kutokana na matatizo

mbalimbali yanayowakabili. Kuyumba kwa uchumi miongoni mwa waimbaji na kusababisha kurudi nyuma.

Malengo ya Kwaya kwa mwaka 2016.

- Kununu Camera (shooting Camera). - Kununua gari aina ya Coaster. - Kununua sare. - Kuongeza waimbaji kwa njia ya kuwahamasisha. - Kwaya itasafiri kwenda Mbulu na Tunduma. - Aidha, kwaya itaalika wageni kutoka ndani na nje ya Dayosisi.

Page 17: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

17

Kwaya ya Hosiana. Kwaya hii inaongowa na Ndg. Jossam Mmbaga ambaye ni Katibu akisaidiwa na Ndg. Grant Mkosyange ambaye ni Mwenyekiti. Kwaya hii ina jumla ya waimbaji 15 tu. Kwa mwaka 2015, Kwaya imefanya mambo yafuatayo:-

- Wamefanya ziara katika Usharika wa Njisi Boder. - Wameshiriki tamaha la uimbaji katika Kanisa la Roman Catholic. - Wametembelea Usharika wa Betheli. - Wamepokea ugeni wa Kwaya ya Mwimbieni Bwana kutoka Usharika wa

Engarenarock kule Arusha. - Wameshona sare ya kwaya.

Changamoto za Kwaya.

Idadi ndogo ya waimbaji. Kwaya inatoa wito kwa Wakristo kujiunga na Kwaya.

Malengo ya Kwaya kwa mwaka 2016. - Kununua gari aina ya Hiace. - Kufanya huduma ndani na nje ya Jimbo kwa njia ya uimbaji. - Kushiriki uimbaji wa Kwaya ya pamoja ya Usharika chini ya Idara ya Muziki. - Kuadhimisha miaka 26 tangu kuanzishwa kwa Kwaya. - Kufanya huduma kwa njia ya uimbaji katika Sharika za Temboni kule Dar es

Salaam na Engarenarock kule Arusha.

13.4. Idara ya Elimu Ya Kikristo. Kiongozi wa Idara hii ni Mwinj. Aminieli Lazaro. Idara hii ndiyo yenye dhamana ya kushughulikia mambo yote yahusuyo Elimu ya Kikristo katika Usharika. Kwa mwaka 2015, Idara imefanya haya yafuatayo:-

- Idara imeendesha mafundisho ya Kipaimara na Ubatizo. Kipaimara walikuwa 41 (Wav. 14 na Was. 27).

- Elimu ya Kikristo imeendelea kufundishwa katika shule za msingi za Meta na Muungano tu.

Changamoto za Idara hii.

Changamoto ya walimu wa dini shuleni imekuwa sugu kwani walimu hujitokeza kwa muda na kukata tamaa tena.

Malengo ya Idara kwa mwaka 2016.

- Kuendelea kuwatia moyo walimu wanaojitolea kufundisha vipindi vya dini shuleni ili waendelee na kazi hiyo kwa moyo kwani ni muhimu sana kwa maisha ya kiroho ya watoto wetu huko shuleni.

Page 18: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

18

14.0. HUDUMA ZA KIROHO ZILIZOPO USHARIKANI. 14.1. Huduma ya MOMs.

Huduma hii inaongozwa na Mrs. Rhoda Mgaya ambaye ni Mwenyekiti akisaidiana na Mrs. Suma Mwaisango ambaye ni Katibu. Katika utangulizi wake, kiongozi wa huduma hii anamshukuru Mungu kwa neema yake ambayo ndiyo inamuwezesha kuifanya kazi hii aliyomkabidhi kupitia Wanawake wa MOMs na anasema “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?”. (Zab. 27:1). Kwa mwaka 2015 Huduma hii imefanya yafuatayo:-

- Wamefanya vikao vya mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka ili kujua maendeleo ya huduma hii.

- Wamekwenda Namanyere Mkoani Rukwa kufungua huduma ya MOMs huko na kuombea watoto, shule, vyuo, walimu, Kanisa na Taifa.

- Wameendelea na huduma ya kuombea watoto, shule, vyuo, walimu, Kanisa na taifa kila jumapili baada ya Ibada mnamo saa 11.00 jioni.

- Wamefanya huduma ya kuombea uchanguzi mkuu wa nchi yetu na uchaguzi wa Mkuu wa Kanisa (KKKT), lakini pamoja na mambo mengine yaliyohusiana na Usharika wetu kwa ujumla.

Changamoto za Huduma hii.

Matatizo waliyonayo watoto shuleni na vyuoni ni mengi lakini wanawake waombaji ni wachache.

Aidha, uhaba wa fedha ni changamoto nyingine inayoikabili huduma hii. Kutokuwa na fedha kumepelekea kushindwa kufikisha huduma katika Sharika za Katumba na Lwangwa ambazo zilikuwa zimelengwa mwaka uliopita wa 2015.

Malengo ya MOMs kwa mwaka 2016. Katika mwaka huu wa 2016, huduma ya MOMs imelenga kufanya yafuatayo:-

- Wanatarajia kufanya huduma kwa wanawake wachanga katika ndoa ili

wafahamu wajibu wao wa kuwapenda waume zao na kuwaombea watoto wao. Semina hii ilipangwa kufanyika mwaka uliopita wa 2015, lakini ilishindikana kutokana na mwalimu aliyetegemewa kupata matatizo ya kiafya.

- Wanatarajia kwenda kufungua huduma ya MOMs katika Sharika za Katumba, Lwangwa na Mwakaleli lakini pia katika nchi ya Msumbiji. Haya yote yatategemea upatikanaji wa fedha.

Page 19: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

19

14.2. Faragha ya Usharika. Faragha hii inaongozwa na Ndg. Mjuni Kyaruzi. Ibada ya Faragha hufanyika mchana mara baada ya Ibada za kawaida za siku ya Bwana lakini pia hata katikati ya wiki. Katika Faragha pamoja na huduma ya Neno, pia kunafanyika huduma za maombezi mbalimbali. Katika mwaka uliopita wa 2015, kulifanyika haya yafuatayo:-

- Kumefanyika Ibada chache za Faragha kwa Jumapili kadhaa. - Imefanyika mikesha ya maombi miwili. Mkesha wa kwanza ulikuwa ni kwa ajili

ya kuombea uchanguzi Mkuu wa nchi na Kanisa na mkesha wa pili umefanyika tarehe 31/12/2015 ambao ulikuwa ni wa mwaka mpya.

Changamoto Za Huduma hii:

Ushiriki hafifu sana wa Wakrito katika Ibada za Faragha hali iliyosababisha Ibada hizi kuzorota na hata kutofanyika kabisa katika Jumapili nyingi.

Malengo ya Faragha kwa Mwaka 2016.

- Kufufua Ibada za Faragha. - Kufanya mikesha ya maombi mingi zaidi. - Kuwa na semina za Neno la Mungu za mara kwa mara.

15.0. OFISI ZA MITAA YA USHARIKA.

15.1. Mtaa wa Forest. Mtaa unaongozwa na Mwinj. Anyitike Mwasakujonga. Mtaa unaundwa na vijiji saba vinavyoongozwa na Wazee kumi na wane. Kati ya hao Wazee wanaume wako sita na Wazee wanawake wako nane. Vijiji hivyo ni Forest, Meta, Forest Mpya, Usalama, Magereza, Mzumbe na TIA pamoja na kijiji kitarajiwa cha SAUT. Kwa mwaka 2015, kazi iliyofanyika ni:-

- Vimefanyika vikao vya Mtaa vinne tu kati ya kumi na viwili vinavyotakiwa kikatiba. Hii ni kutokana na wahusika na vikao hivyo kutohudhuria.

- Amefanya huduma ya mazishi. Wakristo waliofariki kwenye Mtaa huu kwa mwaka 2015 ni watatu nao ni Aneth Kasape na Mrs Mwakyoma wote kutoka Kijiji cha Meta na Joyce Masorini kutoka Kijiji cha Usalama.

- Ameshiriki na kuongoza Ibada za Vijiji katika Vijiji vya Forest Mpya, Magereza, Meta, Usalama na Forest Station. Katika Ibada hizo amekuwa akielekeza juu uendeshaji wa Ibada hizo kwa mujibu wa taratibu, kuhimiza mahudhurio na kutoa elimu kuhusu takwimu ya Wakristo.

- Aidha, alikutana na kufanya mazungumzo na Wazee wa Kijiji cha Meta na kupendekeza kwao wazo la kukigawa Kijiji hicho ili kurahisisha huduma kutokana na upana wa eneo lake na idadi kubwa ya Wakristo.

Page 20: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

20

- Ametembelea wagonjwa na waliopoa lakini pia alikutana na wanafunzi wa ubatizo Kijiji cha Magereza. Aidha, alihamasisha uandikaji wa takwimu kwa kila Mkristo katika kila Kijiji.

- Alitembelea na kufundisha darasa la watoto katika Mtaa wake tarehe 25/10/2015.

- Ibada za nyumba kwa nyumba katika Vijiji zimeendelea vizuri na kwa mafanikio mazuri.

Hapa chini ni taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka 2015 katika Vijiji vya Mtaa huu:- NA KIJIJI MAPATO MATUMIZI SALIO

01 KIJIJI CHA META 2,651,750= 1,213,000= 1,438,750= 02 KIJIJI CHA FOREST ST. 1,451,800= 1,093,000= 358,800=

03 KIJIJI CHA FOREST MPYA 1,953,300= 1,446,500= 506,800=

04 KIJIJI CHA USALAMA 230,000= 180,000= 50,000= 05 KIJIJI CHA MAGEREZA - - -

06 KIJIJI CHA MZUMBE - - - 07 KIJIJI CHA TIA - - -

08 JUMLA 6,286,850= 3,932,500= 2,354,350=

Malengo ya Mtaa kwa mwaka 2016.

- Kufanya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba. - Kufanya ziara katika Vijiji vya Mtaa. - Kuendelea kuhimiza umuhimu wa Ibada za nyumba kwa nyumba. - Kijiji cha Forest Station wanatarajia kufanya huduma ya kuwahudumia watoto

yatima.

15.2. Mtaa wa Sinde. Mtaa huu unaongozwa na Mwinj. Aminieli Lazaro. Mtaa unaundwa na Vijiji vitano vinavyoongozwa na Wazee kumi. Kati ya hao Wazee wanaume wako wane na Wazee wanawake wako sita. Vijiji vinavyounda Mtaa huu ni Sinde, Ilolo, Ilala, Ilamba na Maanga. Kwa mwaka 2015, Mwinjilisti amefanya haya yafuatayo:-

- Ameongoza na kusimamia vikao vya Mtaa. - Ameshiriki Ibada za mazishi. Wakristo waliofariki katika Mtaa wake kwa mwaka

2015 ni watano nao ni Tusajigwe Kyonya kutoka Kijiji cha Ilala, Lupakisyo Mbapa kutoka Kijiji cha Sinde na Godwin Mwakatobe, Rahabu Fungo na Elia Mwafyela wote kutoka Kijiji cha Maanga.

- Amewatembelea na kuwaona wagonjwa. - Amefanya usuluhishi mbalimbali. - Ibada za nyumba kwa nyumba katika Vijiji zimeendelea vizuri.

Page 21: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

21

Ifuatayo hapa chini ni taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka 2015 katika Vijiji vya Mtaa huu:-

NA KIJIJI MAPATO MATUMIZI SALIO

01 KIJIJI CHA SINDE 331,900= 289,000= 42,900= 02 KIJIJI CHA ILOLO 450,000= 250,000= 200,000=

03 KIJIJI CHA ILALA 214,800= 70,000= 144,800= 04 KIJIJI CHA ILAMBA 128,000= 101,100= 26,900=

05 KIJIJI CHA MAANGA 221,600= 123,500= 98,100= 06 JUMLA 1,346,300= 833,600= 512,700=

Changamoto za Mtaa.

Mahudhurio Ibadani huwa kidogo sababu watu wengi wana shughuli za kusafiri. Baadhi ya Wakristo kutokushiriki huduma za kiroho kwa sababu ya kutofunga

ndoa za Kikristo.

Malengo ya Mtaa kwa mwaka 2016. Kwa mwaka 2016, Mtaa umepanga kufanya yafutayo:-

- Kuwa na semina kwa Viongozi wa Vijiji. - Kufanya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba. - Kuwatia moyo waliopoa. - Kuendelea kuhamasisha Ibada za nyumba kwa nyumba.

16.0. MALENGO YA USHARIKA 2015.

Mwaka uliopita wa 2015 tulikuwa na malengo yaliyogawanyika katika makundi mawili kama ilivyo hapa chini:- 16.1. Malengo ya Kiroho.

Tulilenga kuimarisha Ibada za nyumba kwa nyuma katika Vijiji vyote na kwamba Ibada hizi zitakuwa zikifanyika kila juma. Kila kijiji kitachagua siku moja katika juma (isipokuwa Jumapili) itakayoona inafaa kwa Ibada ili kila nyumba ya Mkristo wa kijiji husika ifikiwe na Msalaba wa Kristo. Utekelezaji: Namshukuru Mungu kwani ibada zimeimarishwa na zinazendelea vizuri na kila Kijiji kinafanya ibada mara moja kwa kila juma. Naomba Ibada hizi ziendelee kufanyika vizuri na kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye muongozo wa ibada za nyumba kwa nyumba.

Aidha, tulilenga kufanya semina mbili za Neno la Mungu. Semina ya kwanza ilipangwa kufanyika kuanzia tarehe 19-26/04/2015, na mtumishi wa Mungu Mchg. Adamu Haji Mohamad kuhudumu katika semina hii. Semina ya pili ilitarajiwa kufanyika mwezi August na kuhudumiwa na Mtumishi wa Mungu Mwl. Mgisa Mtebe.

Page 22: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

22

Utekelezaji: Tunamshukuru Mungu kwamba tumefanya semina nyingi zaidi ya tulivyotarajia. Tulipanga kuwa na semina mbili tu, lakini kwa neema ya Mungu tumefanya semina kumi. Kati ya hizo, semina sita ziliandaliwa na Usharika, semina mbili ziliandaliwa na Idara zetu za Wanawake na Watoto na ile ya Malezi ya Vijana, wakati semina moja iliandaliwa na kutolewa na Baba Askofu na nyingine moja iliandaliwa na Mchg. Jacob Mwakatobe. Hivyo kwa mwaka 2015 tumekuwa na jumla ya semina zipatazo kumi.

16.2. Malengo ya Maendeleo.

Ilikuwa ni kuendelea kwa nguvu zote kujenga Hekalu la BWANA kwa mpango utakaoletwa na kamati husika. Utekelezaji: Tunamshukuru Mungu kwa kuijalia maono kamati yetu ya Ujenzi na Maendeleo pamoja na ile ya Ujenzi. Tulikuwa na awamu mbili za kutoa sadaka zetu kwa kazi hii. Awamu ya kwanza ilikuwa kati ya mwezi March hadi Juni 2015 na awamu ya pili ilikuwa kati ya mwezi August hadi Desemba 2015. Matokeo ya maono haya ndiyo yaliyotuwezesha kupata jumla ya Tsh. 100,020,600=, ambazo ndizo zimetufikisha katika hatua hii tunayoiona sasa.

17.0. MALENGO YA USHARIKA MWAKA 2016. 17.1. Malengo ya Kiroho.

Kwa mwaka huu wa 2016, tumepanda kufanya semina za Neno la Mungu zipatazo tano kwa mpango ufuatao hapa chini:- Tutafanya semina ya kwanza ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2016

itakayoendeshwa na Ndg. Aminiel Issa tarehe 01-03/01/2016. Tutafanya semina ya pili katika juma la Pasaka tarehe 20-27/03/2016

itakayohudumiwa na Mchg. Zakayo Malekwa na Ndg. Nuhu Mkirumi. Tutafanya semina ya tatu itakayoendeshwa na Mchg. Longan Rein

(Mwisrael) kutoka Arusha inayotarajiwa kufanyika tarehe 19-26/06/2016. Tutafanya semina ya nne tarehe 07-14/08/2016 itakayohudumiwa na

Ndg. Mwanri kutoka Arusha. Na tutafanya semina ya tano katika juma la Krismasi tarehe 25-

31/12/2016 itakayoendeshwa na Ndg. Landa kutoka Dar es Salaam.

Kutoa mafundisho juu ya theologia ya Ibada.

Kutoa mafundisho juu ya Zaka na kuona namna mpya ya utoaji wa Zaka yaani kutoa mara moja kila mwezi.

Kuendeleza huduma ya maombezi kwa makundi mbalimbali katika Usharika.

17.2. Malengo ya Maendeleo. Kukamilisha ujenzi wa HEKALU la BWANA kwa mpango utakaoletwa na kamati husika.

Page 23: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

23

18.0. HITIMISHO. Narudia namshukuru Mungu kwa neema na upendo wake lakini pia uzima na afya avyotujalia kila siku.

- Nawashukuru timu ya Waombaji kwa huduma yenu njema ya kutuombea watumishi, kuliombea Kanisa, kuliombea Taifa letu na kuombea kazi ya Mungu katika Usharika wetu. Kazi yenu hii kubwa isiyoonekana kwa macho, ndiyo sababu ya mafanikio mengi tunayoyaona sasa katika Usharika wetu. Nawaomba sana, endeleeni kutumika kwani huduma hii ni muhimu sana kwa maisha ya Watumishi na Kanisa. Mungu kupitia kinywa cha Mtume Paulo anasema:- “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena”. Kol. 4:2-4.

- Namshukuru Mkuu wangu wa Jimbo Mchg. Andindilile Mwakibutu kwa kunishauri, kunielekeza na kuniongoza katika utendaji wa huduma hii ya Kichungaji. Shukrani hizi pia zimfikie Msaidizi wa Mkuu wa Jimbo Mchg. Mmenye Mwasampeta kwa msaada na ushauri wake wa busara kwangu.

- Nawashukuru Wachungaji wenzangu wote wa Jimbo hili kwa jinsi tunavyoshirikiana na kusaidiana katika utumishi huu tulioitiwa.

- Namshukuru Katibu Mtunza Hazina wa Jimbo na Makatibu wa Idara katika Jimbo kwa ushirikiano wao mzuri katika mambo mbalimbali ya Kijimbo tunayokuwa nayo.

- Namshukuru Mwanafunzi wa Uchungaji Mtheol. Ambonisye Kajange kwa kazi kubwa anayoifanya. Hakika amefanyika baraka sana katika huduma yangu. Mara nyingi nimekuwa nikimwachia majukumu mengi na mazito na anayafanya kwa moyo tena pasipo kuchoka. Baraka za Mungu ziwe pamoja naye wakati wote.

- Nawashukuru watumishi wenzangu Wainjilisti ambao ndiyo wasaidizi wangu kwa ushauri na msaada wao kwangu. Wanafanya kazi kubwa ya kuongoza Mitaa, kufundisha Kipaimara na mambo mengine mengi ya kiutumishi. Mungu awabariki.

- Namshukuru Katibu Mtunza Hazina kwa ushirikiano wake kwangu, namshukuru Parish Worker kwa huduma yake ya kutunza Ofisi na mambo yote yanayohusiana na Ibada lakini pia ushirikiano anaotoa kwangu.

- Nawashukuru Viongozi wa Idara wote na Viongozi wa Kwaya zote kwa jinsi tulivyoshirikiana, naomba tuendelee hivyo kwa mwaka huu pia.

Page 24: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

24

- Wazee wa Kanisa, Madikoni, Wazuru na Wajumbe wote wa Halmashauri ya Usharika pamoja na Kamati ya Utendaji na kamati nyingine zote, pokeeni shukrani zangu za dhati kwa umoja na mshikamano mliouonesha katika kumtumikia Mungu. Endeleeni na moyo huo.

- Nawashukuru walimu wa watoto wetu wa shule ya jumapili kwa kazi yao njema sana wanayoifanya ya kuwaelekeza watoto wetu katika kumjua Mungu wetu wangali wadogo. Wanafanya kazi muhimu sana kwa Kanisa, kubwa na nzito tena kwa kujitolea. Naomba niwatambue kwa majina watumishi wa Mungu hawa ambao ni Ndg. Furaha Mwifyusi ambaye ndiye kiongozi wa walimu hao, Mrs. Mariam Ihola Mwamupwa, Ndg. David Bariki na Ndg. Yona Mwaisango. Wengine ni Mrs. Edina Yohana, Mama Nelusigwe Lupembule, Bi Tatu Mwinuka na Ndg. Issa Sanga. Neno la Mungu katika Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli linasema:- “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataicha, hata atakapokuwa mzee”. Mithali 22:6.

- Aidha, namshukuru mtumishi wa Mungu Jestina Ndambo kwa kazi kubwa na nzito anayoifanya ya kuhakikisha eneo letu linakuwa katika hali ya usafi wakati wote.

- Naishukuru Kampuni yetu ya Ulinzi ya BERMIC SECURITY SERVICES COMPANY LTD chini ya Mkurugenzi wake Ndg. Cyprian Lugazia kwa kazi yao kubwa ya kulinda eneo hili usiku na mchana.

- Nawashukuru watumishi wa Mungu wanaofanya kazi kubwa ya usafi Kanisani kila siku ya Jumamosi. Watumishi wa Mungu hawa ni Mrs. Suma Mwaisango na Mrs. Maria Mwandugulile. Mungu awabariki kwa huduma yao hii.

- Nazishukuru Kwaya zote pamoja na timu ya Kusifu na Kuabudu kwa huduma kubwa mliyoifanya mwaka uliopita na mnayoendelea kuifanya sasa ya kumhubiri Kristo katika Ibada zetu hapa Usharikani na hata nje ya Usharika wetu. Huduma yenu hii ya uimbaji ni muhimu sana katika Kanisa kwani wengi wanaokolewa na kuponywa kupitia nyimbo zenu. Neno la Mungu linasema “...Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa”. Ebr. 2:12.

- Naishukuru timu ya wapishi wetu jikoni wakati tunapokuwa na ugeni hapa Usharikani. Wamama hawa walio chini ya uongozi wa Wanawake, wanafanya kazi nzuri sana tena kwa moyo. Hakika wanaupa heshima Usharika wetu kwa chakula kizuri na kitamu wanachowaandalia wageni wetu.

- Aidha, nawashukuru vijana wetu wanafunzi wa Mzumbe, TIA, SAUT, CBE pamoja na watoto wetu kutoka Sekondari ya Sangu kwa ushiriki wao pamoja nasi katika Ibada zetu hapa Usharikani. Hakika tunabarikiwa sana na uwepo wao.

Page 25: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

25

- Nawashukuru Washarika wenzangu wote kwa kujitoa kwenu kumtumikia Mungu, mmekuwa baraka sana katika huduma yetu, mmetutia moyo na mmeuitikia kwa moyo wito wa Bwana wa katumika katika Kanisa lake. Aidha, mimi binafsi na kwa niaba ya mke wangu na watoto wetu, tunawashukuru sana kwa jinsi mnavyotuombea na mnavyotunza maisha yetu. Kila siku tunashuhudia ukarimu wenu mkubwa kwetu. Mungu awabariki.

- Mwisho, lakini kwa umuhimu mkubwa na wa pekee kabisa, namshukuru sana Mke wangu Jestina na watoto wetu wapendwa, kwa kuniombea, kunishauri na kunitia moyo katika huduma hii.

Kwa unyenyekevu mkubwa nawaomba muipokee taarifa hii, ikiwa ni matokeo ya kazi kubwa tuliyowezeshwa na Mungu kuifanya katika Usharika wetu wa FOREST kwa mwaka wa 2015. “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”. 1Pet. 5:6-7. Kwa heshima na unyenyekevu, naitoa kwenu. USHARIKA WA FOREST – KKKT/DKO. ................................... Mchg. Felix Mbogela. KIONGOZI WA USHARIKA. Nakala: Mkuu wa Jimbo.

Taarifa hii inapatikana pia katika tovuti ya Kwaya yetu ya Uinjilisti kwa anuani ya

www.uinjilistiforest.org

Page 26: EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA …uinjilistiforest.org/wp-content/uploads/TAARIFA-YA...Sakramenti ya Meza ya Bwana tarehe 01/02/2015. Tumewapokea Viongozi wa Kitengo cha Vijana

26