Upload
others
View
5
Download
0
Embed Size (px)
Citation preview
© Boston University
LANGUAGE PROGRAM, 232 BAY STATE ROAD, BOSTON, MA 02215 www.bu.edu/Africa/alp
[email protected] 617.353.3673
Chovya chovya humaliza buyu la asali: Mazoezi
Zoezi la 1: Toa maana ya msamiati huu
i) Kuwahi ii) Hongera
iii) Kabati
iv) Vyombo v) Kuzunguka
vi) Kitenge
vii) Kuacha viii) Shoga
ix) Sogea x) Kifuta jasho
Zoezi la 2: Tumia maneno hayo juu katika sentensi kisha utafsiri
Zoezi la 3: Jibu maswali haya
i) Baba Chaurembo alipata nini kazini? ii) Baba na Mama chaurembo walipanga kutumia vipi fedha zile?
iii) Mama Chaurembo alifanya nini badala yake?
iv) Unafikiri mama Chaurembo ni mwanamke mwenye tabia gani? v) Je Unafikiri jina la mama chaurembo lina mfaa au vipi?
Zoezi la 4: Jibu kweli au Si kweli
i) Mama Chaurembo alipenda sana urembo ii) Baba Chaurembo hakumwamini mkewe
iii) Mama Chaurembo alikuwa na tamaa
iv) Kabati la vyombo lilitengenezwa kwa haraka v) Mama chaurembo alifikiri fundi atachelewa kumaliza kabati
2
vi) Mama chaurembo alikuwa mtu mwenye kujipenda sana
vii) Methali ya chovya chovya huonyesha watu wasio kuwa na kiasi
Zoezi la 5: Kelezea maana Elezea maana ya methali hii “Chovya chovya humaliza buyu la asali” kama
Ilivyotumika katika hadithi hii.
Zoezi la 6: Muhtasari
Andika Muhtasari wa igizo hili kama unamwadithia mtu mwingine.
Zoezi la 7: Kulinganisha na Kutofautisha Linganisha kisha tofautisha methali hizi mchovya hachovi mara moja na chovya chovya humaliza buyu la asali
Zoezi la 8: Jibu Swali hili
Taja methali au msemo wa Kiingereza unayofanana na methali hii
Unaweza kuelezea methali hiyo hutumikaje?
Zoezi la 9: Jibu Swali hili Andika kisa kifupi kuelezea methali “Chovya chovya humaliza buyu la asali
Zoezi la 10: Jibu Swali hili Jaribu kuigiza methali hii ili kufanya mazoezi